Waraka No. 1 wa China wasisitiza kujenga nchi yenye nguvu kubwa ya kilimo

Waraka No. 1 wa China wasisitiza kujenga nchi yenye nguvu kubwa ya kilimo

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
VCG111324971061.jpg
Hivi karibuni serikali kuu ya China ilitoa waraka No. 1 wa mwaka huu kuhusu suala la kilimo. Huu ni mwaka wa 20 mfululizo, ambapo China imetoa waraka No.1 kuhusu kilimo, na jambo ambalo linaonesha kuwa suala hili limepewa kipaumbele zaidi nchini China. Mwaka huu, kwa mara ya kwanza waraka huo umesema China itajenga nchi yenye nguvu kubwa ya kilimo.

China ina ustaarabu wa muda mrefu wa kilimo. Miaka elfu sita iliyopita, kilimo lilianza kustawi kwenye Bonde la Mto Manjano na Bonde la Mto Yangtze, na kilimo ndio chimbuko la ustaarabu wa Kichina. China ina watu bilioni 1.4, na kati yao takriban milioni 300 wanajishughulisha na kilimo, na kwa miaka mingi iliyopita, China imeshika nafasi ya kwanza duniani kwa utoaji wa nafaka, mboga, matunda, nyama, samaki na mazao mengine ya kilimo.

Hata hivyo, ikilinganishwa na sekta za viwanda na huduma ambazo zimeendelea kwa kasi katika miongo kadhaa iliyopita nchini China, kilimo bado kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo tija ndogo ya nguvukazi vijijini, njia isiyofaa ya matumizi ya rasilimali, na uwezo mdogo wa ushindani katika soko la kimataifa.

Mwaka 2022, ripoti iliyotolewa kwenye mkutano mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China iliweka lengo la kuijenga China kuwa nchi ya kisasa ya ujamaa yenye nguvu kubwa katika pande zote. Kilimo ndio msingi wa nchi yenye nguvu, na ili kufikia lengo hilo, China inapaswa kuendeleza kilimo kwa kuchukua hatua madhubuti.

Uamuzi wa China wa kujenga nchi yenye nguvu kubwa ya kilimo pia unatokana na mazingira ya kimataifa. Katika miaka ya hivi karibuni, hali ya kimataifa imebadilika kwa kiasi kikubwa, na suala la usalama wa chakula linafuatiliwa sana na jumuiya ya kimataifa. China ni nchi yenye idadi kubwa zaidi ya watu duniani, na ni muhimu kwake kuhakikisha usalama wa chakula. Hivi sasa teknolojia nyingi za hali ya juu za kilimo zinamilikiwa na nchi za magharibi. Katika siku zijazo, China itajitahidi kuendeleza kilimo, na kuboresha uwezo wake wa ushindani katika soko la kimataifa.

Ili kujenga nchi yenye nguvu kubwa ya kilimo, ni lazima kuongeza mapato ya wakulima. Juhudi za China za kupunguza umaskini imepata mafanikio makubwa, lakini umaskini vijijini bado haujaondolewa kabisa. Kutokana na waraka NO. 1 wa mwaka huu, pamoja na kuhakikisha usalama wa chakula, wakulima pia watapata faida zaidi kutoka kwa shughuli za kilimo, na kupewa haki za kutosha zaidi za kumiliki mali, ili kuimarisha mageuzi ya mfumo wa ardhi vijijini.
 
Sisi tuna Maziwa makubwa manne, Mito zaidi ya Sita yenye urefu na upana sana ila hatujui kama ni mali kabisa na hatuitumii kama msaada kwenye kilimo

Hebu tuamke siku moja tuwe wakulima wakubwa Africa nzima kwa ardhi tuliyonayo

Wachina wanatafuta ardhi mpaka Africa ili walime wakawalishe watu wao na ipo siku mkicheza mtakuwa wakulima wa mchina badala ya sisi kuwauzia
 
Nini kifanyike boss
 
Nini kifanyike boss
Tuachane na jembe la mkono
Vijana wachukue mashamba kama serikali ilivyokubali
Ila mashamba yawe makubwa sana na ya umwagiliaji
Tutumie maji tuliyonayo kwa ajili ya umwagiliaji

Mito ichungwe na itumike kwa nidhamu sana na hata atakaekiuka afungwe na faini kubwa sana kuanzia million 10 kama ni kampuni

Mito yetu itumike kama vyanzo vya usafiri pia kwa kusafirisha mazao na matunda pia

Kama tutachunga mito yetu mbona ina faida kubwa sana

[emoji631] kwa siku bidhaa zinazopita kwenye mito yao ni $2b hiyo ni siku moja tu bidhaa za $2b sio mchezo

Sasa sisi mito yetu ina kazi gani kama hatujui hata kuitumia
Kama Mungu katupa akili kuzidi wanyama mbona tunajiweka kwenye kundi la kondoo sasa
 
Wenzetu wanatumia mali asili zao vizur ..cc tunajidai kuilinda cjui Nan aje kuitumia ....ety itaisha xaxa iko ili iweje Kama hatuezi tumia kwenye kilimo
 
Sisi tulianza na kilimo kwanza kipindi cha mkwere baada ya miaka 10 tukaamia kwenye viwonder vya nagu baada ya miaka6 hatujui samia anashika nini!!

