Waraka wa Bernard Membe kwa Askofu Mwamakula: Sitishiki, sitakaa kimya na kamwe sitaabudu mtu wala miungu wengine

Waraka wa Bernard Membe kwa Askofu Mwamakula: Sitishiki, sitakaa kimya na kamwe sitaabudu mtu wala miungu wengine

Kama siyo fisadi kwanini anamchukia magufuli siange shikamana naye Leo wauza ngada na mafisadi ndiyo wanamaumivu na magufuli
Wacha porojo.
Kuna Mahali Membe kasema anamchukia Magufuli ?
Au kamtaja Magufuli.
Hivi wengine mmeishia darasa la ngapi ?
Kwanini msiwe mnakomenti kule Jukwaa la ChitChat.
Huoni kuwa unajivua nguo huku...!
 
“Niguse ninuke”

"Baba Askofu Emmaus Mwamakula!

Tumsifu Yesu Kristo!

Napenda nikushukuru sana kwa ujumbe mzito na wenye tija katika Taifa. Nikiri kwamba nami nimekuwa nakufuatilia sana kwa maoni na ushauri mbalimbali ambao umekuwa ukiutoa kwenye mitandao. Endelea kufanya hivyo! Nikiri pia kuwa nimekuwa nafuatiliwa, nazushiwa shutuma za hatari kama vile za uhaini, usaliti, ufisadi, uhujumu, kufanya kampeni ya Urais nk.

Nikuhakikishie hakuna hata chembe ya ukweli kuhusu yote hayo na ndiyo maana huoni na hutaona hatua za kisheria zikichukuliwa dhidi yangu. Labda wanichukulie hatua zingine! Nimepata vitisho mbalimbali kutoka kwenye Chama changu, makundi mbalimbali ya wachawi na Serikali vya kunifukuza, kuniloga, kunitupa Gerezani kana kwamba mimi ni mhalifu. Baba Askofu, kwa kuwa moyo wangu ni safi, na kwa kuwa sijatenda kosa lolote, SITISHIKI , SITAKAA KIMYA na KAMWE SITAABUDU MTU WALA MIUNGU WENGINE.

Ninakushukuru sana kwa ushauri na maneno ya busara uliyonipatia. Tusipotokea wachache wa kuyasema na kuyakemea mabaya Baba Askofu, nchi hii itaingia kwenye matatizo makubwa zaidi ya haya tunayoyaona! Serikali ya Awamu ya tano imepewa ridhaa ya Uongozi na sisi wenyewe. Lakini leo sisi tunaonekana ni maadui wa Serikali na hakuna jema lililofanywa na awamu zilizopita. Ninawasikitikia washauri wanafiki na waoga wanaokaa kimya au kumshauri vibaya Rais wetu. Wanafiki wanaomlinganisha Rais wetu na Yesu na wanaomwomba Mungu amshukuru Rais wetu kwa yote anayoyafanya. Pamoja na makosa yote yaliyofanywa na Awamu zilizopita, Serikali na Viongozi hao walijitahidi kuheshimu Katiba, Uhuru, Sheria na Haki za binadamu. Huo ndiyo msingi wa Uongozi Bora Duniani.

Baba Askofu, usichoke kutushauri na kutupa moyo wa kuyatenda yale ambayo yatampendeza Mungu. Unifikishie salaam zangu kwa Maaskofu wote! Ubarikiwe sana Baba Askofu Mkuu Emmaus Bandikile Mwamakula na tuzidi kuombeana.

Bernard K. Membe. Mstaafu!"

NB: Waraka huo hapo juu kutoka kwa Mheshimiwa Membe (pichani), umenifikia leo kupitia nami nimeona niuweke hapa hasa ikizingatiwa kuwa ujumbe wangu wa awali kwake niliuweka hapa pia.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani (World Fellowship of Moravian Revival Churches)
Huu mwiba una sumu kali sana, tutaelewana tu. Kwa nguvu zetu wenyewe tumeshindwa tumeamua kuomba huruma ya mwenyezi mungu. Membe; Mwenyezi alishasahau haya unayomkumbusha ''Wanafiki wanaomlinganisha Rais wetu na Yesu na wanaomwomba Mungu amshukuru Rais wetu kwa yote anayoyafanya'' unamkumbusha Mungu ili iweje?, ukimya wako ulikuwa unawapa watu shida sana maana hakuna aliekuwa anajua unapanga nini, umeanza kuongea tena utaharibu mipango yetu tena. Kaa kimya mbona njia iko wazi kabisa.
 
Kwa mtindo wa utendaji wa utawala huu wa awamu ya tano, tusije shangaa "wakamzushia" huyo Askofu na Membe wake, kuwa wote siyo raia wa nchi hii!
Ikitokea hivyo WaMoravian wote kwa umoja na wingi wao wasimpigie kura Jiwe na CCM yake!
 
Chadema mpeni Membe nafasi agombee urais maana mnampenda sana
 
Njaa ndio inamsumbua Membe. Anafikiri serikali ya sasa ni ile ya watu wa pwani, kingozi kama yeye alitakiwa kutumia busara na kuacha kufata maneno ya mitandaoni na mitaani. Kwani mpaka sasa ameitwa na chama chake na kupewa onyo? Au amefunguliwa kesi ? Sasa mbona anajishakia shakia?
Njaa ipi aliyonayo uwoga hofu aliyonayo huyu Mungu wenu ndio chanzo cha ugoro wote huo nani aliye anza kumtukana membe???
Base to the fact bana unajichotowa sio eeehh? Talking about a shot memories sio?
 
Tutasikia na kuona mengi.

Acha movi iendelee.
 
Sijui lini na Masheikh watakumbukwa nao waombwe kuwaombea waumini.

Mimi naeaona mnavyoinajisi nchi hii kwa kuingiza haya mambo ya udini dini na ukanisa kanisa.

Mhe. Membe kwa hili unalolifanya lutafakari upya ni siasa mbaya sana. Tanzania yetu Ni kubwa kuliko udini wenu, ukabila wenu na ukanda wenu.
 
Membe ni Kati ya watu wenye uwezo mkubwa sana wa Akili na Uongozi.

Ni kwa sababu tu hapa nchini hatuna utaratibu wa kuwafanyia midahalo Viongozi wetu wanaogombea cheo cha Urais

Kama tungefanya midahalo ya wagombea ni wagombea wachache sana wangeweza kufikia kiwango cha Membe cha kujieleza.
Membe ni Genius, huwezi simama nae kwenye mdahalo na ukamshinda kirahisi.

Jambo jingine, Membe Yuko humble, hana makuu na anawajari watu sana.
Cheo cha Uraisi ni kama bahati vile, ila Membe ana hadhi ya kuwa Raisi wa Tanzania.

Namna moja ya kumpima mtu mwenye IQ kubwa ni kumsikia anavyo weza kujieleza na kuyaelezea maswala mbali mbali.
Ndio maana nchi zilizoendelea Kama Marekani wagombea Uraisi hupitia midaharo mingi.

Hapa nasema ukweli mtu Kama Lowasa uwezo wa kujieleza ni Zero. Na angebahatika kupata Urais mambo mengi yangefanywa naw engine
Nchi hii kutoka na taratibu mbovu zinazofatwa ili kumpata Raisi wa nchi iko siku tutampata Raisi Zero Brain, au MWENDAWAZIMU.

La tuanze kuwafanyia midahalo wagombea wetu ili tujiridhishe na utimamu wao.
Alisikika akisema NAJUA WOTE MNATAKA NYAMA LAKINI SI MSUBIRI BANDA LIJAE, alimalizia yule asiyependa kuvaa viatu.
 
Wacha porojo.
Kuna Mahali Membe kasema anamchukia Magufuli ?
Au kamtaja Magufuli.
Hivi wengine mmeishia darasa la ngapi ?
Kwanini msiwe mnakomenti kule Jukwaa la ChitChat.
Huoni kuwa unajivua nguo huku...!
Jamaa amenena maneno magumu sana kueleweka kwa baadhi ya watu. Unatakiwa uyasome na uyatafakari ndipo utamuelewa. Hasemi mtu ila anatoa hadhari na kuuhabarisha umma
 
Nashauri walaka huu uwekwe kama kumbukumbu ya yanayozidi kutokea huko mbele..
Kwani waweza kuwa mwiba kwa wote wawili au kuwa balabala nyoofu kwa Membe.

