Kiingereza ni kigumu kidogo. Mlinzi alifikishwa polisi. Baada ya yeye kusema kuwa alikaribishwa na Zainabu, Zainabu alishauriwa amshitaki yeye, kampuni iliyomwajiri na hata hoteli yenyewe. Zainabu alikataa kufanya hivyo kutokana na ushauri wa mawakili wake. Yeye akasema alipwe fidia ya dola 10000, lakini hoteli ikamwambia kuwa hawawezi kumlipa bila Mahakama kumkuta mlinzi ana hatia. Hoteli isingeweza kumshitaki mlinzi kwa sababu wao sio injured party. Na wangemshitaki halafu akathibitisha kuwa kweli Zainabu alimkaribisha, angeweza kuishtaki hoteli kwa kumharibia jina. Kitu kingine ni hofu ya kuset precedence. Watu wakijua kuwa hoteli iko tayari kutoa pesa ili kuepuka kuchafuliwa wengine wangemuiga Zainabu. Na itathibitisha kuwa huo ndio mchezo wa hiyo hoteli.
Inawezekana kuwa yalimpata kweli Zainabu lakini kukataa kwake kwenda mahakamani kumemharibia. Na hata kama ni PTSD, kukaa mwaka mzima kabla ya kuweka wazi yaliyomkuta yanafanya asionekane mwaminifu. Kingine ni simulizi zake kuhusu kunuka kwa jamaa, kumuita "baby", kukubali kwenda kuchukua kondom, kota kunanukia kutia chumvi.
Zainabu hapo mwanzo hakuzungumzia msaada na ushirikiano alioupata kutoka kwa wanasheria wa kizanzibari bali alikazania kuwa si hoteli wala polisi walimsaidia! Hii ni kujenga hoja kuwa wazanzibari ni watu ovyo sana.
Zainabu angeaminiwa zaidi kama angetumia huo mwaka aliokaa kimya kukusanya ushahidi kuwa kile kitendo hakikuwa isolated na kuna wengine yaliwakuta hayo hayo. Wengi wetu hatuna imani na polisi wetu na tunajua kuna watu waovu ambao wako tayari kuwatenda vibaya wanawake waliokuwa peke yao. Ila kwenye hili, Zainabu kawaangusha wenzake. Bahati mbaya kwake tunajua pia kuwa kuna wanawake ambao wanatembea na wafanyakazi wa hotelini, beach boys n.k. Kuna wanaume pia wanaofanya hivyo hivyo.
Amandla...