Waraka wa Bernard Membe kwa Askofu Mwamakula: Sitishiki, sitakaa kimya na kamwe sitaabudu mtu wala miungu wengine

Waraka wa Bernard Membe kwa Askofu Mwamakula: Sitishiki, sitakaa kimya na kamwe sitaabudu mtu wala miungu wengine

"Nikuhakikishie hakuna hata chembe ya ukweli kuhusu yote hayo na ndiyo maana huoni na hutaona hatua za kisheria zikichukuliwa dhidi yangu. Labda wanichukulie hatua zingine! Nimepata vitisho mbalimbali kutoka kwenye Chama changu, makundi mbalimbali ya wachawi na Serikali vya kunifukuza, kuniloga, kunitupa Gerezani kana kwamba mimi ni mhalifu. Baba Askofu, kwa kuwa moyo wangu ni safi, na kwa kuwa sijatenda kosa lolote, SITISHIKI , SITAKAA KIMYA na KAMWE SITAABUDU MTU WALA MIUNGU WENGINE."
Huyu kenge wa mtama anabaki huru kwa sababu tu ya JPM kumuonea aibu JK,lakini isingekuwa hivyo wala asingekuwa nje.

Lakini kwa hali hii huenda makaburi yakafukuliwa kidogo.

Ni suala la muda tu.

Anyway mzee JPM wewe chapa kazi hawa wanataka kukutoa off track.

Endelea kuwapotezea ,sisi watanzania tunachokitaka ni maendeleo sio sura wala uhuru wa habari.

Sisi watanzania wengi tunataka elimu bure na bora.

Matibabu bure na hakika.

Miundombinu ya usafirshaji na huduma za maji na umeme kila kona ya nchi na kwa kiwango cha hali ya juu.

Baada ya hapo nasema wazi

#VIVA JOHN POMBE MAGUFULI.[emoji1241][emoji818] WATANZANIA TUKO NYUMA YAKO NA TEMBEA KIFUA MBELE!
 
Huyu kenge wa mtama anabaki huru kwa sababu tu ya JPM kumuonea aibu JK,lakini isingekuwa hivyo wala asingekuwa nje.

Lakini kwa hali hii huenda makaburi yakafukuliwa kidogo.

Ni suala la muda tu.

Anyway mzee JPM wewe chapa kazi hawa wanataka kukutoa off track.

Endelea kuwapotezea ,sisi watanzania tunachokitaka ni maendeleo sio sura wala uhuru wa habari.

Sisi watanzania wengi tunataka elimu bure na bora.

Matibabu bure na hakika.

Miundombinu ya usafirshaji na huduma za maji na umeme kila kona ya nchi na kwa kiwango cha hali ya juu.

Baada ya hapo nasema wazi

#VIVA JOHN POMBE MAGUFULI.[emoji1241][emoji818] WATANZANIA TUKO NYUMA YAKO NA TEMBEA KIFUA MBELE!
Umeandika kishetani
 
Hiyo ni kauli thabiti. Ni sawa na ile ya shahidi wa uganda aliyeifia dini ya Kikristo. Alipewa vitisho, aliona wenzake wakiuawa, na yeye akielekea kwenye njia ya kifo lakini bado kwa ujasiri mkubwa alinena:

INANIPASA KUMHESHIMU MUNGU ZAIDI KULIKO MWANADAMU

Kama raia wema kwa Taifa letu na watu tunaomtii Mungu, pale viongozi wetu wanapokengeuka na kutoheshimu katiba yetu, SISI TUNASTAHILI KUSIMAMA KATIKA UKWELI WA KUHESHIMU NA KULINDA KATIBA. Yatupasa kunena kwa ujasiri:

TUNASTAHILI KUILINDA, KUHESHIMU NA KUIFUATA KATIBA kuliko kauli ya mtawala iendayo kinyume na katiba yetu. Na kauli yetu iwe thabiti hasa, na mtawala mwenye kutenda kinyume na katiba aweze kufahamu kuwa hana nafasi ya kuongoza Taifa letu.
Umenena vyema lakini bana kuba aliyajua haya mapema nio maana asubuhi na mapema akaingiza ukabila sehemu zote nyeti ili iwe rahisi kuyavuruga yote yenye mantiki
 
“Niguse ninuke”

"Baba Askofu Emmaus Mwamakula!

Tumsifu Yesu Kristo!

Napenda nikushukuru sana kwa ujumbe mzito na wenye tija katika Taifa. Nikiri kwamba nami nimekuwa nakufuatilia sana kwa maoni na ushauri mbalimbali ambao umekuwa ukiutoa kwenye mitandao. Endelea kufanya hivyo! Nikiri pia kuwa nimekuwa nafuatiliwa, nazushiwa shutuma za hatari kama vile za uhaini, usaliti, ufisadi, uhujumu, kufanya kampeni ya Urais nk.

Nikuhakikishie hakuna hata chembe ya ukweli kuhusu yote hayo na ndiyo maana huoni na hutaona hatua za kisheria zikichukuliwa dhidi yangu. Labda wanichukulie hatua zingine! Nimepata vitisho mbalimbali kutoka kwenye Chama changu, makundi mbalimbali ya wachawi na Serikali vya kunifukuza, kuniloga, kunitupa Gerezani kana kwamba mimi ni mhalifu. Baba Askofu, kwa kuwa moyo wangu ni safi, na kwa kuwa sijatenda kosa lolote, SITISHIKI , SITAKAA KIMYA na KAMWE SITAABUDU MTU WALA MIUNGU WENGINE.

Ninakushukuru sana kwa ushauri na maneno ya busara uliyonipatia. Tusipotokea wachache wa kuyasema na kuyakemea mabaya Baba Askofu, nchi hii itaingia kwenye matatizo makubwa zaidi ya haya tunayoyaona! Serikali ya Awamu ya tano imepewa ridhaa ya Uongozi na sisi wenyewe. Lakini leo sisi tunaonekana ni maadui wa Serikali na hakuna jema lililofanywa na awamu zilizopita. Ninawasikitikia washauri wanafiki na waoga wanaokaa kimya au kumshauri vibaya Rais wetu. Wanafiki wanaomlinganisha Rais wetu na Yesu na wanaomwomba Mungu amshukuru Rais wetu kwa yote anayoyafanya. Pamoja na makosa yote yaliyofanywa na Awamu zilizopita, Serikali na Viongozi hao walijitahidi kuheshimu Katiba, Uhuru, Sheria na Haki za binadamu. Huo ndiyo msingi wa Uongozi Bora Duniani.

Baba Askofu, usichoke kutushauri na kutupa moyo wa kuyatenda yale ambayo yatampendeza Mungu. Unifikishie salaam zangu kwa Maaskofu wote! Ubarikiwe sana Baba Askofu Mkuu Emmaus Bandikile Mwamakula na tuzidi kuombeana.

Bernard K. Membe. Mstaafu!"

NB: Waraka huo hapo juu kutoka kwa Mheshimiwa Membe (pichani), umenifikia leo kupitia nami nimeona niuweke hapa hasa ikizingatiwa kuwa ujumbe wangu wa awali kwake niliuweka hapa pia.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani (World Fellowship of Moravian Revival Churches)

-------

****UJUMBE WA ASKOFU MWAMAKULA ULIOJIBIWA NA BERNARD MEMBE****​

UJUMBE MAHSUSI KWA MHESHIMIWA BERNARD MEMBE.

Mheshimiwa Bernard Membe!

Pokea salaam za upendo kutoka kwangu mimi niliye mdogo sana miongoni mwa Maaskofu wa Kanisa la Mungu hapa duniani nisimamaye katika zamu yangu sasa! Nimekuwa nikifuatilia kwa makini na kusikia mengi juu yako katika siku za hivi karibuni. Ninatambua kuwa wewe ni mwanasiasa na siasa ni uwanja wa hoja.

Hata hivyo, kwa mazingira yalivyo tumeshuhudia kauli nyingi kukuzunguka wewe ambazo wakati mwingine zinatia hofu na mashaka. Kauli zinazoashiria kuwa siasa za Tanzania zimeanza kuonyesha dalili za watu kuanza kukosa kuvumiliana hasa pale watu wengine wanapoonyesha muono tofauti wa mambo.

Ninapenda nikuhakikishie kuwa pamoja na ukimya wao, Maaskofu walio wengi katika Nchi hii wanafuatilia kwa karibu sana mambo yanayohusu nchi hii ambayo Mungu amewaweka kuwa watumishi na mawakili wa siri zake. Pengine utatiwa moyo kusikia kuwa mimi pamoja na Maaskofu, Wachungaji, na watu wengine wengi usiowajua tunakuombea na kulitaja jina lako mbele za Mungu wetu.

Tunapenda ifahamike kuwa kukuombea kwetu hakutufanyi sisi kuwa lazima tukubaliane na muono wako wa mambo kuhusiana na siasa za Nchi hii, la hasha! Bali tunakuombea kutokana na ukweli kuwa kwa mazingira yaliyopo sasa baadhi yetu tunahisi kuwa unaweza kujikuta unaishi katika maisha ya hofu na wasiwasi mkubwa.

Tunamuomba Mungu ili akupe utulivu moyoni na pia akupe ulinzi dhidi ya watu ambao wanaweza kutaka kukudhuru kutokana na wao kutokupenda misimamo na mitazamo yako. Kwa kuwa na washindani wako na wao pia watausoma ujumbe huu, tunawasihi sana wasije wakaingia katika mtego wa kugusa uhai wako. Lakini pia, na wewe uepuke kuingia katika mtego wa kutaka kuwadhuru washindani wako. Mungu wetu atahusika na mtu ye yote anayejipanga kumwaga damu ya mtu mwingine iwe yeye mwenyewe au kuwatumia watu wengine.

Tunapenda wanasiasa wote wafahamu kuwa Mungu anapotoa kibali kwa mtu, kibari hicho hakiwezi kuondolewa na mtu au mamlaka ye yote ya kidunia. Kupambana na mtu aliyepata kibali kwa Mungu ni sawa na kupambana na Mungu mwenyewe. Tunapenda ifahamike kuwa kama wapo watu ambao Mungu amewapa kibali, wewe ukipambana nao utakuwa unajisumbua bure. Lakini pia, kama wewe utakuwa umepata kibali kutoka kwa Mungu, basi wale watakaoinuka kupambana na wewe na wao watakuwa wanafukuza upepo!

Tunakemea mambo yote ya kutishana na kunyamazishana na hata kutaka kupotezana miongoni mwa wanasiasa iwe ni katika Vyama vya Upinzani au ndani ya Chama Tawala. Kiongozi ye yote atakayeasisi au kushiriki katika vikao au mikakati ya kutaka kumuua mtu mwingine kwa sababu za kisiasa na mambo mengine nje ya mfumo na mchakato wa ki-Mahakama atakuwa anajitoa mwenyewe katika kibari cha Mungu kwa kuwa damu ya mtu haiwezi kumwagika bure pasipo kupiga kelele!

Ninaomba ukipata nafasi uweze kutafakari kwa kina Zaburi 35.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula -
Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani
Ahsante tuondoke ngoma acha inoge"SITISHIKI , SITAKAA KIMYA na KAMWE SITAABUDU MTU WALA MIUNGU WENGINE."
 
Ubarikiwe sana Baba Askofu Mkuu Emmaus Bandikile Mwamakula na tuzidi kuombeana


Hapa ndipo hivi vyeo vinanichanganya! Askofu Mkuu, wa chini yake ni Maaskofu wepi?
 
Hayo mabilioni ya Libya, una kielelezo chochote? Naamini siyo kweli.

Kama ingekuwa ni kweli, yaani kwa utawala huu na jinsi unavyomchukia Membe, angekuwa wa kwanza kufunguliwa kesi ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha.

Kwa sababu hakuna lolote mpaka sasa dhidi yake, itakuwa ni kweli kuwa anasingiziwa.
ndo mana kishasema madai yooote wanayomshushia hayana ukweli kama ukweli upo mbona hawamkamati?
 
"Tumwombe mungu amshukuru Rais Magufuli kwa anayoyafanya"
​
Aliyeelewa maana ya 👆 hiyo kauli aseme neno.
 
Awamu zote nne zilizopita hazijafanya chochote kabisa

Tumwombe mungu amshukuru Rais Magufuli kwa anayoyafanya
1570629261207.png
 
Tatizo siyo kula tu je nchi inajengwa
hata watangulizi wake pia walijenga nchi,,hawakuiacha tu,,unaonaje km magufuli angeingia madarakani ndio aje aanze ujenzi wa daraja la kigamboni?,,yy ameingia madarakani akaja kulifungua tu,wenzake walotangulia walijenga,ungeonaje km yy mtukufu wako ndio angekuja kuanza ujenzi wa uwanja mpya wa mpira wa miguu?,,ungeona vizuri km hadi leo tungekua tukitoka arusha kwenda mwanza lami tunaiacha pale minjingu kisha tunachakata vumbi hadi shinyanga?,,leo hii minjingu bbt ni lami,bbt singida ni lami,singida mwanza ni lami,bbt dodoma ni lami,dodoma iringa ni lami,,kote huko na kwingine ni maendeleo yalijengwa na watangulizi wa mtukufu wenu ila leo mnawaona hawakufanya kitu ila walikula tu,,wasingefanya hayo kipindi cha uongozi wao leo hii mtukufu wenu asinge nunua ndege hata moja ila angejenga barabara na asingeweza kufanya chochote anachofanya sasa ila angeanza kuziba ma gap ya nyuma kwanza lkn kumbe kabla yake ma gap yalishazibwa so yy anaendeleza mbele..kingine tu ujaribu kujifunza kuwa maendeleo ya nchi yyt duniani sio kuwa na miundombinu na uzuri wa miji yako sio utajiri wa nchi yako
 
NIGUSE NINUKE
Mwanakondoo ameshinda,
NIGUSE NINUKE!

"Sitaabudu Mtu au Miungu Wengine"
tumfuate!

C&P “Kuna mtu mmoja anaitwa Bernard Membe namuona anavyohangaika hangaika leo nina safari ya kwenda China kwa ziara ya kikazi. Membe namuweka kiporo nikirudi nitashgulika naye kwa sababu namjua vizuri na hana chochote,” LIVINGSTONE LUSINDE a.k.a kibajaji (MB) Mtera
 
Back
Top Bottom