Waraka wa Marehemu Chacha Wangwe na Hatma ya Siasa za CHADEMA

Waraka wa Marehemu Chacha Wangwe na Hatma ya Siasa za CHADEMA

makamo chacha wangwe kaandika waraka huu

makamo wa chama Arif kaachia manyanga kwa kua hawaendani na mwenyekiti

naibu katibu wa chama bwana zitto nae yamemfika yalipomfika kisa mwenyekiti

jamani huyu mwenyekiti ana nn ? nnaona chadema ijiangalie sana. maana sasa nnaona zile kauli za mwalimu kua wapinzani bado kuaminiwa kupewa nchi. uongozi wa nchi haujaribiwi

dhahiri kua wananchi weshaichoka ccm, wanatamani sana chama mbadala wanatamanikufanya mabadiliko, lakin chama gani kinawapa matumaini watanzania? kwa sasa hamna.

warioba hapendi ubabe wa chama chake, analalama kua ccm wanawalazimisha wananchi kukubali katiba yenye mapendekezo ya ccm, lakini wakati huo anakiri kua wapinzani bado kuwachia nchi.

kuna ttz
 
kila siku SISI TUNASEMA KWAMBA CHADEMA NI CHAMA CHA UDINI UKANDA NA UKABILA NASHANGAA SIJUI KWA NN HAWA WATU HAWATUELEWI


1.ALIANZA CHACHA WANGWE KUTAKA KULETA MABADILIKO KWENYE HII SACCOSS YAO,WAKAMTENGENEZEA ZENGWE HAWA WACHAGA WA CHADEMA,WAKAONA HIYO HAITOSHI WAKAMUUA MOJA KWA MOJA,KISA ETI ANAVUJISHA SIRI KWA CCM,SIRI GANI??HAWAZISEMI,ILI HALI UKABILA NI SUALA LILILO WAZI KABISA NDAN YA CHAMA HIKO.

2.SAID ARFI NAE WASHAMWEKEA ZENGWE KWA SABABU HIZO HIZO NA HATAKIWI KWENYE CHAMA CHAO CHA UDINI NA UKABILA,

3.LEO HII TUNAONA ZITO KABWE YAMEMKUTA YALE YALE,SASA TUNAHOJI HIVI HAWA WACHAGA WA CHADEMA WANADHANI NANI NI MJINGA WA KUWAAMIN WAO KIAS CHA KUFIKIA KUWAPA DOLA??

HIVI NI NANI KAWAROGA WACHAGA HAWA.
 
R.I.P Chacha Wangwe...

Naamini huko uliko kama unaona yanayotokea duniani utakuwa unafurahia kuwa chama chako ulichokipenda kimezidi kukua na kuimarika zaidi na zaidi...
 
Huu ushabiki wa kisiasa utawaangamiza nyinyi msiojitambua, na kamwe hautawaacha salama. Mtatafuta kuivuruga Chadema lakini kamwe hamtaweza kuwavuruga Watanzania wenye nia madhubuti ya kuleta mabadiliko. Yawezekana malalamiko ya marehemu Wangwe yana msingi wake. Ila hapa ni vipi Zitto ameingia humo? Je, kipindi Wangwe anasimamishwa uongozi, Zitto alikuwa na mamlaka gani kwenye chama? Na je, Zitto aliyatumia mamlaka yake vipi kumsaidia Wangwe kama kweli anaonewa?

Wangwe alikiacha chama (kwa bahati mbaya kwa kufariki) akiwa na mawazo kuwa chama kisingestawi chini ya Mbowe. Mbona basi ndo chama kilikua zaidi na zaidi? Mbona basi nguvu ya chama imekuwa zaidi hadi huko vijijini kulikoonekana hakupati ruzuku? Naomba kusema kuwa, hapa mimi simtetei Mbowe, na sitaki kusema kwamba anakiendesha chama kiutukufu wote utakiwao. Hapa nikimaanishacho ni kuwa, wale wote wasababishao mipasuko kwenye vyama imara vya upinzani wanahafifisha ndoto za Watanzania kuuondoa ufisadi wa CCM madarakani. Watu hawa mimi binafsi siwezi kuwaona ni watu wazuri kamwe.

Tunayo mapambano kwenye nchi hii. Mapambano yetu si dhidi ya chama chochote cha siasa, bali ni mapambano dhidi ya mafisadi na mafisidi wa uchumi wa nchi yetu, rasilimali za nchi yetu. Watanzania tumeshachoka, na hatutajali mtu anayehafifisha harakati zetu ana umaarufu gani. Yeyote atakayejaribu kuvuruga harakati hizi, awe yuko Chadema, awe CUF, au awe CCM, ni hakika Mungu atasimama na Watanzania kumwadhibu mtu huyo.
 
Akili ndogo siku zote itabaki kuwa akili ndogo tu. Kolimba aliuwawa na Mainterahamwe kwa kusema ukweli kwamba "CCM imekosa mwelekeo" kwa maneno haya matatu tu MACCM wakaamua kuchukua uhai wa Kolimba. RIP Kolimba.
 
