Waraka uliowaondoa Zitto Kabwe na Kitila Mkumbo CHADEMA huu hapa


Unakosa consistency hapa kijana.Ijui ndio panic au?Umesema hao jamaa zako ndio wneye chama nikakupa majibu.sasa kabla hujahitimisha unakimbilia lingine au umeona kuwdai ndio wenye chama haiina mshiko tena?

Kodi yako unalipa CCM au unalipa CDM?Kwanza wewe hufanyi kazi ya kulipa kodi.ZItto alikuwa akiwakata kodi?au hata mwigulu na wengine wanakata kodi?je una hakika wanaifiksiha au ni chao cha juu?

Kwanza lini usaliti umehalalishwa kiasi cha kuingiza kodi.Ni wazi TRA watakuwa wamepanua sana wigo wa kodi,pengine sasa hata wanawake wanaotoka nje ya ndoa, na wengine wa jinsi hiyo watalipa kodi kubw asna ktk hii nchi.
 
Re: Kuvuliwa uongozi kwa Zitto; CHADEMA Mmejipangaje kuepuka propaganda za UDINI na Ukanda zidi yenu
Katika hili, "Tuwe werevu kama nyoka lakini wapole kama hua." Tutashinda!


Reply Reply With Quote Send PM
Haki sawa
Today 02:47 #147
JF Senior Expert Member
Array
Join Date : 4th October 2007
Posts : 668
Rep Power : 9404
Likes Received
544
Likes Given
6
Tafsiri ya Udini na Ukanda wa CHADEMA kwa hatua za Kamati Kuu.
Kikao cha Kamati Kuu ya Chadema kilichomalizika juzi na maazimio yake kutangazwa jana kiliamua kuwavua Uongozi wajumbe wa Kamati kuu wawili ambao ni aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu , Mhe .Zitto Kabwe na Dr. Kitila Mkumbo.
Aidha kilimvua madaraka ya uongozi aliyekuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Arusha Samsoni Mwigamba .


Ukiangalia kwa umakini uamuzi huo wa Kamati Kuu utaona kuwa kwa upande wa dini , Ukabila , Mikoa na Ukanda utaona ifuatavyo;


Zitto Kabwe , huyu ni Muislamu, Kanda yake ni Magharibi , Kutoka Mkoa wa Kigoma , Kabila lake ni Muha.....


Dr.Kitila Mkumbo, huyu ni Mkristo, Kanda yake ni ya Kati, Kutoka Mkoa wa Singida, Kabila lake ni Mnyiramba .....


Samsoni Mwigamba, huyu ni Mkristo, kanda yake ni Kaskazini, Mkoa wa Arusha ( ndio alikuwa Mwenyekiti wa Mkoa) , Kabila lake kwa kweli sijui, ila Nina uhakika kuwa huyu sio Muha wala sio Mnyiramba.


Ukafanya uchambuzi ambao sio biased , kwa vyovyote vile utaona kuwa kwa upande wa dini, Muislamu yuko mmoja na Wakristo ni Wawili.Hii ni sawa na kusema kuwa 75% ni Wakristo ndio wamepunguzwa Chadema na 25% ya Waislamu ndio wa epunguzwa kwa maamuzi hayo, huwezi kusema kuwa kulikuwa na ajenda ya kuiumiza dini moja , ila dini iliyoathirika zaidi ni Wakristo kwa kuwa ni asilimia 75% ndio wameathiriwa na maamuzi hayo.


Ukija kwa upande wa Ukanda unakuta kuwa Kanda ya Magharibi imeathirika kwa 33.33% , Kanda ya Kati imeathirika kwa 33.33% na Kanda ya Kasikazini imeathirika kwa 33.33% , hivyo maamuzi hayo haya kufanyiwa kwa misingi ya Ukanda Kwani kila Kanda imeathirika kwa kiwango sawa sawa, huwezi kutoa conclusion kuwa kulikuwa na ajenda ya Ukanda katika maamuzi yaliyofikiwa.


