Sheikh Mussa Juma amesema Wapinzani na Maaskofu wanaomsaka Rais Samia Suluhu Hassan hawana shukrani wanaendekeza Udini na maslahi yao binafsi nakusahau hisani waliyowafanyia kipindi walipokuwa hawana kitu.
Akizungumza huko visiwani Zanzibar katika mawaidha Sheikh Mussa Juma amesema Rais Samia ni kiongozi wenye huruma na uadilifu ndani yake hivyo wanaomsakama wanafanya hivyo kwa maslahi yao binafsi.
"Hapa kwetu ndio kabisa madudu haya ya kisiasa sijui wakina Mbowe kina Lissu waliyoyaficha ndani ya mioyo yao yalikuwa ni makubwa zaidi kuliko wanayoyadhihirisha, angalia sasa hivi wanavyotapika maneno yale angalia ni udini tu ule, kama huyo Dkt. Slaa yeye ndio kamaliza mchezo mmemsikia mwenyewe Udini tu ule hakuna kitu kingine Udini tu..sasa yale ndio yaliyokuwa yamejificha hawana shukrani hata kidogo" alisema
Sheikh Mussa Juma amesema Rais Samia ni mtu mwenye imani wanaomuanda wanapaswa kumshukuru na kumheshimu kutokana nakuwafanyia hisani kwa kuwarejeshea vitu vyao walivyopoteza kipindi cha awamu ya Tano.
"Alikuwepo Magufuli kawanyongesha watu, kawaadhibu watu, kawatesa watu hawana hatia wamenyamaza kimya, Mwenyezi Mungu kafanya Rehema zake katuletea mtu ana imani watu wanaishi kwa raha , watu wanapendana, wanasaidiana, mnyonge anasaidiwa leo hawa wakina Mbowe, Lissu hawana Shukrani mtu kama huyo alowafanyia hisani kama huyu Lissu alipofanyiwa mambo mazito mtu wa kwanza kwenda kumtizama ni Rais Samia wale waliobakia wote maaskofu ambao sasa hivi ndio wanamtukana Samia kwa sababu ya uislamu hakuna kingine na maslahi yao waliyokuwa wanaipata kwenye ile bandari wanamsaka hawana shukrani wote hao maaskofu walikuwa wameufyata wanamuogopa Magufuli , lakini tazama alichomfanya Rais Samia kamlipa kila kitu chake kamrejeshea ambavyo alikuwa kanyang'anywa na huyo Mbowe hivyo hivyo kila kitu chake karejeshewa kalipwa pesa chungu mzima ambazo zingewasaidia wananchi , Rais Samia anaonyesha huruma kwa rai wake alafu hawa wanakuja juu wanamtukana na kumkashifu kwa maslahi yetu wenyewe sisi wananchi lakini kwa sababu wao kuna maslahi yao ya dini pale wanahisi atakuja kuondoka , pamoja na maslahi yao walikuwa wanapitisha vitu pale...." alisema Sheikh huyo
Pamoja na yote Sheikh Mussa dunia ilipofikia sasa mambo mema yanaonekana mabaya huku mabaya yakionekana mema hata hivyo amemuomba Rais Samia aendelee kuishi maisha marefu kutokana na uadilifu na huruma alionao katika uongozi wake.
"Mbona mambo sasa hivi yanaanza kuchimbuka yaliyokuwa yamejificha na sisi ndio tunayasubiri kwa hamu kwa sababu tulipokuwa tunasema nyinyi mlituona sisi wabaya lakini sasa hivi Mwenyezi Mungu anayachimbua, mmemsikia Slaa alivyosema nyie waislamu mmekaa tu mmemsikia na uislamu wenu mnasikia wanavyomfanyia muislamu mwenzenu wanavyomwandama, wanaranda kwenye mikoa kwa kutumia pesa hizi hizi wanazopewa zetu wenyewe kama rai wanamsakama Mhe. Rais Samia lakini Mwenyezi Mungu atamuhifadhi, atamlinda na shari zao ataendeleza uadilifu, ni Rais pekee aliyekuwa hana mfano na waliyokuwa wamepita mwenye huruma mpaka na vilema tunamuombea dua na tutazidi kumuombea sasa kama wewe unanuna nuna"_ Sheikh Mussa Juma akizungumza msikitini Zanzibar