Waraka wa TEC umesomwa kwenye Jumuia yangu ya Mt. Marcelino. Tunawashukuru Maaskofu. Kesho utasomwa vigangoni na Parokiani Mt. Antoni wa Padua

Waraka wa TEC umesomwa kwenye Jumuia yangu ya Mt. Marcelino. Tunawashukuru Maaskofu. Kesho utasomwa vigangoni na Parokiani Mt. Antoni wa Padua

Inshort huo waraka ni lazima isimwe kwenye kila jumuiya, kigango, kabisa na parokia kui zote..., hadi vijijini pasipo hata na minara ya simu ni lazima upelekwe kwa maandishi na usomwe wote bila kuacha hata herufi!

Na hoja zijibiwe!!!

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
2. Serikali sasa iwe makini sana, kumbuka dini haina mipaka eneo la kazi, tumechanganyana humo, wako wabunge, mahakimu, mapolisi, wanajeshi, wakulima, walimu, madaktari, wafanyakazi bandarini, yaani popote na kwa kawaida WUMINI HUWA HATUPINGI MAELEKEZO YA KIROHO, KWA SASA KUTOKUBALIANA NA MKATABA WA BANDARI NI SUALA LA KIROHO

Nimekuelewa sana mkuu hasa hapo ulipo kazia kwa herufi kubwa, ni wakati sasa mama kuja mbele na kuvunja huo mkataba na wote waliokuwa mbele ya mkataba huu kuchukuliwa hatua akiwepo yeye mwenyewe
yeye mwenyew kala ela
 
Mie ni Anglican, ILA wakatoliki hapo ndio nawapenda, they are very smart!
Msimamo unapokuwa ni wa TEC basi rasmi unakuwa wa wakatoliki wote👏🤝💪
Anglican walivurunda walivyomualika juzi kufungua jengo lao Dodoma.

Haukuwa muda muafaka, walichofanya ni sawa na kilichofanywa na Simba S C.
 
Leo Mambo yamependeza sana, Waraka wa TEC unaofafanua Mkataba wa Bandari za Tanzania na DPW ya Dubai wenye ujumbe mwanana wa Sauti ya Watu ni Sauti ya Mungu.
Yaliyojitokeza ni waumini kuuelewa na kuukubali. Pembezoni nimeteta na Mh. Mbunge wa Jimbo letu, Ni muumini wa Jumia hii, kwa ufupi anasema waraka huu na yeye na wengine umewapa amani, wamepata pa kushikia, Nafsi zao zilisongwa sana kwenye vikao ndani ya chama. lakini sasa wametua mzigo. Wanasubiri kama utarudi bungeni au utatupwa kapuni. Niliyyapata kwa waumini mchanganyiko, akina mama, wazee wa familia, wafanya biashara na mmoja mtu muhimu serikalini.
1. Wao kama WAKATOLIKI na Watanzania wako tayari kuulinda, kuutetea Waraka huu hata kama ni kimyakimya.
2. Serikali sasa iwe makini sana, kumbuka dini haina mipaka eneo la kazi, tumechanganyana humo, wako wabunge, mahakimu, mapolisi, wanajeshi, wakulima, walimu, madaktari, wafanyakazi bandarini, yaani popote na kwa kawaida WUMINI HUWA HATUPINGI MAELEKEZO YA KIROHO, KWA SASA KUTOKUBALIANA NA MKATABA WA BANDARI NI SUALA LA KIROHO.
3. Ujumbe huu ukiwa na hoja muhimu ni vema zijibiwe kwa uwazi na weledi, halafu waumini na viongozi wetu kiroho tukiyaelewa majibu yenu Spika, Rais, Prof. Mbarawa tutarudi kwa waumini kuwaambia mmeeleweka .

Asanteni kwa Sasa. Kesho nitahudhuria misa ya Kwanza, Asanteni Maaskofu.
Walaka umelenga uwafikie viongozi wootw kokote waliko makanisani, jumuiyani na Kwenye vigango.

Kesho utasomwa Nchi nzima
 
DP world wameshaingia nchini kazi inaendelea.nendeni mkashtaki Vatican
kwan athari za mkataba huu watapata wavatican ? ukiitwa nyqn unalalamika , ila akili zako znasadiki , hili sio swala la kidin hata kdg , kama waarab wana nia njema kwann watumie njia za panya ? zaid ya 1B imetumika kutoa rushwa ili mkataba upitishwe , jiulize wabunge , waandishi wa habari na viongoz wa serikalin wote wamepewa mgao
 
Back
Top Bottom