Warembo wangu, upo tayari kufunga ndoa bila sherehe?

Warembo wangu, upo tayari kufunga ndoa bila sherehe?

Wote tunafahamu kuwa swala la ndoa ni jambo la heshima na baraka katika misingi ya kijamii na kiimani.

Swala la kufanya ndoa kama sherehe kubwa liko katika maamuzi na mapenzi ya wanandoa wenyewe japo linaweza chagizwa na wazazi ama walezi pia.

Leo nataka nipate tathmini kutoka kwa wachumba esp. wadada je, wewe upo tayari kufunga ndoa bila kuinvolve sherehe?
Sherehe lazima ila ukubwa wa sherehe ndio itategemea sasa
 
Nini sherehe, hivi hakuna uwezekano wowote hiyo ndoa tuifungie tu kabisa ndani, mfungisha ndoa akimaliza tumfungulie mlango atoke, halafu sisi tuanze zetu maisha mapya ya ndoa?? 😂
Umenena vyema mkuu.

Wanawake wengi wangekuwa na msimamo kama huu ndoa zingekuwa nyingi zaidi, maana kwa ME sherehe zinaleta stress tuu
 
Mimi nipo tayari ila mama yangu atasema over my dead body hahahahaha. Zile hekaheka za sherehe na zinavyomaliza hela kazi ya kukumbushia michango ni kazi kubwa mno kwangu kama nikiwa na chaguo la kufunga ndoa bila sherehe nitafanya.
Unalo chaguo.

I thought you are a free person
 
Sherehe baada ya ndoa ni anasa zisizo na ulazima.... binafsi napendelea ndoa simple tu... wawepo mashahidi na wazazi/ walezi inatosha. Na kama tutakuwa na pesa kidogo tutatoa sadaka kwa Yatima kwa ajili ya kumshukuru Mungu kutuvusha salama.

Kwa research yangu fupi ni kwamba ndoa nyingi zilizokusanya watu kwa sherehe kubwa huwaga hazidumu maana zinakuwa zimegubikwa na showoff na maigizo yaliyokosa Upendo ndani yake, kazi yao kubwa huwaga ni kufurahisha watu ili waonekane hawajafulia.....! Ngoja niishie hapo.
Dah..
KE wenye akili kubwa hivi mtandaoni wapo ila mtaani hakunaga🙄
 
Ndugu katibu mkuu Mnyatiaji kwa kweli kazi unayoifanya ni hadhina kubwa sanaaa
Kama mwenyekiti nimekukabidhi Hundi ya shilling 300 utapata mia hamsini

Na hiyo nyingne tutamnunulia Dada Carleen soda utamwambia mangi ela nyingine tunaiskilizia
Muweka hazina The Icebreaker naomba ufanye kazi hiyo kama muweka hazina uliyechaguliwa

Wenu mtiifu mwenyekiti uwabata
Kaka madenge
Naona mmeanza kutumia madaraka vibaya, kutoa huyo pesa yote burebure ni ufujaji wa pesa za chama. Mjitafakari.
 
Mimi nipo tayari ila mama yangu atasema over my dead body hahahahaha. Zile hekaheka za sherehe na zinavyomaliza hela kazi ya kukumbushia michango ni kazi kubwa mno kwangu kama nikiwa na chaguo la kufunga ndoa bila sherehe nitafanya.
Ukweli ni kwamba, wanaopenda sherehe mara nyingi ni wazazi, ndugu, jamaa na marafiki!

Wewe unaweza ukawa unataka kufanya kimyakimya, ukiwaeleza wazazi, kaka/dada, mashangazi nk wote wanakujia juu mara "ooh, sisi tumeshachangia watu wengi sana, hutaki na wao watuchangie? Tutaelewekaje uoe ata tusialike marafiki zetu/jamaa/vikundi vyetu vya kusaidiana/jumuia/wafanyakazi wenzetu nk?" "Utaoaje kimyakimya kama vile hauna ndugu/watu wa karibu?" "We usijali tuachie sisi kila kitu tutashughulikia..!!"
 
Hahahha not to my mother kuhusiana hasa na hiyo kufanya sherehe ama laah. Wazazi wa kiafrica wanapenda masherehe ndio muda wao wa kutamba. Utasikiaa weeeh mi nshawachangia sana halafu uolewe kimya kimya huna ndugu kwani.
Hahahahahahaha

I know what you are saying.... its Africa

Nice knowing that you are not married yet
 
Ukweli ni kwamba, wanaopenda sherehe mara nyingi ni wazazi, ndugu, jamaa na marafiki!

Wewe unaweza ukawa unataka kufanya kimyakimya, ukiwaeleza wazazi, kaka/dada, mashangazi nk wote wanakujia juu mara "ooh, sisi tumeshachangia watu wengi sana, hutaki na wao watuchangie? Tutaelewekaje uoe ata tusialike marafiki zetu/jamaa/vikundi vyetu vya kusaidiana/jumuia/wafanyakazi wenzetu nk?" "Utaoaje kimyakimya kama vile hauna ndugu/watu wa karibu?" "We usijali tuachie sisi kila kitu tutashughulikia..!!"
Kabisa yani. Halafu hamnaga tuachie sisi kila kitu unashangaa hela inakutoka tu mwanzo mwisho.
 
Back
Top Bottom