Kama mtanzania napenda majadiliano zaidi kuliko vitisho na ubabe kwenye maamuzi.
 
Jap ni kuhoji tu na sio mahakamani..
Kweli membe ameandika "niguse ninuke"
Au mbwembwe za mwandishi?
 
NIGUSE NINUKE
Acha wamguse tuone kama atatoa harufu yoyote ya kunuka kama anavyodai. Hamna chochote hapo ni makelele ya kujihami tu hayo! Aliguswa mamvi akajifanya kususa, lakini mwenyewe kajirudisha Kwa USO wa soni, sasa hivi kimyaaaa utafikiri hayupo. Hakuna aliye mkubwa kuliko chama, huko ni kujidanganya tu! Huyo mbeme ni MTU Mdogo sana na alipaswa akishukuru chama na uongozi wake maana bila chama hakuna ambaye angekuwa anamjua mbeme Leo!
 
Membe endelea hii nchi siyo ya Jiwe, sasa anavyojimwambafy kwani yake si kakabidhiwa tu dhamana, sasa limbukeni kaona waliomkabidhi wajinga, bado anatesa, anadhulumu watu, kaua uchumi, biashara, sekta binafsi, kaharibu maisha ya watanzania, kaleta ufukara wa kutisha kwa watanzania, hafai, anajidai anajua kila kitu, hashauriki, anajimwambafy hata kwa mambo asiyostahili.
 
Membe ni Kati ya watu wenye uwezo mkubwa sana wa Akili na Uongozi.

Ni kwa sababu tu hapa nchini hatuna utaratibu wa kuwafanyia midahalo Viongozi wetu wanaogombea cheo cha Urais

Kama tungefanya midahalo ya wagombea ni wagombea wachache sana wangeweza kufikia kiwango cha Membe cha kujieleza.
Membe ni Genius, huwezi simama nae kwenye mdahalo na ukamshinda kirahisi.

Jambo jingine, Membe Yuko humble, hana makuu na anawajari watu sana.
Cheo cha Uraisi ni kama bahati vile, ila Membe ana hadhi ya kuwa Raisi wa Tanzania.

Namna moja ya kumpima mtu mwenye IQ kubwa ni kumsikia anavyo weza kujieleza na kuyaelezea maswala mbali mbali.
Ndio maana nchi zilizoendelea Kama Marekani wagombea Uraisi hupitia midaharo mingi.

Hapa nasema ukweli mtu Kama Lowasa uwezo wa kujieleza ni Zero. Na angebahatika kupata Urais mambo mengi yangefanywa naw engine
Nchi hii kutoka na taratibu mbovu zinazofatwa ili kumpata Raisi wa nchi iko siku tutampata Raisi Zero Brain, au MWENDAWAZIMU.

La tuanze kuwafanyia midahalo wagombea wetu ili tujiridhishe na utimamu wao.
Kuwa na akili nyingi hakumfanyi MTU kuwa mwadilifu, akili siyo kigezo cha kwanza cha kuwa Rais Bali UADILIFU ndiyo kigezo mama cha kuwa Rais mzuri wa nchi!!!! Watanzania tulijue hilo! Kuna harufu kali katika kigezo cha uadilifu kinachomnyima sifa Huyo mbeme!!
Tuwe wa kweli, hivi kuna mtanzania yeyote aliye mfuatiliaji wa siasa za nchi hii ambaye hajawahi kusikia harufu mbaya kimaadili kuhusu mbeme? Aweza kuwa mwanadiplomasia mzuri sana, aweza kuwa na akili sana, aweza kuwa na uwezo mkubwa was uongozi, lakini Kwa harufu hii hatufai!!.
Kwa kuzingatia jinsi Rais alivyo na madaraka makubwa sana kwenye hizi nchi zetu, Rais akikosa uadilifu ni majanga makubwa!!, nchi inaweza kuuzwa, raslimali zinaweza kuuzwa nk!!
 
Back
Top Bottom