andrewk
JF-Expert Member
- Apr 13, 2010
- 3,102
- 489
Kama unadhani anatumika, basi ujue hata huko nako watamtosa, maana amadhara ya kutumia huwezi kuaminika tena mbele ya jamii zote
Purukushani iliyomwondoa Zito ndani ya Chadema imegundulika kuwa ni mkakati wake wa kutaka kuwa Mwenyekiti wa Chama na kusimamishwa kugombea Urais kwa tiketi ya CDM,mpango uliokuwa ukifadhiliwa na kupangiwa mkakati wa hali ya juu na CCM.
Sasa ni wazi kuwa mission hiyo ime fail ila kwa vile inaonyesha anakubalika sana ndani ya CCM (Hata naibu katibu mkuu wa CCM Mwigulu Nchemba amelionyesha hilo katika thread yake humu JF) nafasi ya kugombea Urais anaweza kuipata huko anakopendwa sana kama inavyoelezwa.
Sasa jee hali itakuwaje kwa zile kambi zinazofahamika dhahiri kuwa zimekuwa katika mkakati wa kuhakikisha mtu wao anapata nafasi ya uteuzi kupeperusha bendera ya chama? Tukumbuke Lowasa,Membe,Sita nk wanafahamika kuwa wametumia nguvu kubwa na rasilimali nyingi,jee watakubali kumwachia "wakuja" kirahisi tuu eti kwa vile anaungwa mkono na akina Mwigulu?
Au watamwogopa kwa vile Zito anatembea na orodha ya mabilioni ya Uswiss "mfukoni".
Nimeleta swali hili la kizushi baada ya kukumbuka hadithi ya Mwarabu na ngamia aliyeomba kuhifadhi kichwa tuu ndani ya banda wakiwa jangwani. Jee huo muziki utakuwaje?