Yani taifa halina dira, lipo lipo tu!!
 
Hawa jamaa wenye macho madogo kiukweli wapo vizuri.
 
Tuachane na jembe la mkono
Vijana wachukue mashamba kama serikali ilivyokubali
Ila mashamba yawe makubwa sana na ya umwagiliaji
Tutumie maji tuliyonayo kwa ajili ya umwagiliaji

Mito ichungwe na itumike kwa nidhamu sana na hata atakaekiuka afungwe na faini kubwa sana kuanzia million 10 kama ni kampuni

Mito yetu itumike kama vyanzo vya usafiri pia kwa kusafirisha mazao na matunda pia

Kama tutachunga mito yetu mbona ina faida kubwa sana

[emoji631] kwa siku bidhaa zinazopita kwenye mito yao ni $2b hiyo ni siku moja tu bidhaa za $2b sio mchezo

Sasa sisi mito yetu ina kazi gani kama hatujui hata kuitumia
Kama Mungu katupa akili kuzidi wanyama mbona tunajiweka kwenye kundi la kondoo sasa
Mkuu neno "akili" unalifahamu ?
 
Wenzetu wanatumia mali asili zao vizur ..cc tunajidai kuilinda cjui Nan aje kuitumia ....ety itaisha xaxa iko ili iweje Kama hatuezi tumia kwenye kilimo
Ndio ujinga wetu
Nyerere alisema eti mpaka watu wangu waelinike ila hakujua maisha yanapanda na watu wanaongezeka

Alipata fursa akashindwa kuitumia
Hivi madini yangechimbwa miaka ya sitini na 70 Leo tungekuwa wapi

Sidhani kama wizi ungekuwepo kwenye taasisi za umma na hata rushwa ingekuwa chini sana

Kwa sababu tungekuwa na utajiri mkubwa na kutanuka kimawazo zaidi

Angalia Waarabu mafuta yalipogundulika tu wakawaambia [emoji631] wachimbe na baadae wazungu wengine wakafuata
Ila kwao ni jangwa na utajiri ni mafuta tu ila hela zao walitaka miji yao iwe kama ya Ulaya

Na sisi eti leo ndio tunafurahia Flyover kama ni kitu kipya wakati overpass ya kwanza ilijengwa mwaka 1843 imagine

Sisi ni wa kuchapwa viboko badala ya kuwaonea watoto darasani
 
Kuna tofauti kubwa sana kati yetu sisi watu weusi na watu weupe, tenga muda wako mara kwa mara waza kuhusu hiki nilicho andika.
Niko nao miaka 33 sasa na ninaishi tofauti
Najua maisha yao kwa sababu niko nao

Miaka 28 iliyopita nilirudi bongo nikiwa nimetoka London
Nilikaa kama miezi 6 baada ya kupigiwa simu na jamaa mzungu kuja kumshikia biashara yake ili awapeleke watoto wake holiday Disney

Kweli nilimuahidi nikarudi London na kumshikia biashara kwa wiki 3 aliporudi alikuta kila kitu kiko sawa na mauzo yameongezeka

Hiyo ndio tofauti yetu na wao
Je unaweza kumuachia mtu biashara zako bongo? Ukaenda holiday na ukakuta faida ?

Sijisifu ila nimejifunza na kukulia kwenye biashara na uaminifu pia
 
Tusingekuwa popote. Mkuu neno "akili" unalifahamu ?
Nakumbuka miaka ya 70 kuna watu wafanya biashara akiwemo baba yangu walikuwa wanamiliki magari
Father alikuwa ni general merchant alinunua Land Rover mpya Enzi hizo

Mzee mmoja jirani alikuwa ni wholesalers wa pombe alikuwa na Peugeot
Na mwingine mkulima alikuwa na Peugeot pia

Sasa mkuu huoni kuwa watu Enzi hizo wakikuwa wanajituma na kufurahia maisha kama waliyonayo wenzetu?

Mkulima ana Peugeot
Ilitakiwa kwa sasa mkulima awe na V8
Sio yeboyebo
Siasa chafu ndio zimedumaza watu
Watu wamekuwa hohehahe

Tungekuwa popote"
 
all this chinese development just to wake up early in the mornng and put a mask on a daily basis..

where is the quality of life?
 
Niko nao miaka 33 sasa na ninaishi tofauti
Najua maisha yao kwa sababu niko nao

Miaka 28 iliyopita nilirudi bongo nikiwa nimetoka London
Nilikaa kama miezi 6 baada ya kupigiwa simu na jamaa mzungu kuja kumshikia biashara yake ili awapeleke watoto wake holiday Disney

Kweli nilimuahidi nikarudi London na kumshikia biashara kwa wiki 3 aliporudi alikuta kila kitu kiko sawa na mauzo yameongezeka

Hiyo ndio tofauti yetu na wao
Je unaweza kumuachia mtu biashara zako bongo? Ukaenda holiday na ukakuta faida ?

Sijisifu ila nimejifunza na kukulia kwenye biashara na uaminifu pia
Huo ni mojawapo ya utofauti uliopo kati yetu sisi na wao.
 
Back
Top Bottom