Wakati Tundu akiongea na wanahabari sina shaka kabisa kwamba waraka huu ndio aliouzungumzia. Kwa jinsi vile hukumu zilivyotolewa, sina shaka kabisa kwamba hukumu hizo zimetokana na waraka huu! Hata hivyo, pamoja na kwamba nimesoma waraka mzima, bado sijaona ni namna gani unaweza kumhukumu
Zitto kupitia waraka huu. Kimsingi, baada ya waraka kuzungumzia udhaifu wa uongozu uliopo hususani Mwenyekiti, waandaaji wa mkakati huo wameona njia muafaka ni kuandaa mkakati utakaofanikisha kumuondoa Mwenyekiti aliyopo na kuingizwa yule anayeonekana kufaa(MM-Zitto Kabwe) Baada ya wanamkakati kufanya SWOT Analysis kuhusu MM (Zitto), wakabaini moja ya THREAT ni kwamba:
SWOT ANALYSIS:
Vikwazo dhidi ya tunayemtaka:
Sisi wenyewe tunaoandaa mkakati huu hatuna uhakika kama tunayemtaka yuko tayari na yuko serious na business hii, na kwa hiyo huenda tusifanye kwa nguvu zetu zote ikiwa hatutapata nafasi mapema ya kukutana na mhusika na akatuhakikishia kwamba yuko serious.
Utayari wa mhusika mkuu kutekeleza yale tunayokubaliana. Inapotokea baada ya kukubaliana sisi na yeye akapata ushauri tofauti na ukauona uko more genuine, basi tuwasiliane kwamba nimeshawishika kufanya hivi badala ya vile tulivyokubaliana kwa sababu hizi ama zile. Hii haitatukatisha tamaa tofauti na kama tutakuwa tunapanga hivi halafu yeye anafanya vile bila maelezo yoyote
Kutokana na maelezo hayo hapo juu, ikiwa unataka kuhukumu kupitia Waraka wa kumchafua Mwenyekiti, utagundua kwamba wakati haya yanafanyika Zitto alikuwa bado hajashirikishwa. Na katika kuthibitisha hilo, wanamkakati hawa hapa:
MTANDAO WA USHINDI:
Mtandao wa ushindi utakuwa kama ifuatavyo. Kwenye ngazi ya kitaifa tutakuwa na kamati yenye members watatu tu. M1 ndiye atakayekuwa anawasiliana na tunayemtaka ambaye ataitwa MM (Mhusika Mkuu). Tumepanga kwamba kusiwe na mawasiliano mengi kati ya kamati na mhusika mkuu kuepuka tracking ya wapinzani wetu. M1 ni mtu wa karibu na MM kwa hiyo mawasiliano yao hayataweza kutiliwa shaka na mtu yeyote hata wangewasiliana mara nyingi kiasi gani. Hata hivyo, linapokuja suala la mkakati huu tunasihi mawasiliano yawe kwa kuonana uso kwa uso ama kwa simu na si sms.
Hapo panathibitisha wazi kwamba MM (Zitto Kabwe) bado alikuwa hayupo kundini na kumbe tu kulikuwa na mkakati wa kumwingiza kupitia M1(
Dr. Kitila Mkumbo) ambae ametajwa kwamba ni mtu wake wa karibu. Je, M1 alishafanikiwa kum-recruit MM? Waraka huu hausemi hivyo, kwa hiyo bila shaka njia pekee ya kufahamu kwamba M1(Dr. Kitila Mkumbo) alishamfikia MM(Zitto Kabwe) ni kuangalia viashiria fulani fulani na hapo ndipo mtu unaweza kupata picha kwamba bila shaka sasa ni wamoja! Ukiusoma Waraka wa Mkakati, sehemu moja ya waraka huo inaweza kutoa viashiria tunavyotaka; hivi hapa chini:
Kuhusu mwenendo wa MM kuanzia sasa:
Ni maoni yetu pia kwamba kuanzia sasa MM aenende katika mwenendo ambao utarahisisha ushindi. Mfano tunapendekeza afanye yafuatayo kuanzia sasa:
Apunguze ukaribu na viongozi wa serikali na wa chama tawala na awe crical zaidi na utendaji wa serikali nje na ndani ya bunge.
Je, Zitto Kabwe amepunguza ukaribu wake na watawala pamoja na wana-CCM kiasi cha kutushawishi kwamba M1 alishamfikia na akafikika na kwamba kazi sasa inaanza kwa vitendo!
