Waraka wa TEC wajadiliwa TV IMAAN
Kwa nini masheikh wamechafukwa hivi na waraka huu dhidi ya mkataba wa Bandari?

Kwamba:

"Wasitufanye kama foreigners katika nchi hii.

Wametoa waraka umeaomwa makanisani na sisi tutoe waraka usomwe misikitini."

View attachment 2725266

Kwani waraka wa TEC ni dhidi ya masheikh au ni dhidi ya waislam?

Kwani masheikh ndiyo wenye mkataba huu?

Au hawa ndugu zetu na jazba hizi ni kwa maslahi ya nani?
🤣🤣🤣!! Mkataba wenyew Wameusoma basi 🤣🤣
 
Walimpinga kwenye suala lipi?hebu nikumbush
Magufuli mkristo alipingwa na kukosolewa na Maaskofu hawa hawa na hakuna aliyesema ni udini..
 
Hivi shida iko wapi? Waislamu wanataka kufanya kama vile mvutano ni wa waislamu vs wakristu, wakati wakristu wenyewe wana madhehebu mengi na kila moja lina msimamo wake!
Sidhani kama ni msimamo wa BAKWATA na ndiyo sababu wengi wa wanao bwabwaja ni mashehe ubwabwa ambao hawajui nini kinajadiliwa!
 
Kwa hiyo kumbe mnatega Rais kwenye vita vya kidini. Sasa hamfai nyie au hafai Samia?

Kama Mkristo na Mkatoliki nasema hapa rasmi. Nitampigia kampeni Samia awe Rais 2025- 2030.

Kumbe ndo maujinga mnayoyafanya eeeh!! Tumewashtukia
Uislamu ima Ukristo Haukuingia Mkataba na dpw!
Ilaha watu ndio walioingia Mkataba....
 
Hapa Naona Watu wapo tayari kufumba macho na kufunika kombe kisa jamaa ni Ndugu katika Imani.

Hakuna imani inabariki wezi hata kama DP world ingekua inatokea Vatkan.

Kimsingi Mimi nawaelewa Tec wamekua wakweli na wamesimama Upande wa Wananchi.

Hapa SERIKALI ina wajibika kwa Wananchi walio ipa Ridhaa ya kuwaongoza na kusimamia Rathilimali zao.

Najua MH Rais ni MTU msikivu na Muungwana kabisa. Uwenda kuna wasaidizi wake Walitaka kumtengenezea Ajali ya kisiasa kwenye sakata hili la Bandari.

Turudi kama Taifa tukae pamoja na kukubaliana katika mambo ya Msingi hasa jinsi ya kuzilinda Rathilimali zetu.

Mungu Hakutupa Rathilimali Mali hizi kwa baati Mbaya Bali Alitupa zitubadilishie hali zetu za Uchumi kama Watanzania.

Tunaelekea miaka 65 ya Uhuru kweli nchi tulizokuwa nazo sawa kiuchumi wakati tunapata Uhuru Leo zimekua dunia ya kwanza??? Kweli tuna hitaji kukanyaga Mafuta ya Upako na hii inasababishwa na usimamizi mbovu wa baadhi ya viongozi walio Aminiwa kuongoza kwenye kila sekta.

Nimalizie kwa kusema MH Rais Tunajua nia Yako Njema na Jitihada zako kutafuta wawekezaji katika taifa letu. Kuwa macho sana na baadhi ya wasaidizi wako Ambao wanatanguliza matumbo yao Badala ya kulifikiria taifa letu na Kukusaidia kutimiza Azima yako nzuri ya kutuletea maendeleo.
 
Kwa hiyo bakwata wanaamini sisi hatujui kuwa hawako huru?? Dharau hii.tunaaamini mahubir yao lakin sio uhuru wao wa maoni huo muda watumie kuhubir uislamu siasa hawawez
 
Wako biased na hatred, subjective in short their judgements are coloured by religion perspective,Kuna kitu kinaitwa cognitive dissonance nadhani wachache watanielewa hili Mana wengi tunasomaga umbeya na tiktok nikiwemo namie
 
Zawadini tusaidiane kupeana majibu. Nchi ni yetu sote tusifike mahali tukafarakanishwa kijinga.
Mkuu Ileje alikuwa anajadili maoni yako namba 474. Akataka atueleze waislamu wanafaidika nini na mkataba wa DP.

Kwanza Ileje na sisi sote tuelewe kwamba kwa sasa hakuna mtu anayefaidika na mkataba wa DP kwasababu haujatekelzwa. Hili linajulikana na kila mtu hata sisi wa marasa, chambilecho akina nyie, seuze Ileje ambaye si wa madrasa. Na hapa nikapata swali nikajiuliza mwenyewe - huna haja ya kujibu hili kwani najiuliza mwenyewe, hivi hata wale wanaojinasibu wameenda shule kumbe nao ni ignorants. Nimetumia hili neno la kigeni kwani ningelisema kwa lugha yetu mtu anaweza kutafsiri kuwa ni tusi.

Sasa nirudi kwenye ombi lako kutaka nisaidie kujibu. Jibu langu ni hili:
Hakuna MTANZANIA yeyote, awe mwislamu, mkristo au mpagani, kwani mkataba haujatekezwa.

Hapa tunapaswa kujadili ni faida au hasara gani zitapatikana wakati mkataba utapotekelezwa

Tafadhali mwambie Ileje kwamba mkataba haujatekelezwa, na hata ungekuwa umanza kutekelezwa bado ni mapema. Huenda wewe atakuelewa kwani wewe hukuenda mdrasa kama mimi na dadaangu FF.
 
Bwana Zawadini tambua faida na hasara za mkataba wowote siyo hadi utekelezwe. Kusuburia kufikia utekelezaji kama ulivyo huu itakuwa tayari tumeshachelewa mno.

Ulisikia mkataba huu hauna ukomo?

Hapo ndipo zile kazi za wanazuoni nguli kweli kweli wa aina za kina:

Prof. Shivji, Prof. Kabudi, Prof. Sifuni Machone, Prof. Ibrahim Juma, Dkt. Tulia, Dkt. Ndumbaro, Dkt. Rugemeleza Nshala, Dkt. Slaa, Dkt. Asha-rose Migiro, na wa namna hiyo wanapokuja kazini.

Zingatia siyo kina Prof. Janabi, Prof. Lipumba, Prof. Ndalichako, Prof. Assad, Prof. Mkenda, Prof. Mbarawa, Prof. Mkenda, Dkt. Msukuma, Dkt. Tale Tale, Prof. Jay, Dkt. Remmy, wala Prof. Maji Marefu. Hawa Wana makwao si kwenye mikataba.

Nadhani title hizo waziona mwenyewe ndugu.

"Joni nikuombe ulinzi japo wa green guard hapa kwa muda."

Hata hivyo wanasema wavumao baharini siyo papa peke yao bali na wengine wapo.

Kuna na timu hii nayo si ya kubeza hata kIdogo:

Tundu Lissu, Peter Kibatala, Dickson Matata, John Malya, Meabukusi, Robert Kidando nk.

Hawa hapa wote hao wana ki kobendera cha "usomi" kabla ya majina yao.

Amini nakwambia hata Paskali tukiamini ni mwenzao Kumbe hana hamu! Kwa mshangao wa wengi pamoja na kuvuta tuzo JF ya unguli huo, kupisha shari kachagua kujifungamanisha na kina aina za kina Farouk Karim, Charles Hilary, au kina Zuhura Yunus.

Sembuse wewe na mimi au hawa hapa chini ndugu yangu?

Naona Waraka Sasa umefika Kila pahala, haujamuacha MTU salama! Naam wanaushambulia Kwa hakika though hakuna tangible points hapa!

Masheikh hawa wanaamini Waraka wa TEC utaleta taharuki. Wanafanya reference ya mambo ya ESCROW.

Wanasema tamko la TEC linataka kuleta taharuki Kwa wananchi na chuki Kwa wananchi dhidi ya serikali ya CCM.
Hivi kwa nini wasionyeshe kwenye hivyo vipengele TEC walivyoviongelea ni kipengele kipi 1) "ni kuchanganya dini na siasa" na kipengele kipi 2) "kitaleta taharuki"? One cannot make a claim without justification. Any claim must be justified. Huo ndio usomi ati.
 
Bwana Zawadini tambua faida na hasara za mkataba wowote siyo hadi utekelezwe. Kusuburia kufikia utekelezaji kama ulivyo huu itakuwa tayari tumeshachelewa mno.

Ulisikia mkataba huu hauna ukomo?

Hapo ndipo zile kazi za wanazuoni nguli kweli kweli wa aina za kina:

Prof. Shivji, Prof. Kabudi, Prof. Sifuni Machone, Prof. Ibrahim Juma, Dkt. Tulia, Dkt. Ndumbaro, Dkt. Rugemeleza Nshala, Dkt. Slaa, Dkt. Asha-rose Migiro, na wa namna hiyo wanapokuja kazini.

Zingatia siyo kina Prof. Janabi, Prof. Lipumba, Prof. Ndalichako, Prof. Assad, Prof. Mkenda, Prof. Mbarawa, Prof. Mkenda, Dkt. Msukuma, Dkt. Tale Tale, Prof. Jay, Dkt. Remmy, wala Prof. Maji Marefu. Hawa Wana makwao si kwenye mikataba.

Nadhani title hizo waziona mwenyewe ndugu.

"Joni nikuombe ul
 
Bwana @Zawadini tambua faida na hasara za mkataba wowote siyo hadi utekelezwe. Kusuburia kufikia utekelezaji kama ulivyo huu itakuwa tayari tumeshachelewa mno.
Mara nyingi huwa unaruka niliyoandika na kuja na mingine ambayo wala sijayagusa. Sina hakika kwamba ni makusudi au ni bahati mbaya. Nilikuwa najadili kauli hii ya Ileje ambayo wewe ulinitag.
"Atueleze waislam mnanufaika vipi na mkataba baina ya Tanzania na Dubai?"

Hapo kuna neno MUNANUFAIKA ambalo ni la wakati wa sasa. Ukimwambia mtu ananufaika kwa kitu ambacho hakijatekelezwa itakuwa ama hujui unachozungumza au unababaisha. Chochote kati ya hivyo viwili si sahihi.

Nilitarajia kwenye mjadala uzungumzie hili kwanza kwani ndo hoja iliyotolewa. Hayo mengine ni baada ya hili.

Naamua kusita hapq kwani sitakuwa nakutendea haki kujadili kitu ambacho kimsingi hakijagusiwa na kwa hivyo hakipo.

Zawadini
 
Nikutaarifu kwa dhati yangu hakuna ninachojaribu kuruka popote hata ni kwa sababu ipi basi?

"Atueleze waislam mnanufaika vipi na mkataba baina ya Tanzania na Dubai?"

Nielewe hoja yako ni hiyo. Yaani kutokea kwa bwana Ileje mwenyewe:

IMG_20230823_120842.jpg

Zingatia hoja ya Ileje inafuatia hoja yangu. Ndiyo maana nawe nokakualika tumsaidie sheikh asiyekuwapo JF, kujibu kiungwana.

Labda tuanze kwa kujiridhisha kama unauona mlolongo huo.

Pili unaona Ileje ambaye anaweza kuwa na dini yoyote, yeye au hata miye, hakumlenga muislam yeyote bali sheikh yule kama nilivyokuwa nimemnukuu mimi kwa clip yake?

Hudhani tuanzie hapo ndugu? Kwamba mlengwa wa hoja alikuwa nani?

Kisha tujikite kumsaidia Sheikh kuyajibu maswali ya bwana Ileje ambayo nayo ni matatu tu, moja baada ya jingine.

Zingatia hapa isije ikawa twaruka hoja kujifanya wakristo au waislam zaidi nje ya hoja.

Tunakubaliana na utaratibu huu ndugu?
 
Tunaoelekea sio pazuri. Tungerudi kwenye msingi wa mkataba na kujadili vipengele vyake.
 
Nikutaarifu kwa dhati yangu hakuna ninachojaribu kuruka popote hata ni kwa sababu ipi basi?

"Atueleze waislam mnanufaika vipi na mkataba baina ya Tanzania na Dubai?"

Nielewe hoja yako ni hiyo. Yaani kutikea kwa bwana Ileje mwenyewe:

View attachment 2726014

Zingatia hoja ya Ileje inafuatia hoja yangu. Ndiyo maana nawe nokakualika tumsaidie sheikh asiyekuwapo JF, kujibu kiungwana.

Labda tuanze kwa kujiridhisha kama unauona mlolongo huo.

Pili unaona Ileje ambaye anaweza kuwa na dini yoyote, yeye au hata miye? Hakumlenga muislam yeyote bali sheikh yule kama nilivyokuwa nimemnukuu Mimi kwa clip yake.

Hudhani tuanzie hapo ndugu? Kwamba mlengwa wa hoja alikuwa nani?

Kisha tujikite kumsaidia Sheikh kuyajibu maswali ya bwana Ileje ambayo nayo ni matatu tu, moja baada ya jingine.

Zingatia hapa isije ikawa twaruka hoja kujifanya wakristo au waislam zaidi nje ya hoja.

Tunakubaliana na utaratibu huu ndugu?
Mosi: Mkuu; nakubalana na utaratibu uliopendekeza.

Pili: Kwa kuwa swali la kwanza nimelijadili kwa kina, naomba nijikite na maswali mawili yaliyobakia.

Waraka sikuusoma, kwani nilimsikiliza askofu aliyewasilsha. Sikuusoma kwasababu niliamini askofu anawasilisha waraka na hivyo hatoi maneno yake. Ikiwa ni hivyo, sikumsikia askofu akitaja waislamu. Si hilo tu, sikumsikia askofu akikejeli, kutukana wala kusema au kushawishi kuundoa uongozi uliopo. Sasa kinachonishangaza ni kuingizwa waumini wa dini; na hili, kwa maoni yangu, halikustahili.

Ama kuhusu swali la je DPW ni uislamu, mimi ninavyojua hiyo ni taasisi au shirika la serikali linaloshughulika na bandari na ambalo lipo Dubai. Imesadifu kuwa Dubai ni nchi/eneo linalo/inayokaliwa na Waislamu walio wengi, na hivyo halna uhusiano na dini kwani si shirika la dini wala di taasisi ya dini, na hapa napo linakuja tena swali, kwanini lihusishwe na dini.

Baada ya maoni hayo, huenda angalau nitakuwa nimejadili na pengine kujibu yale maswali matatu. Karibu sana Mkuu.
 
Back
Top Bottom