Ukitazama maamuzi hayo kwa Dhana ya Mikoa , utakuta kuwa hakuna Mkoa ambao uliathiriwa kuliko Mkoa mwingine Kwani kila Mkoa umeumia kwa kiwango sawa yaani Singida 33.33%, Arusha 33.33% na Kigoma 33.33% , hivyo unaweza kufikia conclusion kuwa hapakuwa na Mkoa ulipokuwa umelengwa Mahususi , ndio maana maamuzi hayo haya wezi kuitwa yalikuwa ya kuumiza ama kupendelea Mkoa fulani.


Ukiamua kuyatazama maamuzi hayo kwa misingi ya Ukabila unakuta kuwa hapakuwa na Kabila ambalo lililengwa Mahususi, kwani hapakuwa na Kabila moja lililoumia kuliko Kabila lingine , yaani kwa kupoteza idadi kubwa ya wajumbe kwenye vikao vya Chadema .


Hivyo, basi nawataka wale wote ambao wana jengo hoja kuwa uamuzi huu ulikuwa ni kwa misingi ya Ukanda, Udini na au ukabila wathibitishe madai yao kwa facts na sio kwa hoja nyepesi na Propaganda za kizamani kama ambavyo wanafanya kwenye kujenga hoja zao ili Jukwaa hili liweze kuwa na heshima yake ya miaka hiyo .


Aidha, kwa wale ambao tunaamino kuwa maamuzi hayo yalifanywa kwa misingi ya haki na kwa lengo la uwajibikaji,tunaamino kuwa hatua ya Kamati Kuu ilikuwa sahihi nailizingatia merits na sio kwa kutazama jambo lingine lolote lile.


Mwenye hoja unakaribishwa kwa mjadala wa Nguvu ya Hoja na sio Hoja za nguvu , kama unafikiri kuwa IQ yako iko chini please soma subiri wengine wachangie kwa kujenga hoja , Moods zingatieni hoja kwa maslahi ya jukwaa hili.


Thanks, CC, Nguruvi3, Mchambuzi, Mkandara, Mwanakijiji, Mungi, et all.
Alinda and TsafuRD like this.
 
chadema imeshakufa, thats all. Kwenye uchaguzi kunakuwa na kambi, kwann chadema ni dhambi kuwa na kambi na ni dhambi kutofautiana kimawazo na mtizamo?

nadhani ukilia kwa malengo yako kukwama ndani ya chadema hasira zote zitakwisha kwa leo.
 
Hujalazimishwa kuwa mwanachama na huwezi kujua kosa la zitto kama wewe sio mwanachama, mambo ya vyama tuachie wanachama we endelea na mambo yako binafsu.
 
Kiukweli huu waraka uwe wa kipropaganda au kimkakati umefanikiwa kuichambua CDM hasa. Na asilimia kubwa ya vilivyoongolewa tunaviona vikitokea ndani ya CDM. Mi nilidhani wangeanza kufafanua hoja hizi kisha kuchukua hatua. Kama kazi hii ni ya kina Zito basi hawa watu ni viongozi makini sana maana uchambuzi wao umeonyesha mapungufu yanayothibitika kabisa ndani ya CDM......ila najua ukipenda utasema chongo, wanaCDM amkeni mukiokoe chama chenu wacheni kujificha kimbuni kimbuni oooh!!!
 
Kwa nchi kama iran,china zitto kitila ni wa kunyongwa pale jangwani!zitto anatamaa ya pesa balaa waraka mzima umejaa maneno uchumi,fedha
 
MM anajua kuwa hakubaliki kihivyo ndani ya taasisi na nje hata kuweza kugombea urais, ndio maana MM alihaidi kuacha siasa ifikapo 2015, hii ni ishara kuwa alijua muda wa kuisambaratisha chadema kupitia migogoro ya ndani ni kipindi karibia na uchaguzi 2015, hivyo akimaliza kazi ya waliomtuma anaacha siasa rasmi. inaonyesha anajijali yeye na familia yake tu. ana upeo hafifu wa kutenda.

huyu MM kasoma lakini hakuelimika, anahitaji ku-probate master yake, this time akasomee marekani tena ajueumuhimu wa nchi yeyote duniani kuwa na strong opposition party. shwaini.
 
