Wasaidizi wa kazi kutembea na Baba wenye nyumba kuna madhara. Dada wa Arusha apokonyea Mwili wa marehemu

Unajua maana ya mke? Mke ni kwenye karatasi, ndio ushahidi unaompa uhalali kwenye kila kitu kuhusu mume wake, awe hai asiwe hai. Kuzaa na mtu, kujengewa sio hoja, na hakuna cha common law kama kuna mke halali wa makaratasi. Huyo binti ameshavuna alichopanda, akae kwa kutulia. Alipanda uharibifu, amevuna uharibifu

Wazungu wanasema.. Play stupid games, win stupid prizes
 
Hii naona ndio taarifa iliyo nyooka kuliko zingine,na sentensi ya mwisho umeimalizia vizuri kabisa kabisa.
Nionavyo;
-Dada wa kazi hakuwa na kosa/hana kosa.Baba wa familia, mume wa ndoa ndio tatizo hapo.
-Mke mdogo kutaka kuzika bila kumshirikisha mke mkubwa, naona kuna njama za ndugu wa mume.
Mke mdogo katumika tu.
 
Kifo cha mmoja ni kumbusho kwa tuliobaki,
Kuna mengi ya kujifunza
 
Victim blaming. Unalalamikia house maids na ndugu badala ya mtu mwenyewe? Alilazimishwa kulala kila Kona na kuzaa nao? Hapo tatizo ni marehemu mwenyewe. Siku mkijua kukubali full accountability ya matendo yenu mtaendelea.
 
Hiyo sheria ni ki#£@m@&*÷o kweli
Ina maana watoto wa kike hawana kauli kwenye mali ya baba yao
 
Kila siku waifu akiniambia anataka alete beki 3 namuangalia kwa huruma sana.
Bora alete ndugu yake amsaidie kazi kuliko bek3.
Unam~Zoom Halafu Unasema
Kusikia Kwa Kenge Mpaka Atoke Damu Puani Na Masikioni
 
Hizi ndizo sababu zinazofanya familia za watu weusi zishindwe kurithishana utajiri kutoka kizazi kimoja kwenda kingine, huku ni kukosa discipline kwa matajiri wetu weusi
Sijawahi kuona wala kusikia tajiri abood ana nyumba ndogo au mambo kama haya
Na abood na ndugu zake wanaishi kwenye same household ,very disciplined hawa wenzetu ,mswahili akipata pesa basi atataka kutomba mademu wote mjini bila ya kuangalia shida atakayoipa kizazi chake, sasa hawa wanawake wataishia kumaliza hela mahakamani na kurogana , typica africans
 
😂
 
Nimeshuhudia picha kama hili.

Ila kilichotokea ni mke mkubwa na watoto kumtenga mume.

Mume akaondoka home, akaenda kuoa mke mwingine.

Alipofariki vikaanza vita vya mali.
 
Mahakama huwa haichagui msimamizi wa mirathi. Bali inamthibitisha tu.

Ni ndugu wenyewe ndio mtampendekeza kwenye muhtasari wa kupeleka mahakamani.

Na ukifoji tu msala
Na kama huyo mke hatakaa vizuri na ndugu, muhtasari kuupata inakuwa kimbembe. Hizi mali zitaua watu. Malumbano yote hayo ni sababu aliyekufa ni yajiri, angekuwa kapuku, hata michango ya msiba inausua sua, na watu wakizika tu hakuna anayetaka hata kujua watoto wa marehemu watasaidiwaje
Sikaki mali ya mtu mimi. Vya kwangu vinanitosha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…