Gavana
JF-Expert Member
- Jul 19, 2008
- 33,637
- 8,947
Uliyenijibu ni mimi na hakuna mahali nimeandika hayo unayoyasema.
weka hapa uliandika nini ???
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Uliyenijibu ni mimi na hakuna mahali nimeandika hayo unayoyasema.
Mimi mwenyewe nimepinga sana kitendo cha Kanisa Katoliki kurudi nyuma katika kupigania haki za watanzania. Ila ninachofanya ni kuwa realistic. Kuhusu Katiba aliyevuruga ni Jakaya Kikwete baada ya kugeuka nyuma, sijui alionywa na akina Mkapa? Kanisa Katoliki lilifanya kazi kubwa sana, ingawa Kardinali Pengo alivunja nguvu jitihada hizo. lakini mvunjaji hasa ni Kikwete mwenyewe aliyeanzisha huo mchakato toka mwanzo.
Unasema madhehebu mengine yamekuwa yakikemea toka mapema? siyo sahihi! Ni juzi tu wakati wa Krismasi ndio Maaskofu walianza kukemea, nao ni KKKT na Katoliki. kabla ya hapo ilikuwa kimya kabisa. Lakini hata hivyo tofautisha kemea ya Askofu mmoja mmoja, na kauli ya Kanisa zima ambayo ni rasmi. hakuna dhehebu la kikristo wala waislamu ambao wametoa kwa kiwango hicho.
Unauliza Waraka unasaidia nini, kwa kweli hakuna chochote kinachoweza kumzuia JPM kufanya chochote anachotaka hivi sasa. isipokuwa, unapokuwa na Maaskofu wametoa tamko kama hilo, unaondoa ule uhuru wa serikali kuongea kwa kujinasibu. it is on the defensive. hiyo inapunguza kasi yake ya kutenda maovu. pia inagalvanise opposition both from outside and inside. pia taarifa kama hizi zinasaidia vyombo vya nje ambavyo vinaweza kufuta baadhi ya mikataba kutokana na kutoridhishwa na hiki au kile. Kumbuka pia kwamba Madikteta wote wanapenda kusikika vizuri. hivyo publicity kama hii inawakera sana, na watajitahidi kuiepuka. hiyo itatusaidia. pia angalau tutashuhudia kupungua kwa "ziara za Rais katika Makanisa na hotuba za kwenye mimbari" huku akiomba "kuombewa". haituongezei ubwabwa lakini angalau inatupunguzia kero.
"Waraka" ambao kiukweli ni "UJUMBE WA KWARESIMA" una sura nne, mbona mnadandia mada? Kwanini msisome na sura nyingine?Hao maaskofu wa kanisa katoliki Tanzania ni wasemaji maneno matupu bila matendo kama wenzao wa nchi ya DR Congo.
Waraka wa wajumbe TEC ni kelele za debe tupu hayana athari kwa serikali yao kama mnavyoona sasa kinachoendelea nchini.
Mara nyingi nyaraka za wakatoliki huwa zinatetemesha sana serikali
Mambo ya kiroho ni pamoja na kukanya, kushauri na kuonya! Huo sio waraka ni Wa maaskofu maana yake ni Wa kidini. Kanisani kaenda kusali sio mahijiano
Toa povu liishe kabisa. I can guess wewe ni mmoja wa waliotumbuliwa. MUACHE RAIS APIGE KAZI. Period!Tatizo ni kwamba hii siyo nchi ya mtu mmoja. MUACHENI AFANYE KAZI! Hakuna anayetaka wala hakuna anayeweza kumzuia Rais kufanya kazi, ila yeye ndiyo hataki wengine wafanye kazi. Hataki vyama vya siasa vifanye kazi wala hataki mihimili ifanye kazi yake kwa mujibu wa katiba.
Yaani unawezaje kumzuia Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kufanya kazi? wewe ni nani? Inavyoonekana Amiri jeshi huyu wa sasa wa Tanzania ana hofu kiasi kwamba hata chama cha siasa kisichokuwa na jeshi wala silaha, anakiogopa. Hii nchi ina Taasisi na mifumo mbalimbali ambayo yote inatakiwa kufanya kazi. Kuna taratibu za kikatiba za watu kukosoa na kupongeza, na kwa ujumla kutoa mawazo yao. Kuna mihimili ya Bunge, Mahakama, na Serikali, ambayo kila moja ina kazi yake na majukumu yake.
Amiri Jeshi wetu ni mwoga sana kiasi hataki mihimili mingine ifanye kazi yake kwa kujitegemea na uhuru kwa mujibu wa Katiba. anataka awe yeye tu. Na hata alivyosema hakuna siasa mpaa 2020, mwenyewe ameendekeza siasa tena za kijinga, kwa kukwapua wabunge waliochaguliwa na wananchi, na kuwalazimisha warudi tena kwenye uchaguzi! Ndiyo kuchapa kazi huko? kutuingiza hasara za kijinga?
Na bado ana mashitaka mengi tu. hiki kitendo cha kuruhusu ubaguzi wa kiitikadi, kiasi kwamba viongozi wanadiriki kutamka hadharani kwamba ukichagua mtu wa CCM ndio mtapata maendeleo, wakati fedha ni zetu sisi wote, Serikali ni mgawaji tu, huo ni UHAINI. Na ni DHAMBI KUBWA SANA. MAGUFULI ANATAKIWA KUTUBU.
Mwisho, kauli ya Maaskofu siyo ya kubeza. wameitoa iikiwa miaka miwili imepita ya serikali hii. hawakuwa na haraka, wengi wamewalaumu kwa kukaa kimya muda mrefu. wamejitafakari kabla ya kuitoa. Magufuli ajipange, ajipime. Kuwabeza viongozi wa dini pale wanaposimama kwenye UKWELI, NI JAMBO LA HATARI SANA.