Waraka uliowaondoa Zitto Kabwe na Kitila Mkumbo CHADEMA huu hapa

Waraka uliowaondoa Zitto Kabwe na Kitila Mkumbo CHADEMA huu hapa

Kwa walio zaliwa mwaka 90 wenyewe kwa akili ya kawaida wanaona huu ni mchezo mchafu,chukulia mfano mtu wako wa karibu akusaliti utafanyaje,?huu mchezo wa wanasiasa wanatuona wananchi ka watoto vile.mara flani mara flan leo zitto,na hii yote si kwa ajil ya uongozi bora na kwaajil ya bora kiongoz,tunarudi kulekule kila siku itakuwa bora ya jana
 
Mkuu hayo mengine siwezi sana kutolea majibu kwani waraka wenyewe ukiuanzia juu hado chini utaona vijana na wazee walitaka kutengeneza movie ya 007 kwa fikra za bongo movies.

Well, labda tuu nikuambie kwa jinsi ulivyojitambulisha kuwa Kitila mkumbo ndie aliyekuvutia ,na hivyo sasa unapata blow sana.Huo ndio ukweli ila umekosea kitu kimoja..hapa ulipaswa umia sana kwa Mtu uliyemtazama anapofanya kitu irresponsibly hivyo.NIlitegemea kwa umri wako ungekuwa umeona jinsi Zitto alivyo irresponsible na mwenye jazba na papara km Waraka unavyosema.Tena kw akiasi ambacho waandaji wameona kuwa ndio tishio lake kuu.Hayo ndiyo tumekuwa tukiyasema sana humu.Na ujumla wake ni kukosa BUSARA km waraka ungeandikwa na mwingine neno Busara lingetumika ktk hii CV ya Zitto au mkakati.

Mkandara kuna watu wengi tuu huvinjwa mionyo yao na Viongozi wa dini waliowamini na kuja kuta wakiwabaka(si madrassa, sunday schools, shule za kidini etc), wapo watu walihisi salama mikoni mwa wazee wao na kujibuka wakiwabaka na kuwaua, wapo walioamini waume na wake zao ni rijali kumbe ni mashoga, wapo walioamini walimu wao wa uchumi ni wachumi kweli,kumbe personala finance ni issue hadi wanajiua.Ndio maana tunakatazwa kumtegemea mwanadamu hata ktk mema.

Dr.Kitila isku zote sijawahi weza pata namna ya kumwondoa ktk uchafuwa UDSM Political Science nanimekuwa nikisema haya sana .Wapenda propaganda na wneye uwezo mdogo wamekuwa wakidhani nashambulia kwa ukanda, sijui ukabila.Nae kwa akili yake akabweteka akidhani Ni msomi wa daraja lake, bila kuw ana clue kuwa shida ni shule aliyosoma na waliomfundisha,ndio wamemwaribu sana pamoja na kwamba propaganda za mlima zinafanya watu waone kuwa ni chuo bora sana.
Ahahaha hili la sinema nalikubali. Lakini, mkuu wangu sinema siku zote hubakia sinema ya James Bond ambaye ni msanii tu ukianza kufikiria kwamba kuna James Bond wa ukweli badala ya riwaya ya kiini macho basi hutapata usingizi. Na ndicho kilichofanyika maana huu waraka umewanyima watu usingizi na sio chama wala wanachama.Isipokuwa sasa mnatulazimisha watu wote tulale na mashoka kwa WOGA.

Pili swala la BUSARA nimekuwa nikisema sana hapa JF kuhusu Vijana na kipawa hiki ya kwamba hakiji kwa barehe bali kula chunvi na kuona mengi. Katika maisha kila mtu hupitia mitihani mingi na maamuzi yake hutokana na kujifunza pale waswahili wasemapo dunia itamfunza na ndipo Hekima na Busara hukupanuka. Katika hili ndio maana watu hushangaa mtu mzima anapo act kama mtoto mdogo kwa maana ya kwamba umri wake haukupanua kiwango cha busara zake!

