Waraka uliowaondoa Zitto Kabwe na Kitila Mkumbo CHADEMA huu hapa

Waraka uliowaondoa Zitto Kabwe na Kitila Mkumbo CHADEMA huu hapa

Tatizo mbowe na slaa wana kinyongo na zitto... Kaza buti jembe zitto tuko nyuma yako
 
Tatizo mbowe na slaa wna kinyongo na zitto mtoto wa kanda ya ziwa... Tuko pamoja jembe zitto
 
Kama unaelewa kilichosukwa na kuimaliza NCCR - Mageuzi kilipokuwa na nguvu kama ilivyo CHADEMA kwa sasa, basi huna haja ya kujiuliza maswali mengi na kujiumiza kichwa bure.

Yale yaleeee ya Yuda Iskariote na vipande 30 vya fedha!


Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums

Usaliti ni aina ya siasa uchwara.... Unajua wengi hawajui ukweli kwamba "uongo" hua hauna nguvu hata km dola ipo nyuma yake .... MUNGU alichagua kuishi katika ukweli na hua inashinda bila hata ya kusemewa.... Wote watakao jiunga na uongo huu wataanguka na kila mtu atajua.... ni ajabu jinsi Zitto alivyo maarufu kwa wanaCCM kuliko alivyo kwa wanaCDM ....?!!!
 
Waraka huu ni kichekesho cha karne!
This is rubbish and should be discarded into the Dustbin! Hakuna mtu mwenye mapenzi na CHADEMA anaweza kuandika ujinga kama huu hata kidogo.

Kwa GT yeyote huu WARAKA UMEANDALIWA NA AIDHA USALAMA WA TAIFA, WATU NDANI YA CHAMA WANAOTAKA KUKISALITI CHAMA AU KIKUNDI MAALUMU CHA WANA-CCM wanaotaka kuona CHADEMA ikifikia tamati ili kuondisha upinzani mkali mwaka 2015!

Nawaomba Viongozi wa CHADEMA someni waraka huu kwa makini(read between the lines)na mnaweza kujua kabisa utakuwa umetoka wapi na kwa nani. Who is MM, M2 and M3? It sounds like the same faces who are behind all these movements of KILLING CHADEMA AT ANY COST B4 2015!

Hawa wanaosema wanapanga kumchagua MM awe ndiyo Mkuu wa CHADEMA ni kina nani kama siyo UWT na CCM yao na mlengwa wa Ukuu huu akiwa huyu jamaa ambaye alisha onyesha nia ya kukalia Ukuu huo tangu siku nyingi?

There are some people,some where doing something very fishy for a total destruction of CHADEMA. But I do believe they shall never succeed. Our motto should be IN GOD WE TRUST. Long live CHADEMA, long live Tanzania,God bless CHADEMA,GOd Bless Tanzania.
 
Siasa za ubabe, Chadema walikuwa wanaelekea mahali lakini kwa hili wamejivunja miguu. Mgogoro huu ulikuwa na fursa nzuri kwa chama kama wangeamua kuangalia tatizo liko wapi kuliko kufukiza watu wanaosikilizwa na wananchi

hiyo ndo tofaut ya ccm na cdm hii ya kuogopa kuwajibisha watu ndo udhaifu wenyew
 
Huu waraka una tatizo gani? Kwani Kikwete alipata je urais? Hivi huyu si alikuwa anaweka mikakati yakuchaguliwa kwenye vikao vya chama? Whats wrong with this?
 
