Waraka uliowaondoa Zitto Kabwe na Kitila Mkumbo CHADEMA huu hapa

Waraka uliowaondoa Zitto Kabwe na Kitila Mkumbo CHADEMA huu hapa

John Heche naona upambe wako kwa Mbowe na Dr.Slaa umefanikiwa kumfanyia fitna Mwita Waitara, lakini kumbuka kuna uchaguz mkuu.
 
habari za vijana wa mbowe sio matamko ya chadema tunaomba mlielewe hilo ,pamoja na upotoshaji huo!!kwenye ule waraka kila mtu amesoma wapi uhaini umeanishwa?kugombea nafasi ya uenyekiti ndani ya chama ni uhaini?
YAMEIBULIWA MASUALA YA FEDHA MULE NDANI YA WARAKA MBONA HATU DISCUSS AU KWA SABABU TUHUMA ZINAMLENGA BOSS WAKO??
jitambue kijana acha siasa za kufuata mkumbo!!
 
Lumumba buku7 kweli hamjielewi... sisi tunaongelea WARAKA wewe unawaza uwakala , sijui wa M-pesa au nini sijui. Mnastahili pole kwa kweli.

Anawaza "uwakala" aliopewa na CCM kuhangaikia CDM. Huyu si wakala wa Ccm pale Lumumba?
Kweli akili za makalioni zina vituko!!
 
Hujaona kwa kuwa Macho yako hayaoni. Kitila Mkumbo alikiri kuwa alifanya kosa na aliomba kujiuzulu lakini hakukubaliwa na uongozi.
Wewe unapodai kuwa hujaona,kwani ungeona ungefanya nini?
Kwanini mnangangana CDM kifanye uchaguzi wa Mwenyekiti?
Niambie ni lini CCM iliwahi kufanya uchaguzi wa Mwenyekiti wa chama Taifa zaidi ya kurithishana??

Mngeanza nyie kuonyesha Demokrasia halafu ndio mkimbilie Cdm. Kuna vyama tangu vianzishwe havijawahi kufanya uchaguzi wala kubadilisha viongozi km TLP,CUF nk. Je hamvioni mnaiona tu CDM!?
CHADEMA hakiwezi kuchaguliwa viongozi na ninyi CCM. mlizoea kuuwa vyama vya upinzani kwa kuwanunua viongozi wake wakuu ila kwa CDM mmeshindwa kwa kuwa Mbowe na Dr Slaa hawana njaa ndio maana mnadhani njia ya kufanikisha malengo yenu ni kuwaondoa. Poleni sana.

Mkuu, sidhani kama matakwa ya hawa jamaa yako nje ya katiba ya chama. Kama katiba ya chama inasema mwenyekiti atachaguliwa kila baada ya miaka 5 haimaanishi kuwa wafate kama vyama vingine vinavyofanya. Katiba ndio muongozo na lazima ifatwe na kama waliiandika wenyewe kwa kukubaliana iweje mtu mmoja aje kutumia mabavu na kufanya kama chama ni chake?

Embu tafakari halafu urudi kimya kimya bila kelele. Kinyume na hapo nadhani utakuwa ni shabiki wa chama na sio hoja zilizotolewa.
 
Sijaona mahala katika waraka wa Mkumbo panapoonesha anataka kuigawa chadema. Hivi maana ya demokrasia ni kuhodhi madaraka maisha?

Hapa, si kuhodhi madaraka daima! Bali ni kutumia njia halali zilizowekwa na taasisi husika katika kushughulikia suala husika. Kinyume cha hapo ni usaliti au kujaribu kuigawa taasisi husika. Sina hakika (labda wana CDM wanielimishe) kama akina Mkumbo (Dr.) wameweka ushahidi katika waraka wao kuonesha kwamba wamejaribu kutumia njia zote za kikatiba katika kulifanikisha walilokuwa wanapigia chapuo katika waraka huo ambao kwa bahati mbaya waliukana haraka sana mara ulipovuja..
 
Sijaona mahala katika waraka wa Mkumbo panapoonesha anataka kuigawa chadema. Hivi maana ya demokrasia ni kuhodhi madaraka maisha?

Huwezi kuona kitu ambacho hutaki kukiona. Ukianzisha kikundi chako ndani ya Chama kama siyo kukigawa maana yake nini. Usituambie kuwa demokrasia unayoielewa wewe ndiyo maana ya demokrasia.
 
Mkuu umesahau na UDP ya Cheyo pamoja na DP ya Mtikila tokea nimezaliwa wote hao walikuwa ni wenyeviti wa vyama vyao lakini CDM tokea imeanza nimesikia mzee Mtei, Bob Makani na sasa Mbowe sasa ni wapi penye demokrasia?

Hawa vimnyela wanatumiwa na maccm na ss hatuwavumilii.
 
John Heche naona upambe wako kwa Mbowe na Dr.Slaa umefanikiwa kumfanyia fitna Mwita Waitara, lakini kumbuka kuna uchaguz mkuu.

Mbona unamtaja sana Kamanda Heche au kakutia kile kitu nini maana tunajua wewe nawe kwa kujipendekeza kwa watoto wa kiume hujambo!?

Halafu tuambie ni lini CCM itafanya uchaguzi wa Mwenyekiti wa Chama Taifa? Au mtaendelea tu kurithishana?
 
habari za vijana wa mbowe sio matamko ya chadema tunaomba mlielewe hilo ,pamoja na upotoshaji huo!!kwenye ule waraka kila mtu amesoma wapi uhaini umeanishwa?kugombea nafasi ya uenyekiti ndani ya chama ni uhaini?
YAMEIBULIWA MASUALA YA FEDHA MULE NDANI YA WARAKA MBONA HATU DISCUSS AU KWA SABABU TUHUMA ZINAMLENGA BOSS WAKO??
jitambue kijana acha siasa za kufuata mkumbo!!

Unaandika huku unawaza buku 7
 
Mkuu, sidhani kama matakwa ya hawa jamaa yako nje ya katiba ya chama. Kama katiba ya chama inasema mwenyekiti atachaguliwa kila baada ya miaka 5 haimaanishi kuwa wafate kama vyama vingine vinavyofanya. Katiba ndio muongozo na lazima ifatwe na kama waliiandika wenyewe kwa kukubaliana iweje mtu mmoja aje kutumia mabavu na kufanya kama chama ni chake?

Embu tafakari halafu urudi kimya kimya bila kelele. Kinyume na hapo nadhani utakuwa ni shabiki wa chama na sio hoja zilizotolewa.

Waraka una maudhui ya kumwandaa Zitto Kabwe awe mwenyekiti. Waraka haukuwa na mikakati ya kudai uchaguzi.Suala la uchaguzi kwanini hawakulipeleka kwenye vikao vya Chama? Usitufanye sisi kuwa hatuna akili
 
Sijaona mahala katika waraka wa Mkumbo panapoonesha anataka kuigawa chadema. Hivi maana ya demokrasia ni kuhodhi madaraka maisha?

we si uwe busy na chama chako ...mbona unawashwa sana na mambo yasiyokuhusu
 
Lumumba buku7 kweli hamjielewi... sisi tunaongelea WARAKA wewe unawaza uwakala , sijui wa M-pesa au nini sijui. Mnastahili pole kwa kweli.

halafu zuzu kweli linaandika kwa kujiamini wakati uwezo kichwani sifuri sijuhi hii MICCM aibu inawekaga wapi?
 
Wana bodi
Hofu imetanda kila kona juu ya muonekano wa CDM huko mbele, kuna kiza kimetanda.

1. CDM pamoja na kuwa na uongozi na wanachama wengi ila kimesahahu kwamba kina wapiga kura wengi kuliko wananchama. Sijui kama viongozi na hata mkutano mkuu umesha fanya SWOT na kujua jambo hili. yaani kujua tu kwanini wafuasi na kura zi nyingi kuliko idadi ya wananchama?

2. Waraka huu, kama unavyo someka kwa wengi ( hasa wapenda mabadiliko ya nchi, wasio wapenda chama) ulipaswa kuwekwa mezani kwenye mkutano mkuu na kujadiliwa, maana una mambo ya kukijenga chama, na hata "ku-assess leadership style" ya chama. Hii ilikuwa nafasi ya chama na vikao vyake kuujadili na kchukua yaliyo mema na kuonya au kutolea marekebisho kwa mabaya na njia ya usiri iliyotumika kuuandaa waraka, pengine kuboresha na kuwa wa kuchukua dola kabisa kwa level ya kitaifa.

3. hakuna mfutailiaji wa siasa za nchi, hasa za mtandaoni ambaye atashindwa kuamini kuwepo kwa makundi ndani ya CDM. Kuanzia wakati ule kina Shonza, Mwampamba et al wanatimuliwa utaona kuna watu walipewa adhabu tofauti. Kama haitoshi chama kina intelijensia "known" na "unknown" na kinafanya uchunguzi hata kwa viongozi wa ngazi za juu, na ripoti yake inapokelewa na baadhi tu ya viongozi. Upande mwingine kuna wanachama kama Yericko Nyerere na team yake, n.k hawa ni wanachama lakini kila mara wamekuwa wakimuandika N/katibu mkuu kwenye media tena kwa ubaya zaidi nani anawatuma, je uongozi umewahi kuwaonya? Zaidi kuna kiongozi wa ngazi ya mkoa alitoa ile iliyo itwa ripoti ya siri ya ya CDM, nini kimetokea? Watasema chama kimekanusha, lakini tulipaswa kuona zaidi ya hapo ikiwemo hatua zilizo chukuliwa dhidi yake.

4. Naomba uongozi wa CDM usiendelee kutumia njia ya kufukuza kwa kila kosa, au kwenda kwenye media kila mara hasa inapo onekana wamefanya maamuzi magumu!! Uongozi unahitaji kukomaa na kuruhusu majadiliano na uwazi, kutofautiana ni sehemu ya kujipanga. Ikumbukwe chama hiki bado kina umri mdogo, na kimekua zaidi miaka ya karibuni hivyo mawazo mapya, tabia na mwenendo wa viongozi wake bado haujaw imara, hivyo bado kina jenga misingi ni bora kuwa na uvumilivu.

Viongozi wa CDM wawe team, wasiruhusu mwanachama mmoja kumsema kiongozi mmoja kwenye mitandao, kwanini mwanachama asiwakilishe malalamiko yake kwenye vikao? maana hilo ndo kosa alilofanya Mwigamba? Je yule wa mkoa wa Kinondoni wamefanywa nini?

Kila heri, kipindi hiki ni muhimu sana kwa CDM, tena ni wakati wa kukuza na kutumia BUSARA ZAIDI, kuliko wakati mwingine, kama ni safari gari letu linapata pancha, tusimame tuzibe, haina haja ya kushusha watu kwa kusema tunapunguza uzito na tutafika, hapana tuzibe, tulianza safari pamoja tutafika wote pamoja.

Mungu ibariki CDM, Mungu ibariki Tanzania
SP
 
njano5,

siku hizi umebadilika sana .hongera sana tuendeleze mapambano dhidi ya ccm na wasaidizi wao

kaka mimi huwa sifuati maneno ya kwenye mitandao,,,,,,mimi huwa nafuata maneno au maamuzi ya chama, chama ndio kila kitu kwangu,,kwenye mtandao mtu anaweza kusema lolote lile analolitaka,,,mbona ilisemwa wewe ulitaka kumuua zitto kwa sumu,,,je,, pia ulitaka tuamini kisa tu kimesemwa kwenye mtandao??? Pia tuhuma za zitto za kwenye mtandao sikuwa na sababu ya kuziamini, tena kitendo cha chama kuwa kimya ndio ilikuwa sababu tosha ya mimi kutokuamini.

Mkakati wa mabadiliko umejadiliwa na chama na wahusika wamekiri kuuandaa kwenye kikao,,,mimi sina namna ya kupinga uamuzi wa chama juu ya hili,,,na sina sababu ya kumtetea zitto juu ya hili hata kama ndiye mwanasiasa ninayempenda. Nchi na chama kwanza,,,wanasiasa baadae.

Siku zote nasema kuwa tuamini juu ya misingi ya chama si watu,,,watu hawaaminiki na muda wowote wanaweza kuacha mapambano na kuingia ccm au kutusaliti kwa namna yoyote. Hata mimi naamini juu ya misingi ya chadema,,,zitto ndio kanifanya niingie chadema,,,sitatoka chadema hadi pale chadema itakaposaliti misingi yake,,,hata zitto akitoka chadema,,,nitaendelea kupambana NA CCM KUPITIA chadema hadi nishindwe mwenyewe. Pia sitamtetea zitto kwa makosa yaliyothibitishwa na kamati kuu, nilichokuwa napinga kitendo chenu cha kutumia mitandao,,,mimi niliona hizi ni kama siasa chafu.

Nawakubali viongozi wote wa chadema na ndio maana kila siku naomba mungu aibariki chadema na viongozi wake.
 
Hebu fikiria hii 2015
Rais mbowe(slaa atatupwa bungeni)
Waziri mkuu sugu
Mambo ya njee afande sele
Madini myika
Tiss yule mchungaji mbeya
Sheria tundu
Afya mdee
Makamo rais yule kibarashia kwenye picha ya mkutano wa kumfukuza ziti
Wizara nyengine zitakuwa chini ya rais
Mhh muungu atuepushe mbali na balaa na zahma hili
 
hujaona kwa kuwa macho yako hayaoni. Kitila mkumbo alikiri kuwa alifanya kosa na aliomba kujiuzulu lakini hakukubaliwa na uongozi.
Wewe unapodai kuwa hujaona,kwani ungeona ungefanya nini?
Kwanini mnangangana cdm kifanye uchaguzi wa mwenyekiti?
Niambie ni lini ccm iliwahi kufanya uchaguzi wa mwenyekiti wa chama taifa zaidi ya kurithishana??

Mngeanza nyie kuonyesha demokrasia halafu ndio mkimbilie cdm. Kuna vyama tangu vianzishwe havijawahi kufanya uchaguzi wala kubadilisha viongozi km tlp,cuf nk. Je hamvioni mnaiona tu cdm!?
Chadema hakiwezi kuchaguliwa viongozi na ninyi ccm. Mlizoea kuuwa vyama vya upinzani kwa kuwanunua viongozi wake wakuu ila kwa cdm mmeshindwa kwa kuwa mbowe na dr slaa hawana njaa ndio maana mnadhani njia ya kufanikisha malengo yenu ni kuwaondoa. Poleni sana.

well spoken kamanda.
 
Mkuu, sidhani kama matakwa ya hawa jamaa yako nje ya katiba ya chama. Kama katiba ya chama inasema mwenyekiti atachaguliwa kila baada ya miaka 5 haimaanishi kuwa wafate kama vyama vingine vinavyofanya. Katiba ndio muongozo na lazima ifatwe na kama waliiandika wenyewe kwa kukubaliana iweje mtu mmoja aje kutumia mabavu na kufanya kama chama ni chake?

Embu tafakari halafu urudi kimya kimya bila kelele. Kinyume na hapo nadhani utakuwa ni shabiki wa chama na sio hoja zilizotolewa.

Labda wewe ndei huelewi. Kwani Katiba ya CDM ina kipengele kisemacho mtu haruhusiwi kugombea zaidi ya mara 2. Na hata km basi katiba inasema kuwa uchaguzi ufanyike kila baada ya miaka 5 ni haki Zitto kutengeneza Kikundi ndani ya Chama!? Je huko sio ndiko tunakotafsiri kua ni kukigawa chama makundi?
Kwanini asisubiri hadi muda wa uchaguzi ufike na agombee na km akizuiwa kugombea ndipo alalamike?

Na vipi kuhusu katiba ya CCM haisemi uchaguzi uwe unafanyika kila baada ya miaka mingapi? Na km inasema je ni lini CCM iliwahi kufanya uchaguzi wa mwenyekiti wa Taifa?
Na je mbona Ccm wanarithishana kile cheo cha Mwenyekiti au Demokrasia inatakiwa tu ionekane Cdm lakini kwa wengine hapana?
 
Sijaona mahala katika waraka wa Mkumbo panapoonesha anataka kuigawa chadema. Hivi maana ya demokrasia ni kuhodhi madaraka maisha?

Upo katika huu uzi kwa msukumo wa "dini" ya Zitto Kabwe..... bhaaasi!
 
Back
Top Bottom