Ashiriki kikamilifu katika shughuli za taasisi yetu zikiwamo vikao vyote vinavyomhusu, operesheni mbalimbali, chaguzi ndogo, nk.
Je, hivi sasa Zitto anashirik shughuli za CHADEMA zikiwemo vikao vyote vinavyomhusu ili turidhike kwamba M1 alimfkia MM na sasa ndo wapo kwenye implementation phase.
Aendelee kushusha nondo ndani ya chombo chetu cha uwakilishi na kuendelea kuwa juu ya wawakilishi wengine katika hoja mbalimbali zenye maslahi ya kitaifa.
Je, MM anashusha nondo bungeni ili tujiridhishe kwamba alishafikiwa na M1? Mbona sikumuona akimwaga povu kwenye issue ya Operation Tokomeza? Mbona sikumsikai akimwaga nondo kwenye issue za mabadiliko ya katiba?
Ajitahidi kudhibiti jazba hata pale anapokuwa amebambikiziwa tuhuma nzito namna gani. Atulie, ashauriane na wazee ili kuona namna nzuri ya kujibu tuhuma zinazomkera. Tukumbuke kwamba wakati mwingine kukaa kimya ni jibu zuri zaidi kuliko hoja nzito.
Je, Zitto Kabwe ameanza kufanyia kazi kiashiria hicho hapo juu ili tushawishike kwamba alishafikiwa? Je, ameanza kukaa kimya hata baada ya kurushiwa kombora? Je, kule kumlima barua hivi majuzi Dr. Slaa tunaweza kuita ndo kukaa kimya? Je, si ni hivi majuzi tu alipoingia kwenye malumbano na Lema?
Sambamba na iv hapo juu, adhibiti sana emotion ili kuhakikisha kila kitu kinachofanywa ama kuzungumzwa kinachomgusa asikimbilie kuongea na vyombo vya habari ama kwenye mitandao ya kijamii bali afuate kile tulichokizungumza kwenye kipengele cha iv hapo juu.
Je, Zitto Kabwe ameshaanza ku-contro emotion zake? je, ameacha kukimbilia kuongea na Medias hadi tushawishike kwamba alishafikiwa na M1 na sasa anatekeleza maazimio? Hivi lile sakata la Zitto kumlima barua Dr. Slaa lilifahamika vipi? Ilikuwaje hadi magazeti yakaandika kama si Zitto aliongea na Media?
Hata hivyo, ni muhimu kukumbushana kwamba wenzetu hawatanyamaza kwa sababu eti sisi tumeacha kuwashambulia kwenye mitandao ya kijamii. Lazima wataendelea! Wataendelea kumchafua MM kwa kupitia wapuuzi kama yule kichaa wa ars na kundi lake. Nini tutakuwa tunakifanya sasa? Tutahakikisha tuko busy kupost mambo mema na mazuri yatakayokuwa yakifanywa na MM kila wakati na kuzidi kusambaza sifa zake njema kila inapotokea nafasi.
Je, mambo mema ya Zitto yameshaanza kuwa posted humu ili tufahamu kwamba MM alifikiwa na akafikika na sasa ametoa rukhsa ya kupambwa kwa maua na mapambio?! Mbona mie nimeona moja tu? Lile la kutaka "kuwataja mabilionea wa Uswis?" Ajabu aliyeleta habari hiyo ni
Mungi, ambae naamini hayupo kambi ya Zitto!! Au Mkuu Mungi unatuzuga tu hapa jamvini na labda wewe ndie M2 na ukaleta uzi wa Mabilioni ya Uswisi ili kumpaka mafuta MM? Lakini wewe haupo HQ bhana ambako ndiko aliko M2; sasa mbona hayo mazuri na sifa zilizotukuka za Zitto hazijaanzakumwagwa ili tushawishike kwamba "kazi imeanza?"
Kuhusu kamati ya kitaifa (hususan M2 & M3):
Tulikubaliana kwa kauli moja kwamba katika kutekeleza mkakati huu tunahitaji members hawa wawe wametulia kimaisha. Inakuwa vigumu kwa mfano kumtaka member aende mahali fulani kwa makusudi ya mkakati huu wakati hajui familia yake nyumbani anaiacha inakula nini. Tuliona kwamba M3 tayari hana kazi kwa sasa tena kwa kufanyiziwa na wakuu waliopo.
Alaah! Kumbe huu mkakati ni wa juzi juzi tu hapa baada ya kuwa M3 (Samsoni Mwigamba) akiwa tayari ameshafutwa kazi!!!