Uhaini huu uliwahi kutokea mwaka 1984 ambapo Aboud Jumbe na wenzake walikuwa na waraka wa siri wa kumpindua Nyerere kwenye suala la Muungano.Kabla ya kutumika waraka ule ulinaswa,na kabla ya kutumika waraka huu umenaswa.Intelijensia ya Nyerere inafanana kabisa na intelijensia ya Chadema.Ikaitishwa halmashauri kuu ya CCM Dodoma mwaka 1984 kujadili waraka ule wa Aboud Jumbe,na imeitishwa Kamati kuu ya Chadema,Blue Pearl,Ubungo plaza Dar es salaam kujadili waraka huu wa Zitto Zuberi Kabwe (MM).
Maamuzi ya Halmashauri kuu ya Ccm mwaka ule ilikuwa ni kuwavua nyadhifa zao(Jumbe na wafuasi wake kina Mohamed Faki) pamoja na kuwafuta uanachama hadi leo.
Maamuzi ya kamati kuu ya Chadema ni kuwavua nyadhifa zao zote(Zitto Zuberi Kabwe na wenzake kina Kitila) na kuwapa siku 14 wajieleze kwa nini wasifutwe uanachama.
Ndugu zangu matukio haya yanafanana sana nami naamini ili kukamilisha usawa huu ni lazima hawa majambazi wafukuzwe uanachama.
Hongera intelijensia ya Chadema.
 
Ieleweke this was not a public document. limekuwa public pale tu jamaa mmoja ilivyoaamua kuvunja katiba kipengele cha privacy na kutoa document za mtu.
 
Sioni tofauti ya waraka huu na ule mwingine wa ripoti maalum kuhusu zitto kabwe, tofauti yake ni kuwa ule ilikuwa ni riwaya wakati hii simulizi. Anyway, tutafika tu. Tusubiri na upande wa pili wanasema nini.
 
Ukifanya summary ya haraka haraka, waraka una takeiban kurasa 12 hivi na yafuatayo ndiyo yaliyochomoza zaidi:-

1) Utangulizi

Wanamtandao waliweka falsafa yao. Sambamba na hilo wakijikita ktk kubuni na kutumia neno "taasisi" badala ya neno "chama". Pia dhana yenye kubeba ujumbe wa "uchaguzi wa nafasi ya mwenyekiti" uliwekwa bayana na kwa msisitizoi.

2) Hoja za wanamtandao ni 11 hivi. Kisha wakafanya SWOT analysis na baadaye wakaweka mkakati na hitimisho.

3) Performance kwenye chaguzi ndogo. Wameonesha kuwa "taasisi" haikufanya vizuri na walitoa mifano ya kati ya 2010-2012. Kwa makusudi hawakuweka matokeo ya Juni 2013! Pia hawakugusia changamoto/matatizo yaliyopelekea matokeo kuwa yalivyokuwa bali walijikita kwenye "ubaya" na si vingenevyo.

4) Matumizi ya fedha za taasisi. Hili linajulikana na kila mwana JF kwani matumizi ya maneno, mtiririko wa hoja, mantiki nk vinalandana sana na tuhuma zilizoletwa na akina Shonza, Tuntemeke et al na hivi karibuni na Bw. Samson Mwigamba. hata

4) Taarifa za fedha: hili nalo kama namba 3 linajulikana kwani lilishaletwa na kujadiliwa mara nying hapa jamvini na kwenye media za ndani.

5) Uchaguzi wa ndani (hasa nafasi ya m/kiti): Hili nalo kwa hisani ya "Mkulima Maskini" aka Mwigamba mlikwishalipata.

6) Udhaifu wa Mh. Freeman Mbowe: Hapa kuna tuhuma nzito za yeye kuingilia shughuli za kiutendaji za taasisi na hata kudhaniwa kuwa anafaidika binafsi na mfumo huo.

7) Matumizi mabaya ya madaraka yanayoweza kuhusishwa na ufisadi: Hapa ni mwendelezo wa kipengele No. 6 wenye muktadha wa "uchaguzi na hasa nafasi ya m/kiti" Hapa zimetolewa shutuma nyingi za jinsi manunuzi ya vitu/vifaa, taratibu za manunuzi ya ndani nk zilivyo kiukwa. Aidha kama ilivyo ada F. A. Mbowe ndiye MM (Mtuhumiwa Mkuu); Zitto yeye ni MM (Mhusika Mkuu) sorry for confusing abbrevs!

