Waraka uliowaondoa Zitto Kabwe na Kitila Mkumbo CHADEMA huu hapa

Waraka uliowaondoa Zitto Kabwe na Kitila Mkumbo CHADEMA huu hapa

Zitto anzisha chama chako, usiende kwa magamba! I will support you to the end!! Achana na hao wenye wachumba uzeeni na vilaza
 
Wewe endelea kulalama lakini mizizi ya CCM ndani ya Chadema imekatwa ingawaje bado mmoja lakini huyo naye atajulikana muda si mrefu. Na kazi yote hii ilikuwa inafanyika kwa kutumia bajeti ya pesa za walipa kodi zilizokuwa zinatumwa ujerumani na ikulu na baadae kumrudia Zitto. No wonder Wassira alikuwa anatamba kwamba CDM itakufa kabla ya 2015. Wakajipange upya.

Tiba

Huyo mmoja ameshaandika barua ya kujiuzulu. Huu ni wakati wa kurudisha umoja wetu ktk chama.
Mungu mkubwa aisee, vinginevyo tulikuwa tunaizika Chadema hivi hivi.
 
NasDaz , kwa jinsi Lissu alivyoripotiwa kusema, ni wazi kuwa jambo hili lilianza "kushughulikiwa" kabla hata ya kikao kilichomalizika. Tunaambiwa MM na M1 waliomba kujiuzuru kama njia ya "kuwajibika" kwa kadhia hii. Lakini walikataliwa kwa sababu kwa kitendo walichofanya hawakustahili "heshima" ya kuachwa wajiuzuru bali "kuwajibishwa" kwa kuvuliwa nyadhifa zao. Labda swali kubwa ni kwa nini walionba kujiuzuru kama ni kweli hawahusiki (actively) kama waraka unavyoonesha? Mimi naamini kulikuwepo na ushahidi mwingine zaidi ya waraka huu - mawasiliano,nyaraka zingine au hata uliotokakana na kuhojiwa kwao - ushahidi ambao kwa mtu "muungwana" kulikuwa hakuna namna nyingine zaidi ya kuomba kujiuzuru.

Pamoja na nia "ovu" ya waraka huu, bado naamini una mambo mazuri na ya msingi kwa CDM. Ni siasa za kisasa! Inatia moyo sana kuona watu wskitumia models (SWOT) kutengeneza mikakati ya kisiasa. Sasa waisaidie CDM kuchukua dola 2015. Hizo analysis zinaweza kufanywa kwa "uwazi" zaidi kwa chama kujitathmini na hata kutathimini mazingira ya nje.
 
Last edited by a moderator:
Kwakweli haya ni matusi makubwa kwa viongozi wetu...na hata sisi wananchi,kama Mbowe na elimu yake ya kidato cha sita,uzoefu mkubwa wa kiuongozi anaitwa AKILI NDOGO, sisi wa darasa la saba tulio wengi si ndo tumetukanwa zaidi?
Hawafai kuwa viongozi kutokana na dharau walizonazo...
Pia wapi wanapata fedha za kutekeleza mipango yao?au ndo ule waraka Yericko ulivyotueleza jinsi ZZK anavyopewa hela na magamba?
 
kiza kinene naanza kupatwa na wasi na CHADEMA chama nilichotegemea kukiondoa CCM! yangu mimi ni maswali mawili tu!
kwa nini matumizi na makusanyo hayahakikiwi kwenye chama na taarifa kutolewa? Na pili kwa nini uchaguzi huru haufanyiki? Na tatu kwanini maaamuzi au maafikio ya kamati kuu huwekwa kando?

Kiukweli naona waraka huu wa Kitila na Zitto hujalenga kuvunja chama bali kutaka mabadiliko chanya kwenye uendeshaji wa chama na kama viongozi wakuu wamehamaki na kuamua kuwavua vyeo hawa wawili basi kuna jambo nyuma yake! yangu mi macho ila dalili ya mvua ni mawingu na yaliyokiua NCCR Mageuzi yatakiua CHADEMA kama hawataacha demokrasia ifuate mkondo wake.
 
kwanza na-declare interest yangu. mimi ni mmoja wa wengi wetu ambao ni "chama-less" tuliojichokea na ukiritimba wa CCM, na hivyo tumejikuta tukiitegemea sana Chadema kama ndiye mbadala.

pia nikiri kabisa kuwa mimi binafsi siuoni kabisa mkono wa CCM kwenye waraka (or rather mpango) huu. it looks to me like a document that has been worked out by a genetically pure Chadema germ.

hata hivyo ninaelewa na kukubaliana na ukweli kwamba jambo lolote, hata likiwa ni zuri kwa kiasi gani, likifanywa kwa kificho lazima litapelekea mtikisiko kwa community husika.
hiki ndicho kilichotokea kwa Chadema.....i.e watuhumiwa wenye nia njema kabisa na taasisi yao wamefanya mambo clandestinely lakini kwa bahati nzuri/mbaya wamekuja kugundulika.

kwa mtizamo wangu, huu waraka una maudhui mazuri sana lakini una mapungufu makubwa ya kimkakati (tactical deficiency) kwa waandaji wake. waandaji hao wanaonekana kuelewa sana walichotaka kukifanya lakini hawakuwa smart...they goofed it big time (and this am particularly addressing to my good friend Dr Mkumbo, going forward).

nikirudi kwa uongozi wa Chadema, mtizamo wangu ni kuwa maamuzi yao dhidi ya watuhumiwa yamekuwa equally poor or worse. huwezi kuchukua maamuzi waliyochukua Chadema with general elections beckoning only 2 years away halafu utegemee eti kushinda uchaguzi huo. itakuwa ni vigumu sana au pengine impossible kabisa. hii inatukatisha tamaa sana - tena sana tu - sisi tunaowategemea.

kuna positives nyingi kwenye waraka huu ambazo uongozi wa Chadema ungeweza kuzichota na kuzifanyia kazi kwa ajili ya kukipeleka chama mbele. daima tukumbuke kuwa, kwa mfano, kwenye football match spectators huwa wanayaona vizuri zaidi makosa ya wachezaji walioko ndani ya pitch kuliko wachezaji wenyewe wanaocheza. hawa watuhumiwa ni kama spectators na ninyi viongozi ndiyo wachezaji - you should (or rather you could) have used approach mbadala anuai za kuwawajibisha watuhumiwa bila ya ku-create drama hii tunaishuhudia leo.
nakubaliana nawe kabisa. Umekuwa balanced ktk analysis yako. Kwa maoni yangu kamati kuu imekuruouka katika kufanya maamuzi. Natamati michangi ya wana JF humu ingeonyesha kutabua kuwa watuhumiwa wanabakia kuwa watuhumiwa mpaka baada ya hizo siku 14. Kwa sisi wanachama wa kawaida tunatskiwa kuwa wavumilivu kwa matarajio kuwa uamuzi uliofanyika ni sahihi. Hata kama hatimaye itathibitika kuwa kamati kuu ilifanya makosa bila kudhamiria tutawasamehe. Ni imani yangu historia itahukumu pande zinazokinzana kwa haki.
Viva CDM.
 
Siyo dhambi kutofautiana kimawazo na siyo dhambi kugombea uongozi na hivyo kufanya hivi basi wote waachie madaraka narejea kauli ya MM mwanakijiji aliwahi kusema na kushauri chadema wafanye nini kwa mwenyekiti!! kwa kiasi fulani hizi tuhuma ni kwa ajili ya uchaguzi ila kuna mambo mengine yana ukweli na siyo sahihi kumvua uongozi eti kwa kusema ukweli
 
Ukiyafuatilia maelezo yao utagundua kuwa yale wanayoyaponda pia na wao wanampango wa kuyafanya. Kwa mfano wanaponda uongozi kukaa kimya na mwisho nao wanasema haitakiwi mm kujibu kila hoja zinazojitokeza. MUNGU HAMFICHI MNAFIKI NA HONGERA CDM KWA MAAMUZI MAGUMU!
 
What is wrong with this political strategy? Absolutely nothing. Yataka moyo kuwa mwanachama wa chama cha siasa, kama kuwa na strategy ya kuweka mtu mnayemtaka ni kosa tosha la kufukuzwa uongozi/ uanachama. Hii mambo ya group thinking imeshajikita hadi katika vyama vya upinzani. Kuwaza tofauti na upper echelon unafukuzwa tena kwa kudharililishwa. Ni amani sana kufuatilia siasa za Tanzania ukiwa raia asiye mwanachama wa vyama hivi.
 
Kazi ya siasa za kinafiki ni kupambana na ukweli na uwazi.

Sijui taratibu, itifaki, kanuni na katiba ya CHADEMA inasema vipi kuhusiana na madhumuni na njia zilizotumika kutengeneza waraka kama huu lakini kikubwa cha kujiuliza, hizi content za kwenye waraka ni kweli?. Je, yaliyosemwa kwenye waraka ni kweli?

Kama yaliyosemwa ni kweli, basi lipi ni kosa kubwa kati ya yaliyosemwa kwenye waraka na njia iliyotumiwa kutengeneza waraka. Nini adhabu zake katika taratibu, kanuni na katiba ya CHADEMA.

Ni kweli huwezi kuharalisha kosa kwa kutenda kosa lakini vile vile, huwezi kukaa kimya na kuharalisha kosa.
 
Aisee kama hivi ZZK hawawezi kumng'oa CDM sema kuna uchocheaji kutoa southern block si vibaya kuzungumzia katiba ya chama katika suala la uchaguzi wa viongozi,na sio vibaya kugombea nafasi kwa mbinu anazozijua yeye ndani ya chama so long as tena ALIAHIDIWA kwa staili hii DJ MBOWE ndo tatizo ndani ya chama na amini usiamini CDM itakufa kwa staili hii ya kung'ang'ania madaraka na HATUTAWEZA kuing'oa ccm kama tunapita kwenye mkondo wa dhambi zilezile za magamba

Je Mbowe hayuko madarakani kihalali? ni upi ushahidi wa kungangania madaraka wakati kipindi chake bado?
kuahidiwa tu, mbona JK aliahidi maisha bora na ahadi lukuki na hajatimiza.
Hongera CDM kwa kuchukua maamuzi sahihi na magumu na ndicho kinachowatofautisha na wale wafanyao madudu magamba wanawahamisha kituo chakazi ili wapate kutapanya uchafu wao
 
Mbinu hizi wengi watasema nizakijinga watakuwa wamekosea saana, Tanzania imepata marais wawili kwa mbinu hii nyepesi, Angekuwepo Nyerere angezuia ingebaki moja aliyofanyiwa na wasaidizi wake, Wengine walioshindwa vibaya kwa mbinu hii ni Prof. Mwandosya, Mzee Malecela, Dr Kigoda, na sasa anaeonekana kuitumia saana ni Mh Lowasa,
 
Uchambuzi: Baada ya kuisoma kwa kutulia huu waraka yaonyesha wazi kwamba muandishi wa ile "RIPOTI YA SIRI" ndie huyo huyo alieandika waraka huu.

Cha kujiuliza ni kwamba kwa nini hawakukubali kuwa chama ndio kiliisuka ile RIPOTI YA SIRI? Kuna senario mbili tu za msingi hapa.
  1. Mh Zitto alikuwa mjanja na alipoupata ule waraka wa Ripoti ya siri akatuma vijana wake waumwage mtandaoni kuwapima viongozi wa CHADEMA (wasukaji-Mbowe, Slaa na Lissu) watasema nini. Zitto alifikiri hiyo ndio njia nyepesi ya kuwanyamazisha.
  2. Viongozi wa CHADEMA (Mbowe, Slaa na Lissu) waliisambaza Ripoti hiyo mtandaoni ili kujua na kupima reactio ya Zitto na kikosi chake na hasa reaction ya wanachadema. Walipoona wanachadema wengi hakumuunga mkono Zitto ndipo wakasuka huu Waraka wa kitoto ili wammalize Zitto na Kitila.

Hiki ni chama cha siasa au chama cha FITINA? CHADEMA IMEKUFA. NIMEWASIKIA MBEYA NA KIGOMA HAWATAKI KUISIKIA CHADEMA TENA. WANAMPANGO WA KUANZISHA CHADME2.

Hivi hiki CHAMA kingechukua nchi 2010 si kingetutosa BAHARINI. Lo ewe Mungu epusha majanga haya.
 
Chadema wamepokea mtazamo HASI huu waraka,mimi nataka CDM ijibu hoja zote za kwenye waraka,ingekuwa siokweli wasingepaniki
 
Back
Top Bottom