Ipo tofauti. Zile Nyaraka za 2010 za Kanisa Katoliki kama kaulimbiu ya kuwaandaa waumini kwa uchaguzi mkuu, na hata ule wa karibuni zaidi ambao Kardinali Pengo aliukana, zilitolewa na kamati za Baraza la Maaskofu. tofauti ni kwamba ile inakuwa imeidhinishwa na askofu mhusika wa kamati. hapo utaona jina la Askofu mmoja tu ambaye ndiye mkuu wa Kamati husika. na pia Waraka unakuwa na nguvu ya kushauri tu, si wa kimamlaka kwa nchi nzima. ndio maana Pengo aliukana bila kuwa na wasiwasi.
Huu wa sasa umetolewa na Baraza lenyewe la Maaskofu na wameusaini Maaskofu wote wa nchi nzima. hapo sasa waraka huu una nguvu za kutumika kama nyenzo ya uinjilishaji kwa taifa zima. Ni kauli rasmi ya Kanisa Katoliki Tanzania na Maaskofu wote kwa kweli wanalazimika kuuheshimu. Ni tofauti kubwa sana na Historia imeandikwa.