Warembo wangu, upo tayari kufunga ndoa bila sherehe?

Warembo wangu, upo tayari kufunga ndoa bila sherehe?

Extrovert

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2016
Posts
70,785
Reaction score
186,690
Wote tunafahamu kuwa suala la ndoa ni jambo la heshima na baraka katika misingi ya kijamii na kiimani.

Swala la kufanya ndoa kama sherehe kubwa liko katika maamuzi na mapenzi ya wanandoa wenyewe japo linaweza chagizwa na wazazi ama walezi pia.

Leo nataka nipate tathmini kutoka kwa wachumba esp. wadada je, wewe upo tayari kufunga ndoa bila kuinvolve sherehe?

1622189722619.png

Nini sherehe, hivi hakuna uwezekano wowote hiyo ndoa tuifungie tu kabisa ndani, mfungisha ndoa akimaliza tumfungulie mlango atoke, halafu sisi tuanze zetu maisha mapya ya ndoa?? 😂
Kaka madenge popote pale ulipo mruhusu muweka hazina amnunulie soda ya baridi huyu dada pia leo akae siti ya mbele kwenye daladala😆😆
 
Kama hali ya uchumi hairuhusu Kwanini niendelee kushupaza shingo yangu ngumu kwa kung’ang’ania sherehe.kwanza ni gharama sana.hiyo pesa si bora tuifanyie uwekezaji ambapo itaongeza kipato.

Wanandoa wengi sana huishi maisha ya stress baada ya kufanya harusi.

Ingewezekana kufunga ndoa na kuendelea kupiga kazi ingekuwa mzuka sana.
 
Kama hali ya uchumi hairuhusu Kwanini niendelee kushupaza shingo yangu ngumu kwa kung’ang’ania sherehe.kwanza ni gharama sana.hiyo pesa si bora tuifanyie uwekezaji ambapo itaongeza kipato.

wanandoa wengi sana huishi maisha ya stress baada ya kufanya harusi.

Ingewezekana kufunga ndoa na kuendelea kupiga kazi ingekuwa mzuka sana.
Uwezekano upo ila je upo tayari, maana swala la sherehe wenye influence zaidi ni wanawake...Atataka awatambie mashoga zake kuwa kaolewa auze sura kwa MC GaraB ndio aone kaolewa.
 
Uwezekano upo ila je upo tayari, maana swala la sherehe wenye influence zaidi ni wanawake...Atataka awatambie mashoga zake kuwa kaolewa auze sura kwa MC GaraB ndio aone kaolewa.
Niko Tayari bila kupepesa macho, achague yeye sasa.. tukitoka kufunga ndoa twende kazini au twenzetu home tukapige game
 
Hakuna tena heshima ya ndoa. Siku hizi watu wanaanza kubanduana na kuishi kama wapo kwenye ndoa, wanafanya ya kwenye ndoa kabla ya ndoa.

Ndoa yenye heshima ni ile tu ambayo ambayo wahusika wanakuwa hawajabanduana, hao pekee ndio wana stahili hata sherehe, ila hao wengine wapige kimya kimya tu
 
Ukweli ni kwamba kama uwezo upo Ndoa na Sherehe inapendeza sana maana ni tukio muhimu sana katika maisha ya mwanadamu lakini kama uwezo hauruhusu hamna haja ya sherehe, ndoa ni muhimu lakini sherehe siyo muhimu.
[emoji106]
 
Back
Top Bottom