42774277
JF-Expert Member
- Aug 24, 2018
- 6,833
- 8,853
Mkuu, You are so Bright. I appreciate.Muandishi maoni yako yanajichanganya kama anavyo jichanganya Zainab na wanavyo jichanganya wenye Hotel.
Unapinga maoni ya kwamba suala la uhalifu lipo, kwa sababu bado uchunguzi hauja toa taarifa. Lakini kabla ya uchunguzi unatuaminisha kwamba Zainab ni tapeli? Hv Royal tour ndio kigezo muhimu cha majumuisho ya tuhuma za Zainab? HAPANA!
Tuhuma za Zainab zina uzito mkubwa, uzalendo pekee hapa ni kuihamasisha serikali kuzifanyia uchunguzi wa kina tuhuma hizi na kuja najibu lenye ukweli, kuliko sisi kupiga ramli kwa kigezo cha Royal tour.
Kwa upande mwingine tuhuma za uhalifu zipo katika nchi zote duniani, hasa kwa wageni (watalii) wanakuwa waathirika wakubwa. Mfano ni mimi mwenyewe, mwaka 2018 niliibiwa vitu vyangu hotelini znz. Na mazingira ya wizi yanaonyesha wazi wenye hoteli ndio walihusika na wizi huo. Wakati wakuandikisha maelezo kituo cha polisi palikuwa na wageni wengine wenye malalamiko sawa na ya kwangu. Lakini nilichogundua ni kwamba waharibifu wa kwanza wa uzalendo ni wenye dhamana (polisi) wanachojali ni maslahi binafsi kuliko athari zinazoipata nchi kwa matendo yao. Ni stori ndefu, lakini kwa ufupi ni kwamba sikuwa na jinsi zaidi ya kushirikisha ubalozi wa nchi ninayoishi baada ya kukosa hata barua ya polisi ili bima iweze kunirudishia vile nilivyo poteza kwa kuibiwa. Na hapa ndio nilipo ona uzalendo wa kweli kwa wenzetu kwa maslahi ya nchi zao.
Sina lengo la kumtetea Zainab, polisi ama wenye hoteli. Jibu sahihi litatokana na uchunguzi wa kina kama serikali ilivyo ahidi. Kwa sababu matukio ya uhalifu yapo znz kama ilivyo kwa nchi nyingi duniani. Uzalendo nikuhamasisha serikali ifanye uchunguzi wa haki, na kila mwenye haki apewe haki yake. Kuhusisha Royal tour na tuhuma za Zainab kwa maoni binafsi bila ya uchunguzi wa vyombo husika sio uzalendo.
You are so Honest.
Mungu akubariki.