Sasa ikiwa umeyaona yote haya ktk waraka huo, kwa nini wewe ndio unazidi kumchukia Zitto badala yake yeye aloandikwa ujinga wake? nilitegemea wewe ungeufurahia huu waraka zaidi maana Zitto kaonyeshwa mapungufu yake na yeyote atakaye gombea dhidi yake angetumia waraka huu kumwangusha Zitto ba kundi lake maana wametuonyesha silaha zao.

Mkuu sinema iwe ya James Bond ama Rambo hizi ni sinema tu hazina ukweli kwako wewe,mimi na watu wengineo kufikia kutishika kuishi ama kuamini maana ni sinema tu. HNa ndio maana nasema huu waraka kwangu ni sinema ambayo ingetumika vizuri ktk uchaguzi ujao kuonyesha mcheza sinema hawezi kuishi ktk hali ya kawaida inapofikia swala hilo na mazingira yale yale. Kuongoza chama sii maneno na mikakati ya usanii bali ni kazi kubwa sana inayohitaji hekima na busara zaidi.

Demokrasia imeundwa ili wananchi wachague viongozi wanaowapenda wao na sii kinyume. Demokrasia inahesabika pale wananchi wanapopewa haki hii na sio kundi la watu, hapana kilichotumika kingelenga tu Katiba imasema nini juu ya swala hili. Hapa Toronto Canada imegundulika kuwa Meya wa mji alikuwa mtumia unga, ni mlevi na mbishi lakini wananchi wanampenda tena baada ya siri hizi kujulikana ndio kapendwa zaidi kwa sababu Meya huyu anaiweza kazi yake. Ni meya pekee ktk historia ya mji ameweza ku balance vitabu,kaondoa rushwa na kujuana, posho na malipo yasiyokuwa na maana. Ametuonyesha vision yake kwa mji huu na hakika wananchi wamemkubali zaidi japo ana mapungufu mengi tu ktk maisha yake. Na unajua nini? Bado yupo madarakani na inasemekana hata uchaguzi ujao anaweza kushinda tena. Sii waziri mkuu, wala nani anaweza kumfukuza kazi isipokuwa wananchi wenyewe...

Hii ndio demokrasia mkuu wangu maamuzi hufanywa na waajiri yaani wananchi wengineo mtapendekeza tu na pengine hata kususia kushirikiana naye lakini hamuwezi kumtoa madarakani kwa sababu hakubaliani na uongozi uliopo. Ni katika mfumo wa Kidikteta na Kikomunist tu ndio unakuta kuwashambulia viongozi ni USALITI na udhabu kama hizi hutolewa lakini ktk demokrasia kiongozi yeyote anaweza kuchambwa tena kwa mawe na asifanye kitu, kinachotakiwa ni yeye kuonyesha uwezo wake zaidi ya madai yalowekwa kisha wananchi watapima wao kati ya mazuri na mabaya yake ni yapi yenye uzito zaidi!

Kundi la Zitto hata kama wangeingia na mbinu zao ktk uchaguzi ujao bado wajumbe ndio wangekuwa na uwezo wa kuwachagua ama kuwatema. Na ukizungumzia Wachawi na wahuni, mkuu wangu mbona wengi tu na wengine huwasoma humu? CDM kuna mapandikizi wa CCM wala sii hao mlowataja na wanapeta. Binafsi yangu nitasema tena maamuzi yalofanyika ni kuwapa nguvu CCM kutawala kwa miaka 10 au 20 ijayo na mtayakumbuka maneno yangu wala sii muda mrefu. Huu ni USALITI kwetu sisi wananchama maana tuliweka tofauti zetu pembeni iwe kwa Mbowe, Slaa ama Zitto na kutazama mwaka 2015. Kwetu sisi malengo ni kuchukua Uongozi wa Taifa na kuwamaliza mafisadi sio uongozi wa chama maana chama ni nyenzo tu ya kufikia malengo yetu (wananchi), hivyo uongozi wa chama ni lazima ulenge kuchukua utawala laa sivyo hatuna sababu ya kujiunga. huu sii Mpira kujenga mashabiki ambao jupewa kiini macho, watu wengine wanachukua mabillioni nyie mmekalia kushangaa ktk TV na kubeba bendera za timu.

Kati ya mada zangu humu kuna sehemu nilipendekeza mwanasheria Tundu Lissu kuwa mgombea wetu ktk uchaguzi ujao kwa maana ya kwamba nayajua mapungufu ya Mbowe,Dr.Slaa, na Zitto. sasa mtu kama miye kwa nini nisiwatazame hawa japo nawakubali sana lakini napima uwezekano wa hawa viongozi wangu kushinda..Hivyo sii lazima umpendaye awe chaguo lako bali nani ataweza kuleta ushindi.
Unapoambiwa usipoziba yfa utajenga Ukuta haina maana upake rangi mpya! CDM bado tutakerwa na maelezo ta waraka huo kama hautakuja na majibu... Na tudsubiri report ya mkaguzi wa mahesabu ya serikali utaona jinsi atakavyo tumaliza maana tumempa njia rahisi kabisa. Subirini mtakuja nambia..
 
Kama walikuwa na mkakati wote huu, sii waanzishe chama chao
 

Alichofanya zitto ni makosa kugawanya chama kinyume na taratibu za CDM, na pia kufanya slandering ambayo ni makosa makubwa duniani kote na ktk maisha ya kawaida.Sasa kwanini wewe uone kuwa inaweza funikwa na michezo ya ushindani?

Wala hakuna haja ya kuifanya kuwa ni politicala strategy.Na alichostahili ni adhabua ambayo kaipata.Zitto naichukia tabia yake ya kutwist makosa kuliko yakubali.Ndio maana kajiwekea ukuta kila mahali,sasa anakwenda ktk njia isiyotoboza.
 
Mkuu SMU,
Nakubaliana na wewe kwamba labda kulikuwa na tangible evidence zaidi ya waraka tajwa! Lakini kubwa kuliko yote, nakubaliana na wewe kwa 100% kutoka hapo kwenye RED....binafsi sijaona uovu wa kutisha kwenye waraka husika ingawaje kwa waathirika kama Mbowe ana kila sababu za kuuogopa waraka huo kv unazungumzia yeye kuondoka madarakani. Kwangu mimi waraka wa ushindi is all about kubadilisha uongozi uliopo kwa kutumia njia halali na mikakati ya kisayansi; sijaona baya la kutisha katika mkakati ule hata kama waathirika(uongozi) wanataka kulazimisha kwamba mkakati una mpango wa kuwagawa watu kwa udini. Haya yaliyofanyika CHADEMA hivi sasa ni yaleyale ambayo yalitaka kumkuta Kikwete kule Dodoma; tusijidanganye kwamba JK na mashushu wake wote wale waliomzunguka bado hakufahamu ni nani walikuwa kwenye mpango wa kumpiga chini kama mwenyekiti wa CCM.

Katika hili sitaki kuwa mnafiki! Haya yamefikiwa kwa sababu moja kubwa kwamba Mbowe hayupo tayari kukabiliana na changamoto. CCM na ukuu kuu(uchakavu)wao wote lakini bado ni mfano wa kuigwa katika kukabiliana na changamoto za aina mbalimbali ndani ya chama. CCM pamoja na uchakavu wake wote lakini bado ni mfano wa kuigwa katika suala zima la uhuru wa maoni miongoni mwa wanachama wake. Inasikitisha kuona chama cha kileo chenye vijana wa kileo huku wengi wao wakiwa ni wasomi wao ndio wabakaji wakubwa wa uhuru wa kujieleza huku ubakwaji huo wa uhuru wa kujieleza ukiwa unavikwa koti la "matumizi ya vikao halali vya chama" huku wengine wakihubiri kwamba eti makamanda wa vita huwa hawabadilishwi wakati wa vita!
 