8) Nani wamuunge mkono (kama mtandao wao wanamtaka nani): Wakatengeneza sifa za mtu wao vs Mbowe.
Eneo hili lilijaa kashfa, dharau, kejeli na propaganda ambazo humu jamvini akina Shonza, Tuntemeke & Mtella wataona fahari kuhusishwa nazo.

9) SWOT analysis: Hapa walijikita ktk kumnadi na kumpamba MM. Uchambuzi ulihitimishwa kwa MM kupata "A-pass marks" na hivyo kuweka mazingira ya MM kuelekea "king".


10) Mtandao wa ushindi: hapa wakaweka mikakati ya namna ya kumpeleka MM "king". Kifupi waliweka structure/miundo mbinu kufanikisha malengo yao. Jambo kubwa linalojitokeza ni namna watakavyotumia chaguzi za taasisi ktk ngazi zote kuweka watu wao. Hili lingeendelea toka ngazi za misingi mpaka kanda na baadaye MM angeingia kingi.

11) Mwenendo wa MM kuanzia sasa, walikusudia yafuatayo
a) MM apunguze ukaribu na viongozi wa CCM na awe mkosoaji wa utendaji wa serikali bungeni na nje ya bunge.
b) Ashiriki kikamilifu shughuli za CHADEMA (?), zikiwemo vikao VYOTE vinavyomhusu, opereshini mbali mbali, chaguzi ndogo nk
c) Aendelee kushusha "nondo" bungeni
d) Ajitahidi kupunguza jazba. Ashauriane na "wazee" (?) kabla/namna ya kujibu tuhuma mbalimbali
e) Kuwawezesha M2 na M3 kifedha, ili kuongeza ufanisi wao ktk majukumu waliyopangiana.

Kwa ufupi (summary) hayo ndio yaliyomo kwenye waraka husika (iwapo utathibitishwa).

Wadau karibuni kuboresha summary kwa kukosoa na/au kuongezea
 
sasa humu kuna nini? daa Tundulissu katumika.

Duuuh! Kama ni kweli haujaona kitu kwenye nondo ya kimaangamizi kama hii! Basi wewe unaweza kumkimbilia chui ukizani paka au kumpiga teke nyoka mchana kweupeee ukimzani mjusi.Loooh! Hovyoooooooo
 
sioni tofauti ya waraka huu na ule mwingine wa ripoti maalum kuhusu zitto kabwe, tofauti yake ni kuwa ule ilikuwa ni riwaya wakati hii simulizi. Anyway, tutafika tu. Tusubiri na upande wa pili wanasema nini.

nampa hongera sana. Na aendelee la moyo huo.
 
Wakati Tundu akiongea na wanahabari sina shaka kabisa kwamba waraka huu ndio aliouzungumzia. Kwa jinsi vile hukumu zilivyotolewa, sina shaka kabisa kwamba hukumu hizo zimetokana na waraka huu! Hata hivyo, pamoja na kwamba nimesoma waraka mzima, bado sijaona ni namna gani unaweza kumhukumu Zitto kupitia waraka huu. Kimsingi, baada ya waraka kuzungumzia udhaifu wa uongozu uliopo hususani Mwenyekiti, waandaaji wa mkakati huo wameona njia muafaka ni kuandaa mkakati utakaofanikisha kumuondoa Mwenyekiti aliyopo na kuingizwa yule anayeonekana kufaa(MM-Zitto Kabwe) Baada ya wanamkakati kufanya SWOT Analysis kuhusu MM (Zitto), wakabaini moja ya THREAT ni kwamba:
SWOT ANALYSIS:
Vikwazo dhidi ya tunayemtaka:
Sisi wenyewe tunaoandaa mkakati huu hatuna uhakika kama tunayemtaka yuko tayari na yuko serious na business hii, na kwa hiyo huenda tusifanye kwa nguvu zetu zote ikiwa hatutapata nafasi mapema ya kukutana na mhusika na akatuhakikishia kwamba yuko serious.

Utayari wa mhusika mkuu kutekeleza yale tunayokubaliana. Inapotokea baada ya kukubaliana sisi na yeye akapata ushauri tofauti na ukauona uko more genuine, basi tuwasiliane kwamba nimeshawishika kufanya hivi badala ya vile tulivyokubaliana kwa sababu hizi ama zile. Hii haitatukatisha tamaa tofauti na kama tutakuwa tunapanga hivi halafu yeye anafanya vile bila maelezo yoyote
Kutokana na maelezo hayo hapo juu, ikiwa unataka kuhukumu kupitia Waraka wa kumchafua Mwenyekiti, utagundua kwamba wakati haya yanafanyika Zitto alikuwa bado hajashirikishwa. Na katika kuthibitisha hilo, wanamkakati hawa hapa:
MTANDAO WA USHINDI:
Mtandao wa ushindi utakuwa kama ifuatavyo. Kwenye ngazi ya kitaifa tutakuwa na kamati yenye members watatu tu. M1 ndiye atakayekuwa anawasiliana na tunayemtaka ambaye ataitwa MM (Mhusika Mkuu). Tumepanga kwamba kusiwe na mawasiliano mengi kati ya kamati na mhusika mkuu kuepuka tracking ya wapinzani wetu. M1 ni mtu wa karibu na MM kwa hiyo mawasiliano yao hayataweza kutiliwa shaka na mtu yeyote hata wangewasiliana mara nyingi kiasi gani. Hata hivyo, linapokuja suala la mkakati huu tunasihi mawasiliano yawe kwa kuonana uso kwa uso ama kwa simu na si sms.
Hapo panathibitisha wazi kwamba MM (Zitto Kabwe) bado alikuwa hayupo kundini na kumbe tu kulikuwa na mkakati wa kumwingiza kupitia M1(Dr. Kitila Mkumbo) ambae ametajwa kwamba ni mtu wake wa karibu. Je, M1 alishafanikiwa kum-recruit MM? Waraka huu hausemi hivyo, kwa hiyo bila shaka njia pekee ya kufahamu kwamba M1(Dr. Kitila Mkumbo) alishamfikia MM(Zitto Kabwe) ni kuangalia viashiria fulani fulani na hapo ndipo mtu unaweza kupata picha kwamba bila shaka sasa ni wamoja! Ukiusoma Waraka wa Mkakati, sehemu moja ya waraka huo inaweza kutoa viashiria tunavyotaka; hivi hapa chini:
Kuhusu mwenendo wa MM kuanzia sasa:
Ni maoni yetu pia kwamba kuanzia sasa MM aenende katika mwenendo ambao utarahisisha ushindi. Mfano tunapendekeza afanye yafuatayo kuanzia sasa:

Apunguze ukaribu na viongozi wa serikali na wa chama tawala na awe crical zaidi na utendaji wa serikali nje na ndani ya bunge.
Je, Zitto Kabwe amepunguza ukaribu wake na watawala pamoja na wana-CCM kiasi cha kutushawishi kwamba M1 alishamfikia na akafikika na kwamba kazi sasa inaanza kwa vitendo!
Ashiriki kikamilifu katika shughuli za taasisi yetu zikiwamo vikao vyote vinavyomhusu, operesheni mbalimbali, chaguzi ndogo, nk.
Je, hivi sasa Zitto anashirik shughuli za CHADEMA zikiwemo vikao vyote vinavyomhusu ili turidhike kwamba M1 alimfkia MM na sasa ndo wapo kwenye implementation phase.
Aendelee kushusha ‘nondo’ ndani ya chombo chetu cha uwakilishi na kuendelea kuwa juu ya wawakilishi wengine katika hoja mbalimbali zenye maslahi ya kitaifa.
Je, MM anashusha nondo bungeni ili tujiridhishe kwamba alishafikiwa na M1? Mbona sikumuona akimwaga povu kwenye issue ya Operation Tokomeza? Mbona sikumsikai akimwaga nondo kwenye issue za mabadiliko ya katiba?
Ajitahidi kudhibiti jazba hata pale anapokuwa amebambikiziwa tuhuma nzito namna gani. Atulie, ashauriane na wazee ili kuona namna nzuri ya kujibu tuhuma zinazomkera. Tukumbuke kwamba wakati mwingine kukaa kimya ni jibu zuri zaidi kuliko hoja nzito.
Je, Zitto Kabwe ameanza kufanyia kazi kiashiria hicho hapo juu ili tushawishike kwamba alishafikiwa? Je, ameanza kukaa kimya hata baada ya kurushiwa kombora? Je, kule kumlima barua hivi majuzi Dr. Slaa tunaweza kuita ndo kukaa kimya? Je, si ni hivi majuzi tu alipoingia kwenye malumbano na Lema?
Sambamba na ‘iv’ hapo juu, adhibiti sana emotion ili kuhakikisha kila kitu kinachofanywa ama kuzungumzwa kinachomgusa asikimbilie kuongea na vyombo vya habari ama kwenye mitandao ya kijamii bali afuate kile tulichokizungumza kwenye kipengele cha ‘iv’ hapo juu.
Je, Zitto Kabwe ameshaanza ku-contro emotion zake? je, ameacha kukimbilia kuongea na Medias hadi tushawishike kwamba alishafikiwa na M1 na sasa anatekeleza maazimio? Hivi lile sakata la Zitto kumlima barua Dr. Slaa lilifahamika vipi? Ilikuwaje hadi magazeti yakaandika kama si Zitto aliongea na Media?
Hata hivyo, ni muhimu kukumbushana kwamba wenzetu hawatanyamaza kwa sababu eti sisi tumeacha kuwashambulia kwenye mitandao ya kijamii. Lazima wataendelea! Wataendelea kumchafua MM kwa kupitia wapuuzi kama yule kichaa wa ‘ars’ na kundi lake. Nini tutakuwa tunakifanya sasa? Tutahakikisha tuko busy kupost mambo mema na mazuri yatakayokuwa yakifanywa na MM kila wakati na kuzidi kusambaza sifa zake njema kila inapotokea nafasi.
Je, mambo mema ya Zitto yameshaanza kuwa posted humu ili tufahamu kwamba MM alifikiwa na akafikika na sasa ametoa rukhsa ya kupambwa kwa maua na mapambio?! Mbona mie nimeona moja tu? Lile la kutaka "kuwataja mabilionea wa Uswis?" Ajabu aliyeleta habari hiyo ni Mungi, ambae naamini hayupo kambi ya Zitto!! Au Mkuu Mungi unatuzuga tu hapa jamvini na labda wewe ndie M2 na ukaleta uzi wa Mabilioni ya Uswisi ili kumpaka mafuta MM? Lakini wewe haupo HQ bhana ambako ndiko aliko M2; sasa mbona hayo mazuri na sifa zilizotukuka za Zitto hazijaanzakumwagwa ili tushawishike kwamba "kazi imeanza?"
Kuhusu kamati ya kitaifa (hususan M2 & M3):
Tulikubaliana kwa kauli moja kwamba katika kutekeleza mkakati huu tunahitaji members hawa wawe wametulia kimaisha. Inakuwa vigumu kwa mfano kumtaka member aende mahali fulani kwa makusudi ya mkakati huu wakati hajui familia yake nyumbani anaiacha inakula nini. Tuliona kwamba M3 tayari hana kazi kwa sasa tena kwa kufanyiziwa na wakuu waliopo.
Alaah! Kumbe huu mkakati ni wa juzi juzi tu hapa baada ya kuwa M3 (Samsoni Mwigamba) akiwa tayari ameshafutwa kazi!!!
 
Last edited by a moderator:
Hawa jamaa na ushahodi wa kuelea elea! Hapo cdm wamejipiga risasi wenyewe
 
Acheni ushamba,muvi hyo...kama maandamano hakuna tena,unafikir wataskikaje?
lengo nikumek headlines,mwsho wa sku wata'act wanamwita zto ajtetee issue inaisha haf chama linasonga.
 
wale wapenzi wa Zitto njooni muokoe jahazi maana linazama .....mshaurini asinadike kitu chochote fb or twitter kabla hamaja mshauri.....
 
Back
Top Bottom