Waraka uliowaondoa Zitto Kabwe na Kitila Mkumbo CHADEMA huu hapa

Waraka uliowaondoa Zitto Kabwe na Kitila Mkumbo CHADEMA huu hapa

vikwazo dhidi ya tunayemtaka:
sisi wenyewe tunaoandaa mkakati huu hatuna uhakika kama tunayemtaka yuko tayari na yuko serious na business hii, na kwa hiyo huenda tusifanye kwa nguvu zetu zote ikiwa hatutapata nafasi mapema ya kukutana na mhusika na akatuhakikishia kwamba yuko serious.

utayari wa mhusika mkuu kutekeleza yale tunayokubaliana. Inapotokea baada ya kukubaliana sisi na yeye akapata ushauri tofauti na ukauona uko more genuine, basi tuwasiliane kwamba nimeshawishika kufanya hivi badala ya vile tulivyokubaliana kwa sababu hizi ama zile. Hii haitatukatisha tamaa tofauti na kama tutakuwa tunapanga hivi halafu yeye anafanya vile bila maelezo yoyote
kitendo cha mkuu aliyepo kung'ang'ania kuendelea nayo ni kikwazo kwa kuwa baada ya kuwa madarakani kwa miaka yote hiyo lazima amejipatia watu wanaomhusudu ama kumpenda ama kumkubali na kuwepo wengine wanaoogopa tu kwamba mkuu aliyepo akitoka taasisi itakufa hata kama hawana sababu yoyote.

kwa mujibu wa waraka huu kumbe zitto mwenyewe siyo key player katika kuuandaa mkakati huu, bali kuna watu wanatamani awe camp yao, sasa iweje zitto aadhibiwe wakati siyo driving force katika huu mkakati?. Uonevu tu.
 
Wanajamii

Naomba niseme Kwamba kama kinachoendelea ndani ya CDM ni hiki kilichofikishwa hapa. Basi chama hiki hakuna mwendo wala mwisho mzuri.

Matatizo ya mbowe na slaa yaliyoainishwa kwenye waraka huu ni ya kweli na ya msingi sana. Hata mm nakubaliana nayo sana na ninayajua yote kabla ya kusoma hapa na kama mdau wa karibu wa chama yamekua yakinitatiza sana na kwa muda mrefu sana.

Uamuzi wa hawa member wanne mm nauona kama ni uamuzi au mpango sahihi kabisa na usio na madhara yoyote Hasi kwenye chama. Tatizo ni Kwamba una madhara hasi kwa wakuu wa chama waliotajwa. Kwa hiyo vita hii na uamuzi huu wa kuwasimamisha Hawa member wane ni vita ya kuchumia tumbo kwa Hawa mabeana Wawili wanaiitwa mkuu na Mtendaji mkuu. Kwa mantiki hiyo basi CDM Sasa iache kujinadi Kwamba inapinga ufisadi wakati ukweli si huo. Uroho wa madaraka wakati uwezo wa uwajibikaji ni Mdogo ni tatizo kubwa sana kwa chama hiki kwa Sasa. Na ndoto ya kuiona ikulu ya magogoni Sasa ni ndoto ya alinacha kwa chadema.

Hivi ni nani asiyejua Kwamba operesheni zote za chama zinakufa kibudu, na tatizo ni mbowe. At the end malengo hayafikiwi hata kidogo, kama kuna mtu atlishiriki katika uzinduzi wa kanda na M4C anafahmu filaments operesheni hiyo ilivyokuwa nzuri lakini imekufa kwa sababu ya mbowe.

Lakini pia mm binafsi sijaona Kama kuna matusi yoyote kwa viongozi hao wakuu wa chama kwenye waraka huu. Hizo ni propaganda za kipuuzi sana. Na dhahiri shahiri Kwamba mkakati huu ulishanaswa mapema mno na ndio maana mwigamba alifanyiwa umafia ule though mkakati huu Unaonekana kama umeandaliwa baada ya tukio lile la mwigamba.
Nimegundua pia kutokana na aina ya ushiriki wa tundu lisu kwenye hili Kwamba na yy pia amesimamia upande wa mbowe na slaa kwa hilo namuona kama si mwanamageuzi wa kweli ndani chama na kwa Tanzania nzima. Nataka nitumie fursa hii kumkumbusha Kwamba wakati Chacha wangwe yanaanza kumkuta kama haya zitto nae akikuwa akifurahia upande wa mbowe, Sasa yamemkuta. Kwa mantiki hiyo lisu akae akijua Kwamba siku na yy atakapotaka kufanya au kusupport mabadiliko yoyote positive ndani ya chama dhidi ya hawa jamaa kaburi la kisiasa ndani ya chama linamsubiria.

Mwisho kabisa niwape pole Hawa member watatu wanaotarajiwa kutokuwa CDM member ndani ya wiki Kwamba niko nao pamoja kimsimamo kwa lile walilotaka kulifanya. Ikiwekekana watumie Namna mbadala Kama itakuwepo kueffect these positive changes.

Thanks
 
Hakuna kamati maalum inayowathibitisha maaintelijensia hao bali wakuu wenyewe wanawachukua wanaowataka. Ni katika mfumo huu wa kipuuzi mida eight amekuwa akitumika vibaya kwa kumshambulia mtendaji mkuu msaidizi hadharani kwa kutumia mitandao ya kijamii na wakuu wanafurahia na kumlipa pesa.

amakweli huyu BenSaanane anawatesa wasaliti, huyu dogo ni JamesBond007 wa siasa za Kitanzania
 
Dr. Slaa mnafiki sana. Yeye ndio mchochezi wa vurugu zote hizi lakini leo anajifanya kamuachia Tundu Lissu ndio atoe taarifa kwa waandishi.

Dr. Slaa ni mwanasiasa mlaghai...

Wewe endelea kulalama lakini mizizi ya CCM ndani ya Chadema imekatwa ingawaje bado mmoja lakini huyo naye atajulikana muda si mrefu. Na kazi yote hii ilikuwa inafanyika kwa kutumia bajeti ya pesa za walipa kodi zilizokuwa zinatumwa ujerumani na ikulu na baadae kumrudia Zitto. No wonder Wassira alikuwa anatamba kwamba CDM itakufa kabla ya 2015. Wakajipange upya.

Tiba
 
Dr. Slaa mnafiki sana. Yeye ndio mchochezi wa vurugu zote hizi lakini leo anajifanya kamuachia Tundu Lissu ndio atoe taarifa kwa waandishi.

Dr. Slaa ni mwanasiasa mlaghai...
Hasira za nini? si mlidai Zito hafukuziki - sasa CDM inawapa jembe lenu si mshangilie lije kwenu mlipe uwenyekiti? au anafaa uenyekiti wa CHADEMA tu, hahahahaaaaa, leo imekuwa siku ya raha kweli!
 
Haihitaji akili ya ziada kutambua kuwa haya ni mapishi yatokanayo na ile michezo ya kibabababa na kimamamama. Ni mepesi mno kuyaamini. Kama kamati kuu imetoa maamuzi kwa kuongozwa na huu waraka basi hakuna kamati kuu ila kuna kikundi cha watu wasiojitambua. Siamini kama Tundu Lisu umejiridhisha na huu waraka labda uniambia mlikuwa mnatafuta sababu of which huu waraka hautoshi kuwa sababu ya kufanya maamuzi yaliyofanyika. Sidhani kama huu ni ushahidi uliojitosheleza. Labda kama kunaviambatanisho vya huu waraka.

Vile vile Sijaona matusi aliyoyasema Lisu. Labda kama mimi sijui matusi ni nini. Pia matatizo ya kiuongozi yalitajwa, kama hayana ukweli, yangepuuzwa. Lakini kama yanaukweli yangefanyiwa kazi ili kuyarekebisha.
 
Hii inanikumbusha NCCR Mageuzi kwenye mkutano wao maarufu wa Raskazoni Tanga miaka ileeeeee mwenyekiti wao akiwa Augustine Lyatonga Mrema. Walitupiana ngumi na kurushiana viti na baada ya hapo haijawahi kuwa chama chenye nguvu na maarufu tena mpaka leo. Tusubiri tuone CHADEMA kitafika wapi na huu utaratibu wao mpya wa kutafunana wao kwa wao naona hata zile kampeni za M4C zimefifia siku hizi kinatamba chama nambari wani tu.
 
Wewe endelea kulalama lakini mizizi ya CCM ndani ya Chadema imekatwa ingawaje bado mmoja lakini huyo naye atajulikana muda si mrefu. Na kazi yote hii ilikuwa inafanyika kwa kutumia bajeti ya pesa za walipa kodi zilizokuwa zinatumwa ujerumani na ikulu na baadae kumrudia Zitto. No wonder Wassira alikuwa anatamba kwamba CDM itakufa kabla ya 2015. Wakajipange upya.

Tiba
labda anaweza akawa yule aliyetangaza kujuzulu unaibu mwenyekiti mda mchache uliopita
 
Kawafuate hawa watu wako Ma MM
Hii ndiyo maana Godbless Lema anataka kuwatoa roho hata ningekuwa mimi ningepiga mtu tofali, watu wamekufa, watu wamejeruiwa, watu wamefungwa watu wamepigwa virungu na mabomu kumbe kuna viazi vinapanga mbinu zao kutugawa Watanzania? hatutaki hatutaki
Kafie mbali na wewe allydou, kafe nao unaoona wanakufa
Wanajamii

Naomba niseme Kwamba kama kinachoendelea ndani ya CDM ni hiki kilichofikishwa hapa. Basi chama hiki hakuna mwendo wala mwisho mzuri.

Matatizo ya mbowe na slaa yaliyoainishwa kwenye waraka huu ni ya kweli na ya msingi sana. Hata mm nakubaliana nayo sana na ninayajua yote kabla ya kusoma hapa na kama mdau wa karibu wa chama yamekua yakinitatiza sana na kwa muda mrefu sana.

Uamuzi wa hawa member wanne mm nauona kama ni uamuzi au mpango sahihi kabisa na usio na madhara yoyote Hasi kwenye chama. Tatizo ni Kwamba una madhara hasi kwa wakuu wa chama waliotajwa. Kwa hiyo vita hii na uamuzi huu wa kuwasimamisha Hawa member wane ni vita ya kuchumia tumbo kwa Hawa mabeana Wawili wanaiitwa mkuu na Mtendaji mkuu. Kwa mantiki hiyo basi CDM Sasa iache kujinadi Kwamba inapinga ufisadi wakati ukweli si huo. Uroho wa madaraka wakati uwezo wa uwajibikaji ni Mdogo ni tatizo kubwa sana kwa chama hiki kwa Sasa. Na ndoto ya kuiona ikulu ya magogoni Sasa ni ndoto ya alinacha kwa chadema.

Hivi ni nani asiyejua Kwamba operesheni zote za chama zinakufa kibudu, na tatizo ni mbowe. At the end malengo hayafikiwi hata kidogo, kama kuna mtu atlishiriki katika uzinduzi wa kanda na M4C anafahmu filaments operesheni hiyo ilivyokuwa nzuri lakini imekufa kwa sababu ya mbowe.

Lakini pia mm binafsi sijaona Kama kuna matusi yoyote kwa viongozi hao wakuu wa chama kwenye waraka huu. Hizo ni propaganda za kipuuzi sana. Na dhahiri shahiri Kwamba mkakati huu ulishanaswa mapema mno na ndio maana mwigamba alifanyiwa umafia ule though mkakati huu Unaonekana kama umeandaliwa baada ya tukio lile la mwigamba.
Nimegundua pia kutokana na aina ya ushiriki wa tundu lisu kwenye hili Kwamba na yy pia amesimamia upande wa mbowe na slaa kwa hilo namuona kama si mwanamageuzi wa kweli ndani chama na kwa Tanzania nzima. Nataka nitumie fursa hii kumkumbusha Kwamba wakati Chacha wangwe yanaanza kumkuta kama haya zitto nae akikuwa akifurahia upande wa mbowe, Sasa yamemkuta. Kwa mantiki hiyo lisu akae akijua Kwamba siku na yy atakapotaka kufanya au kusupport mabadiliko yoyote positive ndani ya chama dhidi ya hawa jamaa kaburi la kisiasa ndani ya chama linamsubiria.

Mwisho kabisa niwape pole Hawa member watatu wanaotarajiwa kutokuwa CDM member ndani ya wiki Kwamba niko nao pamoja kimsimamo kwa lile walilotaka kulifanya. Ikiwekekana watumie Namna mbadala Kama itakuwepo kueffect these positive changes.

Thanks
 
Haihitaji akili ya ziada kutambua kuwa haya ni mapishi yatokanayo na ile michezo ya kibabababa na kimamamama. Ni mepesi mno kuyaamini. Kama kamati kuu imetoa maamuzi kwa kuongozwa na huu waraka basi hakuna kamati kuu ila kuna kikundi cha watu wasiojitambua. Siamini kama Tundu Lisu umejiridhisha na huu waraka labda uniambia mlikuwa mnatafuta sababu of which huu waraka hautoshi kuwa sababu ya kufanya maamuzi yaliyofanyika

waraka umekamatwa kwenye laptop ya mwigamba na amekiri hili tatizo lliko wapi? Kitila na zitto waliitwa wakakubali na kuomba kujiuzulu nyazifa zao, tatizo liko wapi?
 
Back
Top Bottom