Wasaidizi wa Rais, Please Msaidieni Rais Wetu Kwenye Public . Msimuachie Kila Kitu Peke Yake! .

Shukuru wewe unagombezwa via vyombo vya habari.

Ulishawahi kujiuliza wale anaokaa nao tangu ameapishwa kuwa Rais wamegombezwa au kupigwa makofi kabisa mara ngapi, usisahu kipigo cha mama jesca , hadi akalazwa Muhimbili.
Shukuru wewe unagombezwa via vyombo vya habari.

Ulishawahi kujiuliza wale anaokaa nao tangu ameapishwa kuwa Rais wamegombezwa au kupigwa makofi kabisa mara ngapi, usisahu kipigo cha mama jesca , hadi akalazwa Muhimbili.
yaani hao kama wakichunguzwa vizuri wanaweza kukutwa binadamu wasio na furaha kuliko wote Africa mashariki
 
Bwana Paskali unaweza kugusia pia watu wa usalama wana wajibu gani kwenye hili na wanaweza kutusaidiaje?
 
Humu hatuna mda wa kumshauri Rais,tutakuwa tunampa makavu LIVE uzuri anapenda USHILAWADU kila siku atakuwa anachezea za uso humu na kuumia kwa stress.Hatucheki na kima humu.'where we dare to speak openly'
 
Paskali uko sawa, lipo jingine ambalo Rais anahitaji kufahamishwa zaidi, ni suala la mchanga unaosafirishwa kwenda nje ili kupata madini mengine..sikubaliani na mtizamo wa Rais katika hili kutokana na yafuatayo:
1. Nchi ambayo mchanga unapelekwa ni Japan, labda kama kuna nchi nyingine siifahamu lkn kwa kadri ya kumbukumbu zangu ni Japan peke yake ndiyo inayo teknolojia ya kutenganisha hayo madini yanayobaki baada ya kutoa dhahabu, sasa ni vzr kujiuliza hata hivyo kabla hujawatuhumu watu, tujiulize yafuatayo, ni wapi Japan imehusishwa na uhalifu wowote nchi yoyote? hata tu raia zake..wapi?? Japan ni kati ya nchi zinazotusaidia katika mambo mengi, je ni sawa kwao kushiriki kutuibia madini yetu kana kwamba wanachopata kwny dili hiyo ni kingi sana kuzidi misaada wanayotoa kwetu..hakuna sehemu yoyote ambayo wenye teknolojia hii wamekubali kuweka mitambo hii kwny nchi zinazochimba dhahabu, nchi zote zinapeleka huko kwao(Japan)..lakini lbd tuangalie mfano huu hivi mkulima wa mahindi akipata mahindi mengi msimu fulani na akataka kuyakoboa apate unga lakin mashine ya kusaga unga hana, ni sawa kufikiri kwamba akienda kwa mwenye mashine ya kusaga kumshawishi ang'oe mashine yake ailete shambani kwake lazima mwenye mashine akubali??? sidhani..anaweza kataa hasa kwa sababu ya continuity, hakuna uhakika wa mwenye shamba kuendelea kulima mahindi siku zote, itakuaje siku amebadilisha akaamua kulima karanga, mashine zitafanya kazi gani..ndio maana wajapan hawataki kupeleka teknolojia yao popote wanapochimba dhahabu..kama hutaki kupeleka mchanga kwao acha..! kwa hiyo mimi sidhani km Tz inaibiwa kwny kupeleka mchanga huko..lkn pia si sawa Rais kurudia kushutumu kwamba tunaibiwa ilhali nchi kunakopelekwa mchanga ni Japan..Japan wanajisikiaje wanapomsikia Rais anawatuhumu kula njama na makampuni ya dhahabu kutuibia????
Rais hana kosa, tatizo ni wale washauri wake, lkn hata km hawasikilizi pengine ni vile ameingia madarakani kukiwa na historia mbaya ya utendaji serikalini hana imani na yeyote! kuondoa hili tatizo tusibaki kumlaumu Rais, tushinikize hizo taasisi zinazomshauri rais ikulu watu wake wabadilishwe kila anapoingia Rais mpya!!! there's no superman in this world! katiba itamke Rais anapoingia ikulu aingie na watu wapya wote..haiwezekani mtu yukpo ikulu zaidi ya miaka 20 unategemea nini, na kwa kweli kwa mtu anayefanya kazi inavyopaswa na kwa nature ya kazi za hapo ikulu, miaka mitano ni mingi sana..ataomba yeye mwenyewe kupumzika! ila kwa msindikizaji hiyo ni ndoto..anachoona yeye ni maslahi zadi na si kazi..kumekuwa na makosa makosa mengi sana kwa watu wa ikulu kwa kipindi hiki, WABADILISHWE! tuone km bado Rais ataendelea kutuhumu watu pas na kujua athari za tuhuma hizo!
 
Kuwa mbayu wayu utamuelewa Pascal .msikilize anacho eleza alafu changanya na akili yako
Inabidi uwe GT kuelewa maandiko yake. Kuna wakati anaandika straight na kuna wakati inabidi kusoma na kuelewa kinyume nyume. Lakini upande anaosimamia haujawai kubadilika toka aanze kuandika kuhudi hii administration
 
Kweli hili la mchanga linahitaji debate ambayo ni Objective. Tunajua mchango wa gold kwenye forex. Tunajua tz ina mikataba tata kwenye hii sector. Lakini na kivutio cha uwekezaji ni pamoja na kuiheshimu. Tumekuwa tukisikia kuwa hii mikataba ni ya hovyo lakini je tunachokifanya ni solution ya muda mrefu? Do we have options? Tuna mpango upi mbadala? Au timeamua kuacha madini ardhini kama tushauriwavyo na wanaharakati wa mazingira?
li
 
Hapa nilipo namchambua sizonje huku kushoto na kulia kwangu wamekaa ma ofisa wa jeshi la Polisi.
I wish they could see ninachokifanya kwa bosi wao.
 
Huu ni muendelezo wa ule wito kwa wasaidizi wa rais wetu, sio tuu kwenye hotuba, bali rais pia asaidiwe kwenye kupanga vipaumbele vyake, kwa maoni yangu vifo vya askari 8 vilikuwa ni muhimu zaidi kwa rais kuhudhuria na hata bendera kupepea nusu mlingoti.

Mwaka 1979 baada ya vita vya Kagera, kwenye ile parade ya mwisho Marubani wawili Capt. Saidi Karama na Capt. Abdala Kikinda waliripoti hitilafu ya kiufundi ya ndege vita ikiwa angani na ilianza kuangukia uwanja wa taifa full packed, ila wakatumia maneuvers na kuiangushia uwanja cha Chuo cha Ualimu. Kwa kawaida ndege hizo zina eject system ya "abandon & eject" ambapo Marubani wangesalimika lakini walijitolea kufa kunusuru maisha ya watu. Hawa walitangazwa mashujaa na Mwalimu Nyerere na bendera tulipepeza nusu mlingoti siku ya mazishi yao.

Pamoja na umuhimu wa mabweni yale, event hii ni static na haina time frame. Kuagwa kwa askari wale ni dynamic event with specified time frame.

Hata kwa jinsi rais wetu alivyo handle janga la Tetemeko la Bukoba it was mishandled na kuwa displeasