WARAKA: Maaskofu Katoliki waonya uminywaji wa demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari nchini

WARAKA: Maaskofu Katoliki waonya uminywaji wa demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari nchini

Toa povu liishe kabisa. I can guess wewe ni mmoja wa waliotumbuliwa. MUACHE RAIS APIGE KAZI. Period!
Sina povu, huyu jamaa aliomba hii kazi kwa kubembeleza hadi kupiga push-up, hatumwachii ng'o, hadi kieleweke. Mimi sijatumbuliwa, lakini haizuii kuona kinachoendelea. kutumbua siyo ishu. ishu ni je nchi yetu inakwenda mbele? gharama nyingi zinatumika kwa mambo ya kijinga kama "uchaguzi wa marudio" ambao hauna sababu kabisa. labda afunge mitandao, lakini tutaendelea kula naye sahani moja
 
"Waraka" ambao kiukweli ni "UJUMBE WA KWARESIMA" una sura nne, mbona mnadandia mada? Kwanini msisome na sura nyingine?
NI kweli kabisa, kuna ujumbe mzito sana katika waraka huu wa Kwaresima, mbali na hayo ya kisiasa. Lakini kwa sababu ni mara ya kwanza wameongelea haya ya siasa, kwa kiwango hiki, katika ujumbe wa Kwaresima, ndio maana mjadala wake umechukua muda mrefu. lakini pia hata ukiangalia ile nukuu ya biblia waliyotumia "Kwani mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?" ni aina ya nukuu ya kimapinduzi, ambapo Maaskofu wanaona tatizo letu watanzania la kutojali mambo yanavyokwenda katika nchi yetu. Katika nchi nyingine tendo la Lissu kupigwa risasi vile ingeleta kashi kashi kubwa sana katika nchi. watu kuzuiliwa kusali kumuombea, kuchangia damu. lakini hapa kwetu watu wapo wapo tu. kwa hiyo kwa vyovyote ujumbe wa Kwaresima mwaka huu ni WAKE UP CALL na hasa imejikita sana katika mambo ya siasa. kwa hiyo mjadala kama huu ni sawa kabisa
 
Ni kama unafiki;
Watu pekee wanaoweza kusikilizwa kirahisi na rais ni viongozi Wa dini;
Maaskofu kila siku wapo na rais huko makanisani wanashindwaje kumkanya? Mtu ambaye kila jumapili mpo naye kanisani sioni haja ya kupoteza sadaka za waumini kukaa kikao ili kuandaa waraka Kwa ajili ya kufikisha ujumbe.
Pamoja na nia ya kuwasemea wananchi, maaskofu wanao uwezo Mkubwa Wa kuomba appointment ya kumuona rais na kumwambia!.

Nashauri rais asipoteze mda kuwajibu maana wameonyesha unafiki;
Haiwezekani mtu unakaa naye meza moja ukamwandikia barua kupitia njia ya Posta!

VIONGOZI WA DINI NDIO ZAO LA KUPATA VIONGOZI HAWA TULIONAO
Hawajamwandikia Rais, Huu ni waraka kwa waumini wakatoliki. lakini ndani yake kuna ujumbe mkali sana unaoelekezwa kwa Serikali, na unawataka waumini kuyajadili haya kama vile yanawahusu, wasitoe visingizio kama vya Kaini aliyemwua nduguye.. Hiyo Moja.

Pili, inawezekana kabisa Maaskofu wamewasilisha serikalini mawazo yao, na inawezekana kabisa utawala huu umepuuza. lakini Maaskofu wanawajibika kwa waumini wao, ndio wachungaji, hivyo unaweza kujiuliza mbona wamekaa miaka 2 ndio wanakuja kutoa kauli? na kwa kweli wengine wanawalaumu kwa kungojea mpaka hali imefikia kiasi hiki. Lakini huwezi jua kilichokuwa kinaendelea nyuma ya pazia. kwa hiyo usilaumu tu, ila ni haki kujadili kile ambacho hatimaye wametuletea.

Rais awajibu, asiwajibu, ujumbe umefika siyo kwa Rais tu, bali kwa taifa zima ndani na nje ya nchi yetu. matokeo yake mijadala imeendelea nchi nzima ndani na nje, na impact yake hakika itakuwa kubwa.
 
Umesoma sura zote nne za "UJUMBE WA KWARESIMA"? Usiandike ili kupata likes za JF bali kuelimisha. soma Sura ya kwanza "BASI ENENDENI", Sura ya pili "SASA NI ZAMU YETU" Sura ya tatu "MIMI NI MLINZI WA NDUGU YANGU?" Sura ya nne "NIMRUDISHIE BWANA NINI?" hapo utapata ujumbe kamili waliotaka jamii iupate na kuufanyia kazi.
Hivi unajua maana ya NEWS? Maneno ya Kichungaji huwa tunayasoma mara kwa mara, lakini pale Maaskofu wanaamua kutoa ujumbe mkali wa kisiasa, tena kwenye charged atmosphere kama hii ya kwetu kwa sasa hivi, ni lazima moto uwake tu. kuna hali tete nchini hivi sasa, na Maaskofu wanaongelea "Kusoma Alama za nyakati" Ni Maaskofu wenyewe walioamua kuweka ujumbe mkali sana wa kisiasa katika Waraka wao wa Kwaresima. ni kauli ya kwanza kutolewa na Baraza la Maaskofu tangu limeanzishwa, kauli kali kwa kiwango hiki, tena umesainiwa na Maaskofu wote. Ni statement ya Kanisa Katoliki Tanzania. Ni Historia. sasa ni bahati mbaya kwamba hayo yamewekwa katika Waraka wa Kwaresima, ambao bila shaka una mambo mazito ya kiroho kama unavyosema. lakini bado hata katika Nukuu yao ya Biblia: "Kwani mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?" wamechagua nukuu ya kimapinduzi, inayowaamsha walengwa waamke na kuchukua hatua. tunaweza kujadili zaidi hili katika muktadha wa kidini, lakini bado overtones kubwa zaidi ni za kisiasa, tena zikilenga taifa zima la Tanzania, siyo waamini tu.

Unaweza pia kusema Maaskofu wametonesha kidonda. Wanaongelea kuzuiliwa mikutano ya vyama vya siasa, kufungiwa vyombo vya habari, na wanatamka bila kupepesa macho: HUU NI UKIUKWAJI WA SHERIA NA KATIBA. Halafu ipite hivi hivi tu? Katika mazingira ambayo mtu mwingine aliyekosoa vikali serikali, alipigwa zaidi ya risasi 38, na bado anauguza majeraha nje ya nchi, na serikali imegoma kumtibu ikidai eti taratibu hazikufuatwa. hivi unapookoa maisha ya mtu unafuata taratibu gani? maana hata AMBULANCE HAIFUATI TAA NYEKUNDU WALA NJANO, NI MOTO CHINI KUOKOA MAISHA YA MTU. sasa Serikali inataka kwa suala la Lissu AMBULANCE ifuate foleni????

Katika mazingira ambayo Ben Saanane alipokosoa Digrii ya Mkulu, amepotea. yule mwandishi wa gazeti la Mwananchi naye kapotea, alikuwa anaandika vitu ambavyo serikali haipendi. Katika mazingira ambayo Askofu wa Kanisa Katoliki, Askofu NiweMugizi, anasumbuliwa na vyombo vya dola kuhusu uraia wake, baada ya kujitokeza kudai Katiba mpya, jambo ambalo Mkulu amesema hataki kusikia. Katika mazingira ambayo Askofu Kakobe aliyehoji mambo kadhaa ya serikali, ameishia kuchunguzwa na TRA kama hana miradi ambayo haijalipiwa kodi, na akasachiwa hadi chupi za mkewe, midume inatafuta miradi sijui miradi gani kwenye chupi za mama Askofu???

Katika mazingira hayo yote, wanajitokeza Maaskofu ambao wanaikosoa serikali hii ya kibabe, lazima pia kuwe na TAHARUKI. hawatahojiwa uraia? hawatapekuliwa? hawatapelelezwa miradi isiyolipiwa kodi? Lazima kuwe na TAHARUKI.
 
