WARAKA wenye kurasa 18 kuhusu uchaguzi mkuu, umetolewa na Jumuiya na Taasisi za Kiislam ukisisitiza mambo muhimu ikiwemo Tume Huru ya Uchaguzi.
“Kwa hakika maelezo yetu ya nini tunataka kwa taifa letu katika uchaguzi huu, yangekuwa na maana sana kama Taifa lingekuwa na Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Tume Huru ya Uchaguzi, vinavyotokana na Wananchi wenyewe,” amesema Sheikh Ponda.
Hata hivyo, Sheikh Ponda amesema kama Tume Huru ya Uchaguzi haitapatikana na kwa kuwa, serikali imeahidi kuhakikisha uchaguzi huo unakuwa huru na wa haki, inatakiwa ifanyie maboresho kanuni za uchaguzi na za uendeshaji zoezi la uchaguzi.
Amesema, ni matamano ya Waislamu kuona Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), zitunge kanuni zitakazoendana na wakati uliopo...