Waraka uliowaondoa Zitto Kabwe na Kitila Mkumbo CHADEMA huu hapa

Waraka uliowaondoa Zitto Kabwe na Kitila Mkumbo CHADEMA huu hapa

Wakimaliza kufukuzana watupe ripoti waliyotuahidi ya kuchakachuliwa matokeo ya uraisi mwaka 2005 na mkanda wa video ya mauaji ya Arusha.
 
Hii inanikumbusha NCCR Mageuzi kwenye mkutano wao maarufu wa Raskazoni Tanga miaka ileeeeee mwenyekiti wao akiwa Augustine Lyatonga Mrema. Walitupiana ngumi na kurushiana viti na baada ya hapo haijawahi kuwa chama chenye nguvu na maarufu tena mpaka leo. Tusubiri tuone CHADEMA kitafika wapi na huu utaratibu wao mpya wa kutafunana wao kwa wao naona hata zile kampeni za M4C zimefifia siku hizi kinatamba chama nambari wani tu.
Waache vinyozi wajinyoe;wapi mwalimu wangu Prof Baregu jamani??!!!
 
dah inasikitisha sana, nafikiri ile laptop,ya mwigamba ndo imeleta yote haya, kweli Mungu hamtupi mja wake
....Mkuu mi nilishasema watu wanamuona Lema kichaa lakini yule jamaa ana akili kupita PhD za akina Kitila. watu walitaka amuombe Mwigamba "...tafadhali kamanda tunaomba utuletee laptop yako tuikague kwenye kikao kijacho cha kamati kuu"
kuna mahali kanuni na ustaarab haulipi!
 
Sentensi na paragraph yako ya kwanza inasema yote juu ya uwezo wa mbowe, kuja kuleta fitina zako za kubuni bila kuangalia mafanikio kwenye para 1 ni uzambiki tafuta wa kumdanganya sio WTz ambao wako macho ndo maana wakajiunga na CDM kupigania uchumi huru na maendeleo. Kutoka wabunge 5, hadi 6 hadi 48 hata baba yako asingeweza kutufikisha hapo kwa kasi aliyonayo Mbowe na Slaa. TUKO NYUMA YENU.
 
Kusoma hii kitu wakati black lebel imejaa kichwani ni impossible. .. nitarudi kesho...
 
Maamuzi ya Kikao ndo hivyo tena, na dalili zote zilijulikana! Kilichobaki ni kuangalia kama maamuzi haya yana impact ya kuelekea 2015 na kushinda kwa kishindo! Only time will tell , manake hapa kila mtu anasema lake!
 
Nimeusoma na kuuelewa....binafsi naona kuna ukweli wa hali ya juu kuliko ubaya wa huo waraka.....kwa anayejitahidi kufikiri nje ya boxi atagundua ukweli huu. Pole zzk vumilia na endapo utavuliwa uanachama subiri kwenye ugombea binafsi..tupo tunaokuunga mkono, waachie taasisi yao inayomilikiwa na mkuu mwenyekiti. Naamin sasa tutaja sikia atakayeitwa msaliti baada ya chacha, wewe, mkumbo kuondoka. Siamini huyo msaliti atakayefuata kama atatokea kaskazini. Cdm imekuwa na demokrasia inayominya uhuru, isiyotaka kubadilisha madaraka kwa wengine, imekuwa ya zidumu fikra za mwenyekiti...hahahaaaa sasa mwenyekiti ana tofauti gani na museveni wa uganda? Think big
 
kwanza na-declare interest yangu. mimi ni mmoja wa wengi wetu ambao ni "chama-less" tuliojichokea na ukiritimba wa CCM, na hivyo tumejikuta tukiitegemea sana Chadema kama ndiye mbadala.

pia nikiri kabisa kuwa mimi binafsi siuoni kabisa mkono wa CCM kwenye waraka (or rather mpango) huu. it looks to me like a document that has been worked out by a genetically pure Chadema germ.

