Waraka uliowaondoa Zitto Kabwe na Kitila Mkumbo CHADEMA huu hapa

Waraka uliowaondoa Zitto Kabwe na Kitila Mkumbo CHADEMA huu hapa

Purukushani iliyomwondoa Zito ndani ya Chadema imegundulika kuwa ni mkakati wake wa kutaka kuwa Mwenyekiti wa Chama na kusimamishwa kugombea Urais kwa tiketi ya CDM,mpango uliokuwa ukifadhiliwa na kupangiwa mkakati wa hali ya juu na CCM.
Sasa ni wazi kuwa mission hiyo ime fail ila kwa vile inaonyesha anakubalika sana ndani ya CCM (Hata naibu katibu mkuu wa CCM Mwigulu Nchemba amelionyesha hilo katika thread yake humu JF) nafasi ya kugombea Urais anaweza kuipata huko anakopendwa sana kama inavyoelezwa.
Sasa jee hali itakuwaje kwa zile kambi zinazofahamika dhahiri kuwa zimekuwa katika mkakati wa kuhakikisha mtu wao anapata nafasi ya uteuzi kupeperusha bendera ya chama? Tukumbuke Lowasa,Membe,Sita nk wanafahamika kuwa wametumia nguvu kubwa na rasilimali nyingi,jee watakubali kumwachia "wakuja" kirahisi tuu eti kwa vile anaungwa mkono na akina Mwigulu?
Au watamwogopa kwa vile Zito anatembea na orodha ya mabilioni ya Uswiss "mfukoni".
Nimeleta swali hili la kizushi baada ya kukumbuka hadithi ya Mwarabu na ngamia aliyeomba kuhifadhi kichwa tuu ndani ya banda wakiwa jangwani. Jee huo muziki utakuwaje?
 
Thubutu! CCM walikuwa wanamtumia Zitto kama kondomu tu!! Sasa kondomu imekwisha matumizi yake! Imechafuka kiasi chake! Hawana haja nayo tena! Sasa mahali pake ni jalalani! Hiyo ndiyo siasa! Kwa maelezo zaidi muulize Mwigulu Nchemba.
 
Chakaza unaakili fupi kama mwili wako kweli, yaani nayo nihoja hiyo?

Mkuu kwanza mie sio mfupi, pili nimekuambia swali la kizushi na tatu nipe jibu hali itakuaje? Maana Zito ana otea madaraka tuu jee ataweza sekeseke hilo ndani ya CCM yenye wenyewe?
 
kwa waraka huu, Mungu saidia wafuasi wote wa zito wajiuzulu, ili kukiacha chama salama, kwa kujiuzulu kwao ni faida kubwa kwa CHADEMA
 
Hehehe Its Too late to catch the train..
"Chadema itakufa kabla ya 2015"-Wassira,Nimeanza kuielewa kauli ya huyu mzee..Kwa hakika Chadema wamefanya moja ya kosa kuu la kiufundi,na litawagharimu mchezoni 2015..Ngoja tuendelee kuona picha la kihindi!!..
 
Hehehe Its Too late to catch the train..
"Chadema itakufa kabla ya 2015"-Wassira,Nimeanza kuielewa kauli ya huyu mzee..Kwa hakika Chadema wamefan

Tatizo ccm waliwekeza sana kwa zitto kama silaha yao muhimu ktk kusambartisha chadema.wakasahau kuwa walitakiwa kuwa na plan B iwapo zitto angetoswa na chama chake , kwa sasa ni dhahiri njia ni nyeupe kwa cdm kuelekea magogoni.CCM walikuwa short tem strategy huku wenzao cdm wakiangalia mbali zaidi.Kutoka kwa zitto kutayumbisha chama lakini kwa muda mfupi then kita-stabilize, na kusanga mbele kikiwa salama bila impurities.kwa ccm ni kilio zaidi ya mhusika zzk
 
Aisee kweli cdm hakuna demokrasia,leo zitto na wengne,kesho lissu, chama cha wachaga hicho,tena wa familia moja. baba mkwe,mke na mbowe . duuh 2tafika kweli.
 
