Warembo wangu, upo tayari kufunga ndoa bila sherehe?

Warembo wangu, upo tayari kufunga ndoa bila sherehe?

Sherehe baada ya ndoa ni anasa zisizo na ulazima.... binafsi napendelea ndoa simple tu... wawepo mashahidi na wazazi/ walezi inatosha. Na kama tutakuwa na pesa kidogo tutatoa sadaka kwa Yatima kwa ajili ya kumshukuru Mungu kutuvusha salama.

Kwa research yangu fupi ni kwamba ndoa nyingi zilizokusanya watu kwa sherehe kubwa huwaga hazidumu maana zinakuwa zimegubikwa na showoff na maigizo yaliyokosa Upendo ndani yake, kazi yao kubwa huwaga ni kufurahisha watu ili waonekane hawajafulia.....! Ngoja niishie hapo.
 
Kuna uhusiano wowote kati ya avatar yako na wewe?
 
Enzi zile kulikuwa na kesi nyingi za maharusi kusepa na pesa za mchango, nina uhakika sababu ilikuwa ni hiyohiyo, eti mtu unashuhudia kabisa ndugu wakichangishana mamilioni na mamilioni kwa ajili ya kutumika usiku mmoja tu, then after wanawaacha mnarudi kwenye vivyumba vyenu, umepandishwa gari ya gharama, hujawahi ipanda na hujui kama utakuja panda tena mpaka kufa kwako.. Yaani ni ufeki feki tuu
 
Yaani katika vitu sijawahi waza maishani ni ndoa yenye sherehe yaani kiujumla mimi sipendi sherehe. Nikienda kwenye sherehe najikaza tu kwasababu ni familia au jirani sio vizuri muda mwingine kujitenga. Mimi napenda ndoa isiyo na mbwembwe as long as nimemridhia niliye naye.

Pia huwa naona sherehe ni kutafuta stress plus usumbufu kwa familia especially wazazi na kwangu pia so sitaki hizo hekaheka mie. Kuna watu watakuja kusema labda huwa sio mtoaji ktk shughuli za watu wengine hivyo labda naogopa na yangu itadoda, familia yangu ni wachangiaji wazuri tu sema ndio hivyo, naona ni kausumbufu fulani kasiko na maana.

Kingine ile shughuli ya kukumbusha mtu achange siku zimeisha siiwezi kabisaa naona kama inakuwa kulazishana sasa kwanini niteseke na kitu kisicho na ulazima kwangu.
 
Kama hivi sio?
 
Attachments

  • IMG_20210222_124204_413.jpg
    IMG_20210222_124204_413.jpg
    104.7 KB · Views: 9
Mie natamani ndoa ya kimya kimya, kwa kifupi sipendi shughuli hata graduation zenyewe nakimbiaga 😀😀
Sasa suala la ndoa ukiwaambia ndoa itakua ya kimya kimya unaambiwa kwani umekua msiba huo
sijui kikombe hiki nitakiepuka vipi?
 
Nini sherehe, hivi hakuna uwezekano wowote hiyo ndoa tuifungie tu kabisa ndani, mfungisha ndoa akimaliza tumfungulie mlango atoke, halafu sisi tuanze zetu maisha mapya ya ndoa?? [emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23]napata wasiwasi kuamini kama hii comment imeandikwa na mdada.....wanawake wengi ninaokutana nao au ninaokuwa nao kwenye mahusiano huwa wanatamani harusi na sio ndoa....yaani anakuwa anapata picha namna atavyovaa shela e.t.c kama ulichondika ni kweli basi wewe ni mwanamke wa aina yako peke yako....
 
Back
Top Bottom