Waraka wa TEC umesomwa kwenye Jumuia yangu ya Mt. Marcelino. Tunawashukuru Maaskofu. Kesho utasomwa vigangoni na Parokiani Mt. Antoni wa Padua

Kweli sasa kanisa limekwisha.
Enzi za Nyenyere na Mkapa haya mambo yalikuwa siri, lkn siku hz kanisa na wafuasi wake linabwata kila uchao
 
Hatuvunji tuone mtafanya nini
 
Mie ni Anglican, ILA wakatoliki hapo ndio nawapenda, they are very smart!
Msimamo unapokuwa ni wa TEC basi rasmi unakuwa wa wakatoliki wote[emoji122][emoji1666][emoji123]
Ni taasisi kubwa kuliko hata ccm yenyewe i swear
Kama kubwa kuliko CCM basi waweke Rais
 
Waambie wakujibu hao maaskofu.
Huku serikali ishamalizana na Mwarabu nyie endeleeni kubwata na nyaraka zenu pelekeni hadi Vatican.
 
Suala la bandari ni uelewa mdogo wa watanzania: Professor Mussa Assad former Controller and Auditor General
 
Naona kama kanisa langu katoliki limepotoka safari hii. Halijamtendea haki Rais Samia na wasaidizi wake.

Padre Kitina ni mwana CHADEMA na mfumo unamwangalia na kumheshimu kwani wanajua wapi watashughulika nae.
Hivi wee hujiulizi vipi huu mkataba ulianza kisirisiri mpaka dak za majeruhi ukatoka, wakati umeshaanza. kunani nyuma yake
 
Mimi pia ni Mkatoliki na kesho Jumamosi Jumuiya inasalia kwangu. Na Father Dk. Kitima ni Mwalimu Wangu SAUT. Siuungi mkono huo Waraka. Kanisa Katoliki Tanzania sio SI Unit ya maoni ya Watanzania. Eti Mababa Maaskofu wanasema maoni ya Wananchi wengi. Wana ushahidi?

Nakumbuka, TEC hawa hawa enzi za Mzee Che Nkapa (Mkatoliki kweri kweri) waliwahi kusema Wakatoliki ni wengi Tanzania kuliko waumini wa madhehebu mengine. Wakaambiwa walete ushahidi, wakaufyata.
Leo wamerudia tena. Ningekuwa Serikali, ningemuita Father Dk. Kitima aoneshe hao Wananchi wengi wanaokataa Mkataba. Akishindwa kunionesha, ANGEPOTEA!!!
 
Huu waraka wa TEC utatumiwa na watu wa dini zote. Huu waraka si wa kidini, ni wa maslahi mapana ya Watanganyika wote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…