Huu waraka wa TEC ni "pandora"s box" ya mabadiliko makubwa yatakayokuja ya kiutawala ndani ya nchi yetu. Badala ya watu kujikita katika kujibu hoja, sasa zinatafutwa sababu dhaifu na za kihistoria na zenye sura ya kidini ili kukwepa hoja iliyopo mezani.
Ilianza na suala la Uzanzibar kutaka sababu za kuokoteza katika sakata hili la bandari ila zikabuma, ikaja sababu za uanamke wa mama Abdul nazo zikafeli, walitafutwa chawa wakashindwa kuzimisha hoja iliyotolewa, makada wakajipanga kuzunguka nchi nzima ili kutoa elimu ila watu wakapuuzia, zikaja kesi za mchongo za kubambikia watu uhaini ila imebuma, sasa dini inaanza kutumika kama silaha ya mwisho.
Sasa litafumuka jingine kuhusu ilipo ndege ya Rais na sababu za kuwepo kwa hapo ilipo. Kama nalo litathibitika kuwa linahusiana na sakata hili la DPW, basi tegemea na lingine pia litafuatia. TEC ni baraza ambalo kamwe huwa halikurupuki, ukiliona tamko mwenye busara na hekima huwa anlifanyia kazi, na wala siyo kulifanyia dhihaka.