Thubutu! CCM walikuwa wanamtumia Zitto kama kondomu tu!! Sasa kondomu imekwisha matumizi yake! Imechafuka kiasi chake! Hawana haja nayo tena! Sasa mahali pake ni jalalani! Hiyo ndiyo siasa! Kwa maelezo zaidi muulize Mwigulu Nchemba.

Duh nouma kweli kweli
 
Thubutu! CCM walikuwa wanamtumia Zitto kama kondomu tu!! Sasa kondomu imekwisha matumizi yake! Imechafuka kiasi chake! Hawana haja nayo tena! Sasa mahali pake ni jalalani! Hiyo ndiyo siasa! Kwa maelezo zaidi muulize Mwigulu Nchemba.

So Sad...
 
Wanabodi wenzabgu,
Ama kweli leo hii nimesikitishwa sana na maamuzi yalofanywa na uongozi wa juu wa chama kuhusiana na WARAKA huu. Ni maamuzi mabaya sana tena yanaweza tafsirika vibaya zaidi kwa sababu waraka mzima unawazubgumzia WATU fulani tu na sio jinsi ya kukiangusha CHAMA.....

Kwa mtazamo wangu...kuna mawili ama hukusoma waraka ule wote neno kwa neno ama umeusoma wote ila unafuta mbinu za kumnusuru rafiki yako Mkumbo. Nasema hivyo kwa sababu...

Mikakati ya kutumia udini, ukanda na ukabila ambayoimeainishwa kwenye waraka ule haiwezi kuwa halali ya kukiimarisha Chama...hiyo ni mikakati ya kukiangamiza chama ni mikakati hii inayotumiwa na wanapropaganda wa chama kikuu cha upinzani dhidi ya Chadema.
 
Wanabodi wenzabgu,
Ama kweli leo hii nimesikitishwa sana na maamuzi yalofanywa na uongozi wa juu wa chama kuhusiana na WARAKA huu. Ni maamuzi mabaya sana tena yanaweza tafsirika vibaya zaidi kwa sababu waraka mzima unawazubgumzia WATU fulani tu na sio jinsi ya kukiangusha CHAMA. Kila naposoma ni maagiz ya kukiimarisha chama zaidi tokana na mapungufu yaliyopo.. Na katika Siasa popote duniani uongozi unapolegalega wajumbe wana kila haki ya kufanya mazungumzo iwe kimtandao ama kwa pamoja kuhoji uongozi uliopo iwe wa chama au hata Yaifa.

Kama mnakumbuka wala sii muda mrefu huko CCM kwenyewe kulikuwa na mpango wa kumwondoa JK ktk Uenyekiti, tena kinyume cha utamaduni wa chama hicho japo katiba yao haitoi utaratibu na wanafi hiyo,. Na kama kusema vibaya mbona Lowassa kisha sema mengi asana ya udhaifu wa JK tena hadharani na kama mnakumbuka alisema kiongozi bora ni lazima uchukue maamuzi magumu. Wala sii pekee yake tumewasikia wangapi wakisema Uongozi wa JK ni dhaifu wakiungana na Mnyika huko vijiweni!

Binafsi yangu nimeshasikia viongozi kibao wa CCM na wengine mawaziri wakitofautiana kabisa na JK lakini kutokana na utendaji kazi wao wameendelea kuwepo ktk chama na serikali kwa sababu kinachohesabika ni uwezo wao wa kazi na madaraka walokabidhiwa kwa wananchi na sii urafiki ama nidhamu yao kwa viongozi wa juu. Ukitazama makatibu wote wa CCM waloenguliwa wote ilitokea kwanza baadhi ya viongozi kutoridhika na uendeshaji wao wa chama na yakafanyika mabadiliko japo sasa hivi ndio uozo kabisa. Lakini mabadiriko yalifanyika kwa kupitia makundi ya wajumbe na viongozi wengine wala haikuwa maamuzi ya JK pekee ama kupitia vikao vya chama eti washauriane kama hawafao ama laa! Na kwa busara kubwa hakuna mtu hata mmoja anayejua sababu za viongozi hao kuenguliwa ama kuonyeshwa waraka ulowataka waenguliwe!

Hebu turudi nyuma na kujiuliza, hivi kama haya yaloandikwa hayana ukweli wowote ule kwa nini yasipatiwe majibu kwanza kuodhoresha kila kipengele UONGO uko wapi na ukweli ni upi ili nasi tusiwe na wasiwasi na hatua zilizochuku;liwa. Na kisha jamani kwa nini kila siku mtu yeyote anayejaribu kuonyesha udhaifu wa viongozi kwa nia ya kuongeza nguvu zaidi ya chama hufukuzwa na kibaya zaidi hadithi tunazosikia ni zile zile za CHADEMA kina wenyewe!..

Viongozi wa CHADEMA nawataarifu tu ya kwamba CCM ina mbinu nyingi sana na yawezekana msaliti kwetu sii hawa vijana isipokuwa uongoozi uliopo kwa sababu haiwezekani vitu hivi vijirudie mara tatu!

1. Mwaka 1998 wakati NCCR ni tishio kubwa la CCM kwa uchaguzi wa mwaka 2000, yalitokea haya ya kina Mrema na chama kikapoteza watu maarufu kiasi kwamba CAF ikashika moto.

2. Mwaka 2008, kabla tena ya uchaguzi wa mwaka 2010 wakati CAF ikionekana tishio la CCM, Uongozi wa CAF wakajikanyaga nao wakafukuza watu kiasi kwamba uchaguzi ulipofika walikuwa hoi bin Taaban.

3. Leo tena mwaka 2013, matumaini yetu yakiwa Chadema inatokea tena chama hiki kufanya yale yale yalowaangusha wengineo. na siku zote walofukuzwa ndio walionekana wenye makosa japo ukichunguza kwa makini hawa watu walofukuzwa hawakuwahi kuwa wanachama wa CCM kabla!

Je, hii kweli ni bahati mbaya tu inatokea ama hivi vyama vyetu vya siasa ni sehemu ya CCM yenyewe na kuna watu walopandikizwa wanaotuchezea akili maana haiwezekani kabisa kwa mara ya tatu, tushindwe kila mara dakika za majeruhi..
Hapo kwenye nyekundu ndipo kwenye jawabu.
 
Mkandara well said. Nimesoma waraka wote sijaona kosa la Zitto. Waraka kuna sehemu inamjadili udhaifu wa Zitto. Ni waraka mzuri sana.

Kiuhakika umenena vyema sana kama hawataazima busara zako basi tena.
 
Last edited by a moderator:
Mkandara well said. Nimesoma waraka wote sijaona kosa la Zitto. Waraka kuna sehemu inamjadili udhaifu wa Zitto. Ni waraka mzuri sana.

Kiuhakika umenena vyema sana kama hawataazima busara zako basi tena.
 
Last edited by a moderator:
ushiriki wa Zitto kwenye tukio la KIbanda ilitosha sana kumtema ndani ya CDM...
 
kama kweli wamemfukuza zitto kwa haki basi wanasitaili kuogopwa na kuheshimiwa kwa kuchukua maamzi magumu. itasikitisha tu kama itakuja kubainika ni fitina. namkumbuka sana zito kwenye operation sangala.
 
Aisee kweli cdm hakuna demokrasia,leo zitto na wengne,kesho lissu, chama cha wachaga hicho,tena wa familia moja. baba mkwe,mke na mbowe . duuh 2tafika kweli.

Kuna baadhi ya taarifa sio lazima uchangie, hapa ni kwa wale wenye foundation course ya 'siasa za kimkakati' Binafsi naogopa hata ku-comment chochote! CDM nimewaogopa jamaa ni zaidi ya.. !
 
Panapokuwa na tatizo bora liwekwe wazi ili suluhu ipatikane kuliko kujenga lango jingine lisilo na manufaa
 
Back
Top Bottom