Wanabodi wenzabgu,
Ama kweli leo hii nimesikitishwa sana na maamuzi yalofanywa na uongozi wa juu wa chama kuhusiana na WARAKA huu. Ni maamuzi mabaya sana tena yanaweza tafsirika vibaya zaidi kwa sababu waraka mzima unawazubgumzia WATU fulani tu na sio jinsi ya kukiangusha CHAMA. Kila naposoma ni maagiz ya kukiimarisha chama zaidi tokana na mapungufu yaliyopo.. Na katika Siasa popote duniani uongozi unapolegalega wajumbe wana kila haki ya kufanya mazungumzo iwe kimtandao ama kwa pamoja kuhoji uongozi uliopo iwe wa chama au hata Yaifa.
Kama mnakumbuka wala sii muda mrefu huko CCM kwenyewe kulikuwa na mpango wa kumwondoa JK ktk Uenyekiti, tena kinyume cha utamaduni wa chama hicho japo katiba yao haitoi utaratibu na wanafi hiyo,. Na kama kusema vibaya mbona Lowassa kisha sema mengi asana ya udhaifu wa JK tena hadharani na kama mnakumbuka alisema kiongozi bora ni lazima uchukue maamuzi magumu. Wala sii pekee yake tumewasikia wangapi wakisema Uongozi wa JK ni dhaifu wakiungana na Mnyika huko vijiweni!
Binafsi yangu nimeshasikia viongozi kibao wa CCM na wengine mawaziri wakitofautiana kabisa na JK lakini kutokana na utendaji kazi wao wameendelea kuwepo ktk chama na serikali kwa sababu kinachohesabika ni uwezo wao wa kazi na madaraka walokabidhiwa kwa wananchi na sii urafiki ama nidhamu yao kwa viongozi wa juu. Ukitazama makatibu wote wa CCM waloenguliwa wote ilitokea kwanza baadhi ya viongozi kutoridhika na uendeshaji wao wa chama na yakafanyika mabadiliko japo sasa hivi ndio uozo kabisa. Lakini mabadiriko yalifanyika kwa kupitia makundi ya wajumbe na viongozi wengine wala haikuwa maamuzi ya JK pekee ama kupitia vikao vya chama eti washauriane kama hawafao ama laa! Na kwa busara kubwa hakuna mtu hata mmoja anayejua sababu za viongozi hao kuenguliwa ama kuonyeshwa waraka ulowataka waenguliwe!
Hebu turudi nyuma na kujiuliza, hivi kama haya yaloandikwa hayana ukweli wowote ule kwa nini yasipatiwe majibu kwanza kuodhoresha kila kipengele UONGO uko wapi na ukweli ni upi ili nasi tusiwe na wasiwasi na hatua zilizochuku;liwa. Na kisha jamani kwa nini kila siku mtu yeyote anayejaribu kuonyesha udhaifu wa viongozi kwa nia ya kuongeza nguvu zaidi ya chama hufukuzwa na kibaya zaidi hadithi tunazosikia ni zile zile za CHADEMA kina wenyewe!..
Viongozi wa CHADEMA nawataarifu tu ya kwamba CCM ina mbinu nyingi sana na yawezekana msaliti kwetu sii hawa vijana isipokuwa uongoozi uliopo kwa sababu haiwezekani vitu hivi vijirudie mara tatu!
1. Mwaka 1998 wakati NCCR ni tishio kubwa la CCM kwa uchaguzi wa mwaka 2000, yalitokea haya ya kina Mrema na chama kikapoteza watu maarufu kiasi kwamba CAF ikashika moto.
2. Mwaka 2008, kabla tena ya uchaguzi wa mwaka 2010 wakati CAF ikionekana tishio la CCM, Uongozi wa CAF wakajikanyaga nao wakafukuza watu kiasi kwamba uchaguzi ulipofika walikuwa hoi bin Taaban.
3. Leo tena mwaka 2013, matumaini yetu yakiwa Chadema inatokea tena chama hiki kufanya yale yale yalowaangusha wengineo. na siku zote walofukuzwa ndio walionekana wenye makosa japo ukichunguza kwa makini hawa watu walofukuzwa hawakuwahi kuwa wanachama wa CCM kabla!
Je, hii kweli ni bahati mbaya tu inatokea ama hivi vyama vyetu vya siasa ni sehemu ya CCM yenyewe na kuna watu walopandikizwa wanaotuchezea akili maana haiwezekani kabisa kwa mara ya tatu, tushindwe kila mara dakika za majeruhi..