Re: Kuvuliwa uongozi kwa Zitto; CHADEMA Mmejipangaje kuepuka propaganda za UDINI na Ukanda zidi yenu
Katika hili, "Tuwe werevu kama nyoka lakini wapole kama hua." Tutashinda!
Reply Reply With Quote Send PM
Haki sawa
Today 02:47
#147
JF Senior Expert Member
Array
Join Date : 4th October 2007
Posts : 668
Rep Power : 9404
Likes Received
544
Likes Given
6
Tafsiri ya Udini na Ukanda wa CHADEMA kwa hatua za Kamati Kuu.
Kikao cha Kamati Kuu ya Chadema kilichomalizika juzi na maazimio yake kutangazwa jana kiliamua kuwavua Uongozi wajumbe wa Kamati kuu wawili ambao ni aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu , Mhe .Zitto Kabwe na Dr. Kitila Mkumbo.
Aidha kilimvua madaraka ya uongozi aliyekuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Arusha Samsoni Mwigamba .
Ukiangalia kwa umakini uamuzi huo wa Kamati Kuu utaona kuwa kwa upande wa dini , Ukabila , Mikoa na Ukanda utaona ifuatavyo;
Zitto Kabwe , huyu ni Muislamu, Kanda yake ni Magharibi , Kutoka Mkoa wa Kigoma , Kabila lake ni Muha.....
Dr.Kitila Mkumbo, huyu ni Mkristo, Kanda yake ni ya Kati, Kutoka Mkoa wa Singida, Kabila lake ni Mnyiramba .....
Samsoni Mwigamba, huyu ni Mkristo, kanda yake ni Kaskazini, Mkoa wa Arusha ( ndio alikuwa Mwenyekiti wa Mkoa) , Kabila lake kwa kweli sijui, ila Nina uhakika kuwa huyu sio Muha wala sio Mnyiramba.
Ukafanya uchambuzi ambao sio biased , kwa vyovyote vile utaona kuwa kwa upande wa dini, Muislamu yuko mmoja na Wakristo ni Wawili.Hii ni sawa na kusema kuwa 75% ni Wakristo ndio wamepunguzwa Chadema na 25% ya Waislamu ndio wa epunguzwa kwa maamuzi hayo, huwezi kusema kuwa kulikuwa na ajenda ya kuiumiza dini moja , ila dini iliyoathirika zaidi ni Wakristo kwa kuwa ni asilimia 75% ndio wameathiriwa na maamuzi hayo.
Ukija kwa upande wa Ukanda unakuta kuwa Kanda ya Magharibi imeathirika kwa 33.33% , Kanda ya Kati imeathirika kwa 33.33% na Kanda ya Kasikazini imeathirika kwa 33.33% , hivyo maamuzi hayo haya kufanyiwa kwa misingi ya Ukanda Kwani kila Kanda imeathirika kwa kiwango sawa sawa, huwezi kutoa conclusion kuwa kulikuwa na ajenda ya Ukanda katika maamuzi yaliyofikiwa.
Ukitazama maamuzi hayo kwa Dhana ya Mikoa , utakuta kuwa hakuna Mkoa ambao uliathiriwa kuliko Mkoa mwingine Kwani kila Mkoa umeumia kwa kiwango sawa yaani Singida 33.33%, Arusha 33.33% na Kigoma 33.33% , hivyo unaweza kufikia conclusion kuwa hapakuwa na Mkoa ulipokuwa umelengwa Mahususi , ndio maana maamuzi hayo haya wezi kuitwa yalikuwa ya kuumiza ama kupendelea Mkoa fulani.
Ukiamua kuyatazama maamuzi hayo kwa misingi ya Ukabila unakuta kuwa hapakuwa na Kabila ambalo lililengwa Mahususi, kwani hapakuwa na Kabila moja lililoumia kuliko Kabila lingine , yaani kwa kupoteza idadi kubwa ya wajumbe kwenye vikao vya Chadema .
Hivyo, basi nawataka wale wote ambao wana jengo hoja kuwa uamuzi huu ulikuwa ni kwa misingi ya Ukanda, Udini na au ukabila wathibitishe madai yao kwa facts na sio kwa hoja nyepesi na Propaganda za kizamani kama ambavyo wanafanya kwenye kujenga hoja zao ili Jukwaa hili liweze kuwa na heshima yake ya miaka hiyo .
Aidha, kwa wale ambao tunaamino kuwa maamuzi hayo yalifanywa kwa misingi ya haki na kwa lengo la uwajibikaji,tunaamino kuwa hatua ya Kamati Kuu ilikuwa sahihi nailizingatia merits na sio kwa kutazama jambo lingine lolote lile.
Mwenye hoja unakaribishwa kwa mjadala wa Nguvu ya Hoja na sio Hoja za nguvu , kama unafikiri kuwa IQ yako iko chini please soma subiri wengine wachangie kwa kujenga hoja , Moods zingatieni hoja kwa maslahi ya jukwaa hili.
Thanks, CC, Nguruvi3, Mchambuzi, Mkandara, Mwanakijiji, Mungi, et all.
Alinda and TsafuRD like this.