Swala la Kitila nadhani unalikosea sana kwa sababu sina mahusiano na Kitila, isipokuwa ndiye alonipa darasa kuhus Chadema na kuvutiwa. Kuna wengi humu JF walijaribu kutushawishi lakini hawakuwa na mvuto ktk ushawishi wao. Pengine hata Mbowe au Zitto wangenambia nisingejiunga ila Kitila aliweza kupandikiza mbegu kichwani mwangu na kuniaminisha kwamba Chadema ndicho chama kinachosimamia sera na ilani nazopigia kelele siku zote. Na kama unakumbuka vizuri, mimi nilikuwa napiga vita vikali sana UFISADI na nikasema Tanzania pasipo kuondoa Ufisadi haita jalisha ni kiwango gani cha makuzi ya GDP, bado wananchi wataendelea kuwa maskini na kuna hatari ya kuunda madaraja (class) ya wananchi. Na kwa bahati tukamchagua Dr.Slaa ambaye kazi yake kubwa ilikuwa kupiga vita UFISADI na hakika Chadema ilipata mvuto mkubwa zaidi kutokana na hili pekee.

Zitto pamoja na mabovu yake tumemsema sana humu JF na sisi wengine tumejiunga CDM bila kujua kuna makundi maana huu waraka unaonyesha hawakuanza jana wala juzi isipokuwa kundi hili lilikuwepo toka mmwaka 1998 na historia inatuonyesha wazi kwamba muda wote wameshindwa kumweka mtu wao kiti kikubwa. Ina maana mbinu hizi hazina madhara kwa chama maana kama ingekuwa hivyo basi ingetokea ktk chaguzi zilizopita.

Nitaendelea kusema tu ya kwamba HEKIMA na BUSARA hutumika wakati nkama huu na hakika sidhani kaa viongozi wetu wametumia HEKIMA na BUSARA katika swala hili. Kama ingekuwa Zitto na Kitila wanataka kuunda chama kingine tokana na CDM na kuwavuta wanachama wa CDM ama kuwaondoa CDM hapo ndipo tungesema huu ni USALITI lakini mbinu zzote za kumuondoa kiongozi ama viongozi ambao wanakwaza ama kukawiza mafanikio ya chama, sidhani kama yanahitaji hukumu kama hii kwa sababu inaondoa kabisa Ushindani ndani ya chama. Nani sasa hivi atadiriki kufanya maandalizi ya kikampeni ili kuchukua uongozi uchaguzi ujao maana lazima mtu ajipange na watu wanaomkubali na maamuzi haya yamekuwa fundisho kwa wale wote wanaofikiria wanaweza kujiandaa kugombea vyeo Chadema.

Huyo Lowassa huko CCM mbona inajulikana vizuri tu kuwa anajipanga kwa ajili ya 2015 na amejaza wajumbe wanaomkubali ktk mabaraza yote muhimu ya chama kwa ajili ya 2015! Nina hakika Membe pia ajipanga, January na wengineo na wala haikuanza jana. Watu hujiandaa kwa miaka, na hakuna kosa kutokubaliana na uongozi uliopo. Kinachotakiwa ni Mbowe na Dr.Slaa kutuonyesha sisi wananchama kuwa wana uwezo mkubwa zaidi ya makundi haya na watapendekezwa kuendelea na madaraka.

Mkuu wangu, wakati mwingine tuikubali Demokrasia pamoja na madudu yake, ndivyo inavyochezwa na hatuwezi kuendelea na mfumo ule ule wa Kikomunisti ambao Upinzani ndani ya chama ni USALITI. Hapa ndicho kilichotumika japo huyo Mwiguru katumia neno - Akili ndogo kutawala akili kubwa. Ukweli ni kwamba akili za kijamaa kikomunist zimetumika badala ya kutambua kwamba huu ni wakati wa Demokrasia ambapo mwenye mvuto zadi ndiye huwa mshindi hakuna kulazimishana. Kundi hili lisingeweza kuwavutia wajumbe wote baada ya kuoneshwa waraka huu na nina hakika wangepigwa chini japo ilikuwa ni siri yao.

Maasalaam nilikuwepo.
 
Hofu yangu nikwamba CHADEMA imepoteza muelekeo kwani hata NCCR ilikuwa hivyo nao naona wameanza migogoro wakumbuke kuwa kujipanga upya mpaka kufika mahali walipo nikazi ya ziada.Halafu nashindwa kuelewa kwanini wanashindwa kuiondoa dhana mbaya ya udini kama ndiyo kashifa kubwa ya chama hicho hatjuwi ina ukweli au inabaki kuwa siri yao ilah!
 
Kweli Wajinga ndio waliwao,naona Ben Saanane hajasahau kujifagilia hapo kwenye hiyo riwaya yao walioitengeneza.

Hapa ni either Mbowe na Dr Slaa ni wajinga sana mpaka wanadanganyika kirahisi hivi au wanamuogopa sana Zitto mpaka kupelekea wao wenyewe ku-engineer huu mchezo wa kitoto wa kujitekenya kisha kucheka wenyewe.

Zitto,tunakuamini!!propaganda za kitoto kama hizi haziwezi kufanikiwa na hazitafanikiwa.Chukua muda huu kutafakari kwa makini na fahamu kuwa tunausubiri mwongozo wako na tutakuunga mkono.

Watu wapumbaav kama nyie mndhani kuvuliwa kwake uongozi huyo yuda kumefanywa na mbowe wakati hayo ni mbmuzi ya kamati kuu ya cdm
 
Jinsi upepo wa kisiasa unavyovuma, siku za Zitto kubaki CDM zinahesabika! Muda si mrefu atanyang'anywa kadi. Je, options zilizopo ni zipi?
1. Atahamia CCM (nyumbani), au,
2. Atahamia CHAUMA (Chama alichokianzisha yeye), au,
3. Atafungua shauri Mahakamani kupinga kuvuliwa uanachama, au,
4. Atahamia Chama kingine kama NCCR (yupo pandikizi mwenzake Mbatia), TLP (nafikiri wataiva vzr na kada mwenzake wa CCM, Dr Lyatonga), au,
5. Ataachana na Siasa. Kumbukeni hili amewahi kulisema huko nyuma kuwa ataachana na siasa na kuendelea na Academics.
Vyovyote itakavyokuwa, Zitto ni mtu hatari sana: "Once a traitor, always a traitor!"
Amesambaza mbegu ya udini/ukanda na ukabila kwa kushirikiana na CCM, labda akiamini kuwa atakuwa nao all along, bila kujali madhara yake katika taifa letu. Watamtumia kama mpira wa kiume kisha haja ikishaisha atatupwa shimoni!
 
Wanajamvi, makala hiyo hapo chini niliisema mwaks 2011, nikimuonya ndugu yangu na kijana mwenzangu Zitto Kabwe juu ya aina ya Siasa zake, nivema tuyarejee yale tuliyoyasema miaka miwili huko nyuma kuhusu siasa za Zitto na wengine,

Hii inatupa fursa ya tafakuri ya nera na machipuko mapya katika kuiendea Tanzania mpya na siasa safi,




Kazi ya kuihujumu Chadema aliyotumwa Zitto Kabwe inapokuwa nzito kwake.


27Sep 2011


Binafsi naitafakari kauli ya Zitto Zuberi Kabwe na ninafurahi kuona kuwa kile nilichoonya kuwa kijana mwenzangu anatumiwa vibaya na ccm sasa kimetimia.

Wakati akihojiwa katika kipindi kiitwacho, Exclusive interview na Millard Ayo cha Clouds FM
Amesema hivi nanukuu “Wazee wetu walitusaidia kutupatia maendeleo ya kisiasa, sasa ni jukumu letu kuleta maendeleo ya kiuchumi. Ila naomba nisisitize, jukumu hili haliwezi kutekelezwa na mtu yeyote aliyezaliwa kabla ya uhuru, na ninatangaza kuwa nitagombea urais mwaka 2015″

Naunga mkono kwamba vijana tujitokeze kuleta maendeleo kwa taifa letu, lakini napingana vikali kauli “jukumu hili haliwezi kutekelezwa na mtu yeyote aliyezaliwa kabla ya uhuru”


Kwanza mimi nasema amewatukana wazee wote Tanzania, huku ni kukosa busara heshima na hana sifa ya Uongozi kwani ni mbaguzi. Wapo Wazee waliozaliwa kabla ya uhuru na wanailetea Tanzania maendeleo na wapo wapuuzi waliozaliwa baada ya uhuru ni wapuuzi wa kutisha yeye akiwemo. Zitto hana busara kwa hili

Amejisemea bila kufikiri. Ana maanisha hata kama mtu ni msomi kama akina Dr Slaa, Dr Gharibu Bilali mtaalamu wa nyuklia na Prof Lipumba hawawezi kusaidia isipokuwa wale waliozaliwa baada ya uhuru? Huu ni uhuni wa kawaida wa Zitto ambaye hujitahidi kujionyesha kama thinker wakati siyo hasa ikizingatiwa hata akiwa shule alipita hivyo hivyo.

Nadhani kwa thinker mzuri hana haja ya kuwatenga watu kwa umri wao bali tabia zao hasa linapokuja suala zima la ujenzi wa taifa. Mbona tuna vijana waliozaliwa baada ya uhuru kama yeye mwenyewe Zitto na wengine lakini bado ni mafisadi???

Kitendo cha kutangaza nia ya kugombea urais 2015 sio kibaya kwakuwa ni haki yake kikatiba, lakini kutangaza nje ya ya utaratibu wa chama chake huu ni uhaini kwa chama. Zitto anajua anachokifanya, na anajua matokeo yake lakini ni jambo la kusikitisha kuwa hajui madhara yake kwake.

Katika tafakuri yangu kwa mapana ya nera, nikamkumbuka mwalimu wangu pale Moscow Urusi, Prof Radav Metbarg aliyenifundisha uhandis wa umeme, huyu alinidokeza aina ya binadamu, hakika ilikuwa muhimu sana ndio maana leo imenijia akilini nikalazimika kuzama kimang’amuzi zaidi, nimefanya hivyo ili nimtambue huyu mtu aitwae Zitto Kabwe kiundani zaidi, Katika aina za binadamu Zitto ni wa aina ya Sanguine, hii ni kwamujibu wa tabia zake za kisiasa. Hakika naamini watu wa aina hii ni hatari hasa ukiwasogeza jirani na uongozi popote pale basi wanaouwezo na msukumo mkubwa wa kukupindua. Hiyo ni sehemu ya sifa ya watu wa aina hiyo na kwa ujumla ni waroho wa madaraka.

Lakini najiuliza kwani Magharibi mwa Tanzani ndiko aina hii ya watu inapatikana kweli au yeye ni chipuzi tu? Nikiangalia wenye tabia zake nawaona kama Kafulia, Mkosamali na Shibuda. Lakini sitaki kujikita katika dhana hiyo ya ukanda bali nasimamia kuwa hao ni chipuzi la aina hiyo ya tabia za binadamu ambao ni hatari hasa uwasogezapo katika vyeo vya juu basi huutaka ufalme hata kwa njia ya uasi tu. Muono wangu ni kuwa Zitto hautaki urais na anajua fika kuwa kwa mujibu wa katiba iliyopo yeye hastahili kugombea URAIS, ila kwa gharama kubwa amejichimbia msituni kukihujumu chama chake kilichomlea na kumfanya leo ajione fahali la masika.

Ninarudia tena Zitto hana nia ya urais, nasema hana hata chembe za kuutaka urais ila analengo moja tu nalo nikukivuruga Chama chake tu. Mwili wa Zitto upo Chadema ila moyo wake upo ccm palipo panono, kweli pesa mwanaharamu.

Lakini wadadisi wa siasa za Afrika tunapaswa kulaumiwa sana, tulipopokea mageuzi ya siasa za kidemokrasia na kuziacha siasa zetu za kiimla lakini tulishindwa kupokea hata miundo ya siasa hizo, mathalani vyama vya siasa vyenye ukwasi wa kidemokrasia huwa na utaratibu wa kutengeneza viongozi wa chama, kitaifa na viongozi wa kimataifa. Hili nadhani hata Hayati Mzee Nyerere alifanikiwa kuliasisi lakini baada ya kufariki mabaka demokrasia wamebaka na kubuni mifumo ya kuzalisha watawala sio kuzalisha viongozi tena.

Hili lisiwe turufu kwa Zitto, naamini anatambua njia aipitayo na madhaifu ya muundo huu wa vyama vyetu vya siasa. Ningefurahi na ninaamini wadadisi wote wa siasa za Afrika wangefurahi pia kama Zitto angeanzisha harakati za kuboresha muundo wa vyama vyetu vya siasa hususani Chama chake cha Chadema kilichobeba tumaini kuu la wazalendo na wengi wa nchi hii. Je ccm ya leo bado inautaratibu wa kuandaa vijana kwaajili ya siasa za kesho? kwaajili ya urais? kwaajili ya wanadiplomasia wa kimataifa wakesho? Chadema je? UDP je? NCCR je?

Jambo la kumshukuru Mungu nikuwa Chadema wanajua kila anachokifikiria kufanya, anachokifanya, anakolalia, anakoamkia, anakokutania na wafadhiri wa uasi huu na kila kitu. Kwaujumla chama kinamjua utosi hadi unyayo.

Chadema wamekuwa wakipigana vita mbili kwa mda mrefu, vita hiyo ni ya nje (ccm) na ndani (Zitto, Shibuda na mamluki wengine) lakini mda wote chadema imeshinda na itashinda na itaendelea kushinda daima kwakuwa ni vita kati ya wema na ubaya kumbuka na elewa kuwa kwenye wema Mungu yupo.

Ninachoamini katika siasa duniani ni kuwa hakuna aliyejuu ya chama chake.
 
Muizike Mara ngapi....hamna uwezo wa kufikiri...mmebakia Na ushabiki uso tija.....Nadhani atakayefuata baada ya zitto ni lissu....hatoki kwa wenye chama....

kwanini CCM roho inawauma zzk kupokwa madaraka? Nitafurahi akijtoa kabisa chamani, hakupendezwa na ujio wa wabunge vijana bungeni, alitaka awe kijana peke yake bungeni..aende akaue panya huko kigoma!
 
Zitto na wenzake watavuna walichokipanda.. Kama analalamika chama kuyumba wakati yeye ni Naibu katibu Mkuu, je mchango wake yeye umeonekana wapi katika kukijenga chama?
Na kwa nini aandae vikao vya siri kama hivi badala ya kutumia vikao halali vya chama kama anaona kuna issues hazitulia?
Hawa ni masalia tu watapotezwa kama akina Juliana Shonza, na Mwampamba... Shame on Zitto and his friends.

Umenena kaka naibu katibu mkuu ni nafasi kubwa sana ndani ya chama.Kama kiongozi unaona kuna tatizo la kiutendaji,ulisaidia vipi kurekebisha hali hiyo manake na ww ni sehemu ya maamuzi.Au ulisubiri ulalame baadaye ili uchaguliwe wewe????!Hizi ni hila tu wala hakuna kutetea.Lazima usome kwa makini dhamira ya Zitto na wenzake.Zitto alikuwa anafanya mambo ya makusudi either kukomoa viongozi wenzake ili baadaye apate fursa ya KULALAMA kwamba mambo hayaendi vizuri kwa sababu ya fulani.Hizi ni HILA na UNYOKA wa mtu mbaya.Chadema ni taasisi inayofanya kazi pamoja,sasa inakuwaje kiongozi alaumu wenzake bila ya yeye kutuambia amefanya nini???!Upuuzi huu wa kushabikia ujinga wa Zitto haufai hata kidogo.Hawezi kuendesha taasisi yeyote ile kama anavyotaka Zitto(hasa ukiwa kiongozi)!!!!Kwenye uongozi kuna kitu kinaitwa COLLECTIVE RESPONSIBILITY,kama jambo baya limetokea basi kila part inawajibika sehemu yake.
 
analazimisha umaarufu..naomba ajitoe uanachama..mtu gani hawapendi wabunge wa upande wake ? Kwanini ccm wanampenda sana huyu KIRUSI?
Kama yeye ni maarufu aanzishe chama chake cha siasa,yeye awe mwenyekiti,kafurila awe katibu mkuu,naibu katibu mkuu awe kitila mkumbo na mama yake awe mwenyekiti wa baraza la wanawake!
 
Back
Top Bottom