hata hivyo ninaelewa na kukubaliana na ukweli kwamba jambo lolote, hata likiwa ni zuri kwa kiasi gani, likifanywa kwa kificho lazima litapelekea mtikisiko kwa community husika.
hiki ndicho kilichotokea kwa Chadema.....i.e watuhumiwa wenye nia njema kabisa na taasisi yao wamefanya mambo clandestinely lakini kwa bahati nzuri/mbaya wamekuja kugundulika.

kwa mtizamo wangu, huu waraka una maudhui mazuri sana lakini una mapungufu makubwa ya kimkakati (tactical deficiency) kwa waandaji wake. waandaji hao wanaonekana kuelewa sana walichotaka kukifanya lakini hawakuwa smart...they goofed it big time (and this am particularly addressing to my good friend Dr Mkumbo, going forward).

nikirudi kwa uongozi wa Chadema, mtizamo wangu ni kuwa maamuzi yao dhidi ya watuhumiwa yamekuwa equally poor or worse. huwezi kuchukua maamuzi waliyochukua Chadema with general elections beckoning only 2 years away halafu utegemee eti kushinda uchaguzi huo. itakuwa ni vigumu sana au pengine impossible kabisa. hii inatukatisha tamaa sana - tena sana tu - sisi tunaowategemea.

kuna positives nyingi kwenye waraka huu ambazo uongozi wa Chadema ungeweza kuzichota na kuzifanyia kazi kwa ajili ya kukipeleka chama mbele. daima tukumbuke kuwa, kwa mfano, kwenye football match spectators huwa wanayaona vizuri zaidi makosa ya wachezaji walioko ndani ya pitch kuliko wachezaji wenyewe wanaocheza. hawa watuhumiwa ni kama spectators na ninyi viongozi ndiyo wachezaji - you should (or rather you could) have used approach mbadala anuai za kuwawajibisha watuhumiwa bila ya ku-create drama hii tunaishuhudia leo.
 
CDM wamejifunza kutoka CCM khs makundi ya kimkakati ktk Chaguzi.
Je, baada Chaguzi kwisha hatma ya hayo makundi ni nn?
Chairman wao, Viongozi wao wamekiri CCM kupasuka, ATHARI iliyojitokeza kutokana na hayo makundi.
Baadae CCM, walikuja na mambo mengi, Vua Gamba.., Mshikamano ktk Chama, etc
Last tym tulimsikia Chairman akizungumzia rushwa ktk Chama chao, Makundi etc.
Bila ya Dola, CCM kingekuwa wapi leo....?
 
Dr. Slaa mnafiki sana. Yeye ndio mchochezi wa vurugu zote hizi lakini leo anajifanya kamuachia Tundu Lissu ndio atoe taarifa kwa waandishi.

Dr. Slaa ni mwanasiasa mlaghai...

buku7@work
 
njaa mbaya sasa kama mtu anachangiwa million 2 ili aendeshe maisha akipewa 40 nini kitatokea, waoneeni huruma tu
 
Dr. Slaa mnafiki sana. Yeye ndio mchochezi wa vurugu zote hizi lakini leo anajifanya kamuachia Tundu Lissu ndio atoe taarifa kwa waandishi.

Dr. Slaa ni mwanasiasa mlaghai...

...we nae mkubwa mzima unakuja na shombo jukwaani,asa dr anaingiaje kwenye maamuzi ya kikao na directions za mwenyekiti. We sema alichokufanya dr. bado kinakutesa tu sio kuropoka ovyo...
 
Dr. Slaa mnafiki sana. Yeye ndio mchochezi wa vurugu zote hizi lakini leo anajifanya kamuachia Tundu Lissu ndio atoe taarifa kwa waandishi.

Dr. Slaa ni mwanasiasa mlaghai...
Mbona mnao lalamika ni nyinyi magamba tu minafikiri mlipaswa kufurahia cdm kumegua au kirusi chenu kimekuwa scaned na kaspesky antivirus mtasema sana gamba wewe.
 
Sioni shida ya huo mkakati, padri wa canonical laws na owner wa bills, jirekebisheni. Kitila sio mtu wa kuachwa msiwavue uanachama
 
Back
Top Bottom