Hii ni hatua njema sana kwa hakika. Hapa ikiwa ninakuelewa sawasawa kuwa:
"Sote kwa umoja wetu, na tuwakemee wote wakiwamo masheikh hawa na wafuasi wao kama lengo ni kutaka kutupeleka kwenye ubaguzi ukiwamo wa kidini ambako hakuhusiki kabisa na jambo hili."
Suala la DPW si la dini, kabila, kanda, jinsia, nk. Hili ni suala la kimkataba ambao kama hauna maslahi, haipo shaka kuwa hautufai.
JF kuruhusu anonymity yaani kuficha utambulisho wa watu ni pamoja na haya ya udini yasiyo na maana yakiwamo nilipo, kabila, ajira, mtandao wa simu, umri, nk.
Aghalabu dini yangu haibatilishi lolote katika mjadala huu.
Hapa tofautisha waislam na masheikh kwa upande mmoja na masheikh hawa na wafuasi wao ninaothubutu kuwaita uchwara kwa upande mwingine.
Zingatia hata huyu ni sheikh wa kiislam niliye na heshima kubwa kwake:
View attachment 2727125
Kwani wewe wamwona je huyu ndugu?
Matumizi ya neno
wenu Wala yasikutie kimuhemuhe.
Kiongozi yeyote ni wenu kama mnaona anawafaa hali sisi wengine tukiona hatufai. Vivyo hivyo ni wetu kama anatufaa hata kama nyie hawafai.
Huu ndiyo ulio uungwana kutokea pande za kwetu kwa kiongozi yeyote: awe mkristo, muislam, baniyani, Buddha, mpagani, nk.
Hapa ni muhimu sana kutambua hatujafahamiana kabisa. Zingatia mantiki badala ya kucheza na kiswahili ambacho sote sisi ni wabobezi, bila kusahau maneno matupu hayavunji mfupa:
1. Tambua Mikataba ni suala la kisheria.
2. Faida na hasara kwa mkataba huchambuliwa na watalaamu. Nilikuorodheshea manguli wenye kofia za u Prof, DKt na wanasheria wasomi kwenye hilo. Kina yakhe kama mimi na wewe, tupa kule!
Ni wazi kuwa hukunielewa. Kwamba ungali huelewi mbona itakuwa shughuli?
Hasara za mkataba wa DPW ni nyingi na mojawapo ni huko kutokuwa na ukomo kama wabobezi wanavyotwambia.
Faida na hasara hung'amuliwa kitalaamu kabla ya utekelezaji.
Hapa ndiyo maana wenye akili zao wako kimya, kuwaachia manguli wa sheria kuchakata hili vilivyo.
TEC ni wakristo. Tamko lao halijawakilisha wakristo bali watanzania wote. Humo tumo wakristo, waislam hata na wapagani. Tamko lao tunakubaliana nalo sisi dhidi ya hawa masheikh uchwara na wafuasi wao wenye kutaka kulifanya jambo hili kuwa ni la kidini.
Sisi pamoja na mzee kikwette tunawaasa masheikh hao na wafuasi wao, wasichanganywe dini na siasa. Kwamba katu mkataba wa DPW au tamko la TEC halina cha kufanya nao wala, ukristo, uislam, nk kama dini.
Hapa nilikutegemea nawe kuwa upande wetu Ili tushirikiane sote kuwaelekeza kwa staha mamburula hao wasiostaraabika wala kuwa na uelewa wowote.
Hili la kunufaika si suala la kulisemea. Ni suala la kulielewa. Zingatia ninaongea mantiki na si maneno matupu. Hatua mbele hupigwa mantiki inapoeleweka. Ina maana gani kufanya mazungumzo au majadiliano yasiyokuwa na mantiki?
Kuwa hutaki Kwa sababu hutaki tu? Huko ni kushupaa wakiita kukaza ubongo. Tofautisha kuwa na ubongo na kupania maembe mahala pake.
Hakuna nilipokuitisha kujadili yaliyopo kichwani kwangu ambayo unajua wazi kuwa huyajui na hutakaa uyajue. Nilidhani tunajadili ninayoandika hapa na kwa kuamini tunajadiliana kwa malengo yenye tija. Kwa sababu hiyo Siyo Siri kuwa nilikuwa nimeyapa umhuhimu wake majadiliano haya.
Nimekwambia sina na wala hatuna matatizo na dini ya mtu bali masheikh hawa na wafuasi wao wenye kutaka kulifungamanisha suala hili la DPW na uislamu.
Ningependa ulielewe hili Ili tusiwe tunalirudia rudia maana liko wazi mno ndugu yangu. Beberu akiliita "trivial". Ambayo ni sawa sawa na sifuri kujumlisha namba au namba kuzidisha na moja.
Tafadhali kama majadiliano haya Yana umhuhimu wowote kwako pia, tujadiliane tukishawishiana kwa hoja.
Hoja haikimbiwi wala kupiga kwa rungu. Siyo kwa kurukia rukia mambo bila msingi wowote. Huo ndiyo ulio uungwana ndugu yangu.
.
Hii inatia moyo. Hata hivyo ni muhimu kutambua ninachoandika hapa si tu kile ambacho zawadini ana tatizo nacho. Nijulie wapi vyote usivyo na matatizo navyo Ili nisiviweke hapa? Au nijueje vyote ulivyo na matatizo navyo ili tu kuwa ndivyo niviweke hapa?
Kauli yako hii ya tofauti za kusema na kutenda nilishakufahamisha ni potofu. Wewe si malaika. Hapa pia nilikwambia kusema hutangulia kutenda. Hapa tunaandika kwa maana ya kuongea. Tunayoyaandika ndiyo tunayoyaamini, tunayoyasema na kuyatenda. Wewe ni nani kuyahoji tuyasemayo kuwa labda hatutayatenda ndugu?
Ileje, mimi, si kuwa tuko peke yetu. Hata kina Prof. Shivji waislam hao, nao ni wenzetu.
Nimesema mara nyingi tatizo letu si masheikh wala waislam bali masheikh uchwara hawa na wafuasi wao. Mbaya zaidi wakiutumia uislam kuwachafua waislam, waislam wenyewe wakiwa wameufyata vilivyo.
Wabaya wetu nilisha kufahamisha wazi wazi na "link" nikakupa na "like" ukanipa.
Ninaiweka tena hapa kukupa nafasi nyingine ya kujikumbusha nayo kwa raha zako:
Tuwatambue wanaohaha kutusambaratisha kama Taifa
Ninao uhakika sijakuuliza lolote zaidi ya mara moja popote, kama jibu lako limekuwa toshelevu. Ndiyo maana nimelazimika kutumia neno
labda kiungwana kila nilipokuwa sina jibu lako la moja kwa moja kwenye lolote ili kufanikisha kuweza kupiga hatua.
"Izingatiwe kama ulivyo wewe hata miye siko nao muda mwingi kiasi hicho, wa kupoteza kwenye jambo au mambo yenye kurudiwa rudiwa pasipokuwa na ulazima wala tija."
Kwamba labda uliulizwa zaidi ya mara moja? Basi tambua jibu lako halikuwa wazi wala kujitosheleza kuweza kuona sehemu hiyo imeeleweka.
Wewe labda useme hapa unakubaliana na Maaskofu wa TEC maana hao ndiyo wanaosema ulicho summarize hapo juu. Summary hiyo ndiyo yetu sisi sote wa aina ya kina ileje na wote wenye kuwashangaa hao masheikh na wafuasi wao bila exception.
Masheikh hawa na wafuasi wao hakuna wanaposema, kutamka au kuashiria vifungu au vipengele vyovyote vya mkataba huu.
Nimekupa clips mbili au hapa nikuongeze nq nyingine zaidi?
"Nionyeshe wapi wanatamka neno kipengele cha mkataba."
Masheikh hawa na wafuasi wao wanasema udini, ukristo, uislam, nk. Wamejaa Shari dhidi ya TEC na dhidi ya wakristo au yeyote mwenye kuupinga mkataba huu au kuwa na mawazo tofauti na wao.
Ndiyo maana sisi wengine bila kujali dini wala itikadi zetu, tunajiuliza kulikoni ndugu zetu hawa na kupagawa huku?
Hali kadhalika na wewe kama uko nao, au kumbe uko nao tunajiuliza kulikoni ndugu yetu huyu suala hili lisilowahusu waislamu au masheikh mbona kutaka kutuletea uchuro wao ya Rabi?
Kwamba labda wewe ni au si mmoja wapo ndiyo maana nikakualika kistaarabu tujuzane labda tukawaelewa?
Lau wewe si mmoja wao tusaidiane kuwaelewesha kwani kwa mawazo yetu wengine, hawa ndugu kwa wanakoelekea wamepotoka kukubwa (big time).
Kufikia hapa nikadhani niupanue uwanja kwa kuwaita ndugu wastaarabu wengine ili kuwa sehemu ya mjadala huu japo kwa taarifa ikiwapendeza. Hii ikizingatiwa, hii nchi ni yetu sote na hasa kama ungali ukikaza ubongo kama masheikh hayo.
Cc:
Pascal Mayalla,
Elli,
tpaul,
Ileje,
denooJ na ndugu wapambanaji wengine.