Waraka wa Bashir Yakub: Tundu Lissu japo unaumwa lakini umeshindwa

Waraka wa Bashir Yakub: Tundu Lissu japo unaumwa lakini umeshindwa

Mtunzi mzuri wa mashairi kutoka 196 bil - 300 Mil ni mafanikio makubwa na za tra zipo humohumo mzungu hazidiwi hesabu amka mkuu
 
Tuliwaita waizi tukawapelekea invoice ya trillion 484 leo wamekubali kulipa dola millioni 300 sawa na billioni 700. Hivi kutoka trillion 484 hadi billion 700 huu si ni ukichaa? Lisu hakukosea aliposema zile ripoti za kina prof Mruma na Ossoro ni Rubish. Yaani tunalipwa 0. Halafu tunajivuna. Mchanga uliopo bandarini vipi mbona kimya? Bado tunaendelea kupigwa sana
Mbona hawajaenda MiGA?
 
Yaan hum ndan watu wengi hawafaham business negotiation, kuna mambo ni trick, ikiwa unataka kulipwa fedha na kampun na pesa ni za makadrio, huwa kuna early invoce na net invoice...

Kilichopelekwa awali ilikuwa ni early baada ya mazungumzo ikawa net... In trade tunasema tz imewin... Kwa kuwa haikuwa na cha kupoteza, ila wao, walikuwa nacho..

Bigup presidor JPM
 
Kwani wametulipa kodi au zile tril 400? Hizi rushwa ndiyo malipo? Wasomi wengine njaa tu
Nyie si mlisema hawatalipa hata senti, na watatuburuza mahakamani, na mkadai mchanga ni Mali yao, leo hata hicho kidogo walichotoa bado mnabadili gia angani na kujifanya mlitaka hela nyingi, Wakati huo huo mlitukejeli kwa kuleta nukuu za magazeti ya nje mkisema hela tulizodai eti ni kituko, hazijawahi kudaiwa duniani, sasa zimelipwa zile mlizokadiria mnaropoka kama akina mama shughuli au kijumbe wa uswahilini aliyekula hela za mchezo za wenzake! Ovyo kabisa machadema!
 
Wewe hujitambui, kati yako na kundi lako mlio tuaminisha kwamba tutalipwa tilioni 4, leo zimekua bilioni 500.sijui kati yenu na Lisu nani mwelevu, acha umazwazwa wewe
We bado unamwamini mgonjwa!! Pamoja na tatizo lake la Akili, bado tunampa pole kwa kuongezewa tatizo la kimwili,! Naona si Habari njema kwake.
 
Yaan hum ndan watu wengi hawafaham business negotiation, kuna mambo ni trick, ikiwa unataka kulipwa fedha na kampun na pesa ni za makadrio, huwa kuna early invoce na net invoice...

Kilichopelekwa awali ilikuwa ni early baada ya mazungumzo ikawa net... In trade tunasema tz imewin... Kwa kuwa haikuwa na cha kupoteza, ila wao, walikuwa nacho..

Bigup presidor JPM
Kwakweli JPM na timu yake walitumia mbinu nzuri sana kwenye kuelekea ktk majadiliano. Rule of thumb ni kwamba lama huna pa kuanzia ni lazima utakosa pa kutokea. Trick ya kudai deni kubwa imesaidia sana kupata terms nzuri kwenye mkataba na hizo USD 300m.
Barick nao wamepata pia pa kutokea wakidai kwamba hawajalipa bali ni kuweka uaminifu tu🙂
Ukweli ni.kwamba wanalipa pesa plus wame-concede hisa 16% na faida ya mapato 50% which in a long run itatupatia hela nzuri tu hata kama jumla yake Haitafikia zile trillions, but hey....
 
Waraka wa BASHIR YAKUB.
+255784482959.

Pole sana msomi Lissu kwa kuumwa. Lakini sasa kwa taarifa za jana ni kuwa unapata nafuu na Mungu Mwenyezi awe nawe urejee.

Hata hivyo huku ulipotuacha ni umeshindwa vibaya. Wale uliosema watatushitaki na kuwalipa mabilioni sasa wao ndio wanatulipa sisi mabilioni.

Kile ulichosema kuwa ni makosa yetu ya mikataba na ulofa, wamekubali kuwa ni makosa yao na wako tayari kwa marekebisho ya "terms" vipengele vipya kwenye mikataba.

Hata zile kesi ndogondogo tulizokuwa nao katika mahakama "tribunal" mbalimbali sasa nazo wamekubali iundwe kamati ya kuzimaliza kwa mazungumzo.

Lakini kubwa kuliko yote msomi Lissu ni kuwa wamekubali mgao wa 50/50 wa faida na Tz kuwa na wawakilishi kwenye bodi ya wakurugenzi na mengine mengi yenye kutia moyo. Sijui, lakin nadhan habari hizi sio njema sana kwako.

Msomi Lissu, siku nyingine ukiambiwa wako watu wana akili kuliko wewe uwe mwepesi tu kuelewa. Ukiambiwa wako watu wanaona maili 50 zaidi yako uelewe haraka.

Hatukatai, unaweza kuwa mzungumzaji mzuri lakin sio mwenye upeo. Upeo hupimwa kwa matokeo ya matendo. Na kwa matokeo haya twaweza tu kupima nani mwenye upeo kati ya wale uliowaita wa hovyo na wewe. Pia twaweza kujua wa hovyo ni nani sasa.

Nilikushangaa sana uliposema huoni kosa la Acacia. Watu wamedanganya uzito wa madini, wamedanganya sampuli walizobeba na ushahidi upo, msomi unasema huoni kosa !!!? , Looh.

Unajua vyema kuwa hawa jamaa wangekuwa upande salama kama ulivyopiga chapuo wasingefikia makubaliano kama haya. Wangeenda kwenye tribunal za kimataifa kama ulivyowasaidia kupendekeza na wangeshinda na tungelipa mabilioni kama ulivyokuwa umetabiri.

Ulikera sana hapa :

Makontena yakazuiwa, ukasema kimkataba ni yao na yamezuiwa kimakosa.

Ripoti ya kwanza ikasomwa,ukasema ripoti hiyo ni takataka"rubbish".

Ripoti ya pili ikasomwa, ukasema hamna jipya.

Akaja bosi wa Acacia Prof. John.L.Thompton akasema watalipa, ukasema hajasema kama watatulipa na hawawezi kutulipa.

Ulidhihirisha uadui na nia ovu na ndio maana ni halali leo kusema JAPO UNAUMWA LAKINI UMESHINDWA. Haikujulikana ulitaka nini hasa.

Msomi, hawa watu hawakuwa wasafi na hili kila Mtanzania aliliona isipokuwa wewe. Kwa matokeo haya sasa twaweza kujua nani ana maamuzi ya KUKURUPUKA na kuzungumza hovyo.

Tunakutakia afya njema lakini upunguze kidogo kuropoka msomi. Watu wako makini kuliko unavyofikiria.

Zuzuuuu 1/100 tumelipwa nn?
 
What a shame to the Government..
From a claim of USD 400+ Trillion and u get only USD 300 Bil..!!
Mruma and Ossoro reports were purely Professorial Nonsense and Rubbish.
Not 300billion usd ni 300million usd ni pesa ndogo kuliko hela ya kumsajili Neimar.
 
Kwani wamelipa, Yakub, wamelipa? Eti na wewe ni msomi! Wanaokuchukua kama wakili nadhani wanaangukia pua kesi zote
Tz kuna wasomi na weledi wangapi tena wazalendo ambao hawako tayari kushirikiana na wezi kama msomi Lisu?....Nadhani sasa ni muda muafaka tujui hii serekali haipo kuleta mbwebwe kama walivyotuaminisha akina TL
 
Zuzu kabadilisha almasi na kipande cha chupa, ha ha ha asante sana Hayati baba wa Taifa.
 
Kama mliukua na akili haya yasinge tokea mwanzo, huyu mtu naona anatafuta kiki tu hadi umeweka namba za cm utafutwe, loh! Embu rudi zako kibiti siasa itakushinda.
 
Back
Top Bottom