Uchaguzi 2020 Waraka wa Uchaguzi wa Shura ya Maimamu Tanzania

Uchaguzi 2020 Waraka wa Uchaguzi wa Shura ya Maimamu Tanzania

Status
Not open for further replies.
Titi...
Huwezi kufananisha historia ya Waislam na kundi lolote labda ikiwa unataka kuchekesha watu.

Unaweza kuanza kujifunza kwa kusoma kitabu cha Abdul Sykes (1998).
Kwa hivyo hapo kwenye hoja ya usawa katika kugawana nyadhifa na mengineyo inahusu raia walio muhimu au bora kuliko wengine?

Mimi niliwaelewa vibaya nilidhani wanataka usawa kwa raia wote toka kila kundi la kiimani.
NB: Kutoamini kuhusu dini na Mungu/Miungu nayo ni imani pia. Kuamini katika miungu au mungu zaidi ya mmoja nayo ni imani pia.
 
Teuzi na upandishwaji vyeo lazima vifanyike kwa kuangalia sifa na vigezo vya mtu husika.
Lazima viwe 'based on merits' siyo sifa ya udini au ukabila.
Waislamu wana hiden motives (agenda) na teuzi na nafasi zote za uongozi, ndio maana huzipigania sana...kwao limekuwa swala la kufa na kupona
 
Kwa hivyo hapo kwenye hoja ya usawa katika kugawana nyadhifa na mengineyo inahusu raia walio muhimu au bora kuliko wengine?

Mimi niliwaelewa vibaya nilidhani wanatka usawa kwa raia wote toka kila kundi la kiimani.
NB: Kutoamini kuhusu dini na Mungu/Miungu nayo ni imani pia. Kuamini katika miungu au mungu zaidi ya mmoja nayo ni imani pia.
Titi...
Tanzania dini kuu ni mbili na unazijua.

Ili ufahamu imekuwaje leo dini imekuwa ni mada ya kujadiliwa inakubidi uisome historia kudai uhuru wa Tanganyika.

Bila ya kufanya hivyo hutoweza kuchangia vyema mjadala huu.
 
Kuna mengi nakubaliana na waraka huu ila hili la kuangalia na kumlazimisha kuwa mtanzania huyu ni wa dini hii au ile hilo lina utata.

Kugawana keki ya taifa n.k kungetumia kikokotoo cha kanda maana kutumia imani bado imani fulani itazidiwa wingi na kuleta mgawanyiko ktk taifa, jamii na familia ila kuangazia kanda inafuta mgawanyiko kwa kufuata imani.
UjuIla makala ndefu jamani,ebu tuendelee kuidadavua.
 
Titi...
Tanzania dini kuu ni mbili na unazijua.

Ili ufahamu imekuwaje leo dini imekuwa ni mada ya kujadiliwa inakubidi uisome historia kudai uhuru wa Tanganyika.

Bila ya kufanya hivyo hutoweza kuchangia vyema mjadala huu.
Utanisamehe mzee wangu, mimi nilielewa vibaya kwamba maimamu wanadai haki sawa kwa raia wote kumbe siyo lengo lao kama nilivyodhania.
Wao wanadai haki za waislam na wakristo tu ziwe sawa ila hao wengine hawastahili haki sawa sababu ya ushiriki wao katika kudai uhuru au sababu ya uchache wao.

Hapo kwenye uchache wao bado pana nitatiza sababu hata sasa huenda kati ya waislam na wakristo kuna kundi moja hapo wapo wachache kuliko wengine hivyo hawastahili kulingana ila wanaweza kuteuliwa kwa uwiano wa idadi.

Usinichoke, nielekeze tu.
Natanguliza shukrani Sheikh.
 
Lakini haya ni maoni yako mkuu wangu.
Ngoja tuwasikilize wenyewe, naomba ufafanuzi zaidi toka kwa Mzee wangu Mohamed Said .
Ndo ukweli huo

Waislamu wana njama zao juu ya taifa hili....kama ni shughuli za kufanya zipo kibao

Wao ni teuzi tuu....

1960s wao ni teuzi, 1970s wao ni teuzi, 1980s wao ni teuzi, 1990s wao ni teuzi, 2000 hadi leo 2020 wao ni teuzi
 
Hao hawatusemei waislamu wote.....hao Wala hawatambuliki KISHERIA kutusemea....

Muislam Mimi SIYATAKI HAYO WAYASEMAYO.....
Muislam mimi na wenzangu tulio wengi tunataka kuiona tume HIIHII iendelee kwani iko KISHERIA na haina dosari zozote.......

Waislam tunasemewa na BARAZA letu kuu BAKWATA......

WENGINE WANAKUWAGA WALE WACHOCHEZI WACHACHE.
Mkuu
Ninamashaka Sana na uislam wako.. Yumkini nyama huli ila Wakula ndizi.. Natumai umenielewa
 
Titi...
Tanzania dini kuu ni mbili na unazijua.

Ili ufahamu imekuwaje leo dini imekuwa ni mada ya kujadiliwa inakubidi uisome historia kudai uhuru wa Tanganyika.

Bila ya kufanya hivyo hutoweza kuchangia vyema mjadala huu.
Hivi huo UKUU wa dini mbili unazo zizungumzia ni wa namna gani?
Kigezo kipi umetumia kusema hizi ni kuu?

Kama kigezo ni idadi yao basi nasikitishwa na kustushwa na mitizamo ya kudai kupewa haki katika taifa kwa kuangalia makundi ya waliyo wengi tu na kuachwa au kupuuzwa makundi ya wale waliyo wachache.
 
Hapo Siro kapata kisingizio, yaani watu wakitaka haki zao yeye anaita uhalifu...polis wetu wameacha kazi yao ya msingi
 
Jumbe Brown,
LOoo, mkuu 'Jumbe Brown', huko nyuma kwenye michango yako mingine nilikuchukulia kama mtu 'serious', sasa hii hapa ni nini mkuu?

Tusibishane, nimeweka tu haya ili ujue nilivyoheshimu michango yako huko nyuma.
 
Mkuu
Ninamashaka Sana na uislam wako.. Yumkini nyama huli ila Wakula ndizi.. Natumai umenielewa

Una UHURU huo kwani TAQWA iko moyoni.

Sidhani km Kuna haja ya kupimwa uislam wangu na BINADAMU ama muumini mwenzangu as nyuma yangu nina RAQQIB na ATTID wanantosha ✍✍✍.

Allahu a'alam.
 
Hivi huo UKUU wa dini mbili unazo zizungumzia ni wa namna gani?
Kigezo kipi umetumia kusema hizi ni kuu?

Kama kigezo ni idadi yao basi nasikitishwa na kustushwa na mitizamo ya kudai kupewa haki katika taifa kwa kuangalia makundi ya waliyo wengi tu na kuachwa au kupuuzwa makundi ya wale waliyo wachache.
Titicomb,
Muda wa kusomesha haya yote hapa sina ninachoweza kufanya ikiwa nia yako ni kujua hili somo ni mimi kukupa rejea za kusoma taratibu.
 
Lakini haya ni maoni yako mkuu wangu.
Ngoja tuwasikilize wenyewe, naomba ufafanuzi zaidi toka kwa Mzee wangu Mohamed Said .
Titicomb,
Tuwe na subira tuwape muda waliokusudiwa waraka huu wausome huenda wakaja na majibu.

Mimi si wa kujibu yale walioelekezewa wenye kutakiwa kujibu.

Nitajibu kama nani?
 
LOoo, mkuu 'Jumbe Brown', huko nyuma kwenye michango yako mingine nilikuchukulia kama mtu 'serious', sasa hii hapa ni nini mkuu?

Tusibishane, nimeweka tu haya ili ujue nilivyoheshimu michango yako huko nyuma.

Nakuheshimu mkuu Kalamu Wala hatubishani AKHI.

Mkuu wangu haya Mambo yanahitaji tafakuri Pana.

Watu huwa ngumu kukubali kutokubaliana kwa sababu yanagusa HISIA za kiimani na kama ujuavyo MITIZAMO ya kiimani na makundi ya kiimani yanagusa MIOYO YA WATU ambao wamekuwa wakiyasikia hayo kila uchao.

Tuendelee kukubali kutokubaliana Kaka.

Thanks Indeed
 
Shura ya Maimamu hawatambuliki nchini, ni BAKWATA tu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom