MADAM T
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 5,747
- 2,977
Ubongo usipojaa vizuri, hii shida hutokea!Zwazwa ni mama yako aliyekuzaa na kukulea
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ubongo usipojaa vizuri, hii shida hutokea!Zwazwa ni mama yako aliyekuzaa na kukulea
Ukiyajua haya mambo kwa kina hauhitaji kuumiza kichwa.Pole, shughulisha ubongo!
[emoji1787]Mambo ya Escrow kamuulize JK ndie alikuwa architect.
Kweli sasa kanisa limekwisha.Leo Mambo yamependeza sana, Waraka wa TEC unaofafanua Mkataba wa Bandari za Tanzania na DPW ya Dubai wenye ujumbe mwanana wa Sauti ya Watu ni Sauti ya Mungu.
Yaliyojitokeza ni waumini kuuelewa na kuukubali. Pembezoni nimeteta na Mh. Mbunge wa Jimbo letu, Ni muumini wa Jumia hii, kwa ufupi anasema waraka huu na yeye na wengine umewapa amani, wamepata pa kushikia, Nafsi zao zilisongwa sana kwenye vikao ndani ya chama. lakini sasa wametua mzigo. Wanasubiri kama utarudi bungeni au utatupwa kapuni. Niliyyapata kwa waumini mchanganyiko, akina mama, wazee wa familia, wafanya biashara na mmoja mtu muhimu serikalini.
1. Wao kama WAKATOLIKI na Watanzania wako tayari kuulinda, kuutetea Waraka huu hata kama ni kimyakimya.
2. Serikali sasa iwe makini sana, kumbuka dini haina mipaka eneo la kazi, tumechanganyana humo, wako wabunge, mahakimu, mapolisi, wanajeshi, wakulima, walimu, madaktari, wafanyakazi bandarini, yaani popote na kwa kawaida WUMINI HUWA HATUPINGI MAELEKEZO YA KIROHO, KWA SASA KUTOKUBALIANA NA MKATABA WA BANDARI NI SUALA LA KIROHO.
3. Ujumbe huu ukiwa na hoja muhimu ni vema zijibiwe kwa uwazi na weledi, halafu waumini na viongozi wetu kiroho tukiyaelewa majibu yenu Spika, Rais, Prof. Mbarawa tutarudi kwa waumini kuwaambia mmeeleweka .
Asanteni kwa Sasa. Kesho nitahudhuria misa ya Kwanza, Asanteni Maaskofu.
Haizuii wenye bandari yao kufanya yaoNa usomwe makanisa yote hiyo kesho [emoji120]
Anakula bata tu.Mama yenu ana hali gani huko alipo?
Hatuvunji tuone mtafanya nini2. Serikali sasa iwe makini sana, kumbuka dini haina mipaka eneo la kazi, tumechanganyana humo, wako wabunge, mahakimu, mapolisi, wanajeshi, wakulima, walimu, madaktari, wafanyakazi bandarini, yaani popote na kwa kawaida WUMINI HUWA HATUPINGI MAELEKEZO YA KIROHO, KWA SASA KUTOKUBALIANA NA MKATABA WA BANDARI NI SUALA LA KIROHO
Nimekuelewa sana mkuu hasa hapo ulipo kazia kwa herufi kubwa, ni wakati sasa mama kuja mbele na kuvunja huo mkataba na wote waliokuwa mbele ya mkataba huu kuchukuliwa hatua akiwepo yeye mwenyewe
Kama kubwa kuliko CCM basi waweke RaisMie ni Anglican, ILA wakatoliki hapo ndio nawapenda, they are very smart!
Msimamo unapokuwa ni wa TEC basi rasmi unakuwa wa wakatoliki wote[emoji122][emoji1666][emoji123]
Ni taasisi kubwa kuliko hata ccm yenyewe i swear
Waambie wakujibu hao maaskofu.Inshort huo waraka ni lazima isimwe kwenye kila jumuiya, kigango, kabisa na parokia kui zote..., hadi vijijini pasipo hata na minara ya simu ni lazima upelekwe kwa maandishi na usomwe wote bila kuacha hata herufi!
Na hoja zijibiwe!!!
Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa
1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)
2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?
3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?
4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!
6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
Pesa za escrow kwani zilikuwa za umma hizo?Na pesa za escrow walizokula maaskofu wa TEC mmepewa kwenye vigango?
Atapewaje wakati yeye ndiye aliekuwa mgawajiHilo ndo jibu? Kwani JK alipewa mgawo?
Suala la bandari ni uelewa mdogo wa watanzania: Professor Mussa Assad former Controller and Auditor Generalwe ni mpuuzi, unafikiri wakishupaza shingo bandari ibinafsishwe unajua athari zake? Unaambiwa huo mkataba una magumashi mengi huelewi. Shenzi zako unafikiri ni wakatoliki tu ndio wanaopinga, wazalendo wote wa nchi hii hawakubaliani na uwekezaji huo tata
kama ni uelewa mdogo toeni elimu ili watanzania wawe na uelewa mkubwaSuala la bandari ni uelewa mdogo wa watanzania: Professor Mussa Assad former Controller and Auditor General
Hivi wee hujiulizi vipi huu mkataba ulianza kisirisiri mpaka dak za majeruhi ukatoka, wakati umeshaanza. kunani nyuma yakeNaona kama kanisa langu katoliki limepotoka safari hii. Halijamtendea haki Rais Samia na wasaidizi wake.
Padre Kitina ni mwana CHADEMA na mfumo unamwangalia na kumheshimu kwani wanajua wapi watashughulika nae.
Elimu inaendelea kutolewa changamoto iliyopo mwekezaji ni mwarabu maaskofu wanaogopa labda wanahisi amekuja kueneza dini ya kiislamu.kama ni uelewa mdogo toeni elimu ili watanzania wawe na uelewa mkubwa
Kumbuka kanisa si chama, na kumbuka Raisi hupatikana kupitia chama cha siasa, kulingana na katiba yetu.Kama kubwa kuliko CCM basi waweke Rais
Mimi pia ni Mkatoliki na kesho Jumamosi Jumuiya inasalia kwangu. Na Father Dk. Kitima ni Mwalimu Wangu SAUT. Siuungi mkono huo Waraka. Kanisa Katoliki Tanzania sio SI Unit ya maoni ya Watanzania. Eti Mababa Maaskofu wanasema maoni ya Wananchi wengi. Wana ushahidi?Leo Mambo yamependeza sana, Waraka wa TEC unaofafanua Mkataba wa Bandari za Tanzania na DPW ya Dubai wenye ujumbe mwanana wa Sauti ya Watu ni Sauti ya Mungu.