Mtoa mada ina wezekana hujitambui, na yanayofanyika katika serikali na chama tawala yako juu ya uwezo wako kifikra,
Nakubaliana na wewe, yatakuwa yako juu ya uwezo wangu. Maana kubomolea nyumba wajane, wenye watu wanaowategemea, unawabomolea nyumba pamoja na vifremu vyao vinavyowaendeshea maisha, halafu unaona hayo ni maendeleo, kwa kweli hilo linapita uwezo wangu.

Kujenga ma-fly-ova ambapo sasa tunaambiwa yanakuja mengine saba, ambayo ni namna ya gharama kubwa ya kupunguza foleni na ni ubishoo kwa nchi kama yetu, wakati uchumi unadorora, huwekezi kwenye uzalishaji, ila unakaba watu koo walipe kodi bila uhalisia, hayo ni mambo yanapita uwezo wangu.

Kuanzisha mradi wa gharama kubwa wa kuhamia Dodoma wakati ni nje ya bajeti, na wakati siyo priority kwa sasa hivi, ni jambo ambalo liko juu ya uwezo wangu.

Kujenga uwanja wa ndege kubwa Chato ili kumfurahisha mkulu, kwa kutumia mabilioni ya fedha za watanzania walalahoi wasiombele wala nyuma, hilo linapita uwezo wangu.

Kubomoa maghorofa ili tu kumkomoa fulani, kwa gharama kubwa na kuathiri utendaji wa shirika kubwa, hilo linapita uwezo wangu.

Kununua chap chap ndege, na kuendesha shirika kwa hasara kwa miaka mitatu sasa, lakini bora liende, na sisi tuonekane tuna ndege, yote hayo yako juu ya uwezo wangu. Yapo mengine mengi tu sana tu, ambayo kwa kweli siyaelewi naona yanapita uweze wangu wa kufikiri
 
Huu ni msumari wa moto kwa dikteta uchwara...najua kuna wawakilishi wake humu...hakikisha habari hizi anazipata kwa wakati. Kama hawezi kusoma, muweekee kwenye audio akasikilize. Katika sako la nyani, ngedere hawabaki salama. Message sent and delivered to hothead at white house.
 
rais wangu piga kazi. hachana na mbwembwe hizo. Serikali haiendeshwi kwa madongo madongo kama hayo. Kwani wao wanaujua mzigo raais alionao? watu wafanyekazi. Siasa mpaka 2020
Mavi yako huyo raisi anakupa nn wewe?
 
Kama najiona Jumapili navoingia kanisani misa ya kwanza kabisa kwa bashasha na moyo mkunjufu
IMG-20180215-WA0005.jpg
 
Sina povu, huyu jamaa aliomba hii kazi kwa kubembeleza hadi kupiga push-up, hatumwachii ng'o, hadi kieleweke. Mimi sijatumbuliwa, lakini haizuii kuona kinachoendelea. kutumbua siyo ishu. ishu ni je nchi yetu inakwenda mbele? gharama nyingi zinatumika kwa mambo ya kijinga kama "uchaguzi wa marudio" ambao hauna sababu kabisa. labda afunge mitandao, lakini tutaendelea kula naye sahani moja
Nchi inakwenda mbele. discipline inakuwepo kati ya walionacho na wasiokuwanacho. Heshima inakuwepo. Hizo gharama unazolilia ni sheria ndo inafuatwa. mbunge au diwani akijiuzuru kuwepo na uchaguzi mwingine. shida nini? hii mihemuko ni shida sana. Sasa na yale mabilioni ya EPA na ESCROW huoni kuwa ni gharama tena pesa za walipa kodi? Muache atunyooshe bana.
 
Nchi inakwenda mbele. discipline inakuwepo kati ya walionacho na wasiokuwanacho. Heshima inakuwepo. Hizo gharama unazolilia ni sheria ndo inafuatwa. mbunge au diwani akijiuzuru kuwepo na uchaguzi mwingine. shida nini? hii mihemuko ni shida sana. Sasa na yale mabilioni ya EPA na ESCROW huoni kuwa ni gharama tena pesa za walipa kodi? Muache atunyooshe bana.
Hivi unaelewa unachoandika wewe..???
 
Back
Top Bottom