Last edited by a moderator:
Reactions: SMU
Mkuu nimeusoma waraka huu zaidi ya mara tano sioni hicho walichomtia hatiani
Huu ni mkakati upo genuine kabisa, Lissu ameniangusha sana
Inawezekana kweli Zitto akawa ni muhaini wa chama lakini si kwa huu waraka

You are right. Waraka huu unaweza usiwe na tatizo (on the face value). Tatizo ni kwamba CCM wanataka/wangependa ZZK awe Mwenyekiti wa CDM. Hili ndio tatizo. Kwa maoni yangu, tatizo hili ni kubwa. And it seems Kitila et al and ZZK were not on the same page. Inaonekana tayari ZZK alishawazunguka kina Kitila na kuomba back up ya CCM katika kutekeleza mkakati ulioainishwa kwenye waraka huu. Sina hakika kama Kitila et al alijua CCM wanahusika katika utekelezaji wa waraka huu.
 

Ni km kusema muuaji aliua kisayansi sana na hivyo asifanywe kitu.Kinamhukumu ni mauaji na si jinsi alivyotekeleza hayo mauaji.
 
Reactions: SMU
haya hayana budi kutokea ili watu wapate kujifunza
 
Waraka tu umewqtishia hadi kufukuzana sasa anhuko kuu la kishindwa uchaguzi 2015 chama kwishneyy
 
sijaona ubaya wa huu waraka!!!!! kama tuhuma ni za uongo si wangekanusha? kwani vifaa visemwavyo kununuliwa si vipo ushahidi wa mnunuzi hauko wazi? bado kuna maswali mengi kuhusu nguvu ya chadema na uwezo na muonekano wa ofisi yake ni KICHEFUCHEFU, hili nalo je?!!! tusiwe wepesi wa kuficha madehambi yetu kwa mtindo utakaogharimu wengi, kama Dr slaa amekuwa kwa mtindo huu shame on you!! yooote uliyoyafanya unahadaika kidogo kwa kiwango hiki,? pole Tanzania.<br><br>
 
Kama walikuwa na nia njema makakati huo wa ushindi walikuwa wanafanya kampeini kwa uchaguzi uliotangazwa lini kwenye Chama? Kwa nini waraka huo uende sambasamba na kauli ya uongo na ya shinikizo ya Nape na baadhi ya Viongozi na wanachama wa CCM kuwa CHADEMA HAIJAFANYA UCHAGUZI KWA MIAKA 12 ??!! Hapa ni mashaka mkubwa.
 
Ndugu wana JF,pamoja na kunaswa kwa ule waraka uliokuwa umeandaliwa kwa lengo la kukigawa na kukipasua Chama cha CHADEMA, jana Mjumbe wa Mkutano mkuu Kitila Mkumbo alikiri kuuandaa yeye na wenzake,lakini hakumtaja mtu mmoja anaetuhumiwa kushiriki nae ktk kuandaa mkakati huo aliejulikana kwa jina la MM2.

Habari za uhakika ni kwamba mtu huyo au Msaliti huyo anaedaiwa kutumia jina la MM2 na anaefanya kazi makao makuu ya CHADEMA na ambae inadaiwa ndie amekuwa akivujisha siri za chama sio Mwingine bali ni MWITA MWAIKABE WAITARA!

Habari hizi ni za kweli na muda sio mrefu ataanikwa wazi ili kumaliza habari za tetesi!

Ikumbukwe kwamba ndg Waitara anategemea kugombea ubunge jimbo la Tarime kwa mara ya 2 baada ya kushindwa ktk uchaguzi wa 2010!

Nawasilisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…