Na hii comment pia:
Sign in to reply
1/19/14johale14
Mollel,
Ni upofu usio mithilika kwa kuwaona Dr Kitila,Mwigamba,Zitto,Marehem Wangwe,M'kiti Mkoa Lindi kuwa hawajui wasemalo eti litakalosemwe na Mh Mbowe ndio sahihi.
Mzee Wangu Lwaitama alinishambulia kwa kuniita CCM kwa kuunga mkono maelezo ya Dr Kitila.wakati huohuo anatetea kuwa Mh Mbowe alichukuwa pesa kutoka Kada wa CCM na kuzitumia kujenga chama,Ila anasema Zitto alichukuwa pesa kutoka kwa watu haohao kwa lengo la kukihujumu chama.Shida inakuja sehemu moja ni ushahidi upi unaotumika kuhalalisha uchukuaji wa pesa izo? na ni vipi upande mmoja iwe haramu na upande mwingine iwe halali?
Magere- J.

Aibu...Aibu... Unachekesha; Hatuko tayari Kutuletea Uongo wako Hapa; Ya Chacha Wange yalishapita, Ya Mwampamba na Juliana Shoza, Ya Mwigamba na Prof. Kitila na Kwa Sasa Ya Zitto yanahitimishwa kwa Maana hayupo hai Chamani zaidi ya Mwaka sasa. Tusonge Mbele Majungu hayatatusaidia Kutimiza lengo la Kuchukua Dola.

Ukombozi wa Nchi Hii toka Kwa Mkoloni Mweusi CCM si lelemama, Ulianza Zamani, Wapo walioianza safari Vizuri lakini Mioyo yao na Miguu yao Ilipata Ganzi na Kupoteza balance " Walipigwa upofu na Fedha za CCM wakapoteza dira, Hao ni Wengi" . Maandiko yanasema sio wote wasemao Bwana, Bwana ni wa Bwana. Pia kwenye Kundi la Mamba Kenge siku zote hawakosekani.

Usaliti ni dhambi kama Dhambi ya Kumkufuru Roho Mtakatifu na zote Hazisameheki. Historia ya Usaliti ilikuwepo hata tunaambiwa Yuda Askariote alipata Kumsaliti Jesus christ kwa vipande thelathini vya Fedha.

South Africa wakati wa utawala wa Makaburu, Watu weusi Katika harakati za Kijikomboa swala la Usaliti liliwatesa sana, Ni kama yale tunayoyaona ndani ya CHADEMA.

Tofauti ya CHADEMA na ANC ni Kwamba Wasliti wa ANC walikuwa wakivishwa Tyre ya gari shingoni na Kupigwa Kibiriti hadi Majivu, lakini CHADEMA inawapasha Wasaliti wote Live na Kuwaeleza Kuwa Milango ya Kutoka iko wazi bila Kudhulika.

CCM wenyewe tunajua wanavyowafanya wale wote wanaopigana na Sera za Chama Chao ( Wasaliti wao), ni wengi tu Walishaenda kwa Pilato...Tukiwataja hapa Utasema ni kheli ya CHADEMA .
 
Hivi zitto na mbowe si ndo watu waliokwenda kupunguza munkari kwa watu wa Tarime juu ya fikra chafu za CCM? sasa leo hii mnakujaje na kuoanisha ili hali zitto alishiriki moja kwa moja juu ya maovu yote enzi ya Chacha Wangwe?

Ama ndo ile inamrudi na yeye kwa kuwa alishiriki na sasa yamrudia?
 
Na mbowe awashukuru usalama wa taifa kwenye msiba wa chacha wangwe la sivyo angekuwa marehemu sasa hivi.......
Naamini cku moja watanzania watajua ukweli kuhusu chadema watafute nyaraka nyingi za chacha wangwe na wengineo
 
Kinachoisaidia chadema kwa sasa ni koti la ukawa, soon kinakwenda kufa kama nccr tu
 
Na mbowe awashukuru usalama wa taifa kwenye msiba wa chacha wangwe la sivyo angekuwa marehemu sasa hivi.......
Naamini cku moja watanzania watajua ukweli kuhusu chadema watafute nyaraka nyingi za chacha wangwe na wengineo

Humu JF kama wengi wetu tungekuwa tunajitokezana majina halisi kuna watu wasingeweza kutembea mchana maana kila mtu angekuwa amewagundua kuwa ni mabongo lala ambayo hayastahili hata kuzungumza mbele za watu kwa kuwa uwezo wa ubongo wao hata mbuzi ana nafuu.
Kweli mtu mzima waweza kurudia maneno yale yale kila siku wakati majibu yake yalishawekwa wazi siku nyingi? Halafu watu mnaowasingizia wanazidi kukubalika na kusonga mbele nyie mpo palepale na maneno yale yale kama mazuzu?
 
Akili Ndogo Zinaonekana tu Ktk Kutoa Comments; Yaana watu walivyopigika unahitaja CCM hapa... Pole Kijana Kizazi Kipya...
Kupigika kwako kunatokana na upuuzi / Uvivu wako wa kujihangaisha usiisingizie CCM. Hakuna chama tawala chochote duniani kinacho badili maisha ya mtu, bali maisha ya mtu hubadilishwa na mtu mwenyewe.
 
Mh! Nashukuru sana sasa nimeelewa somo maana nilikuwa mbishi sana kumbe chadema ni zaidi ya janga la ebola.
 
Mapambano ya kuwaondoa mafisadi madarakani si kazi rahisi. Watatunga uongo mwingi, propaganda nyingi za uongo, watatuteka/ tesa/ ua lakini naamini tulio na moyo tutastahimili hadi mwisho. Hivi kweli wanataka kutuaminisha kwamba CHADEMA ni mbaya kiasi wao ni wazuri tuendelee kuwaacha madarakani!? Haiwezekani. October mwaka huu lazima watoke madarakani kwa namna yoyote ile.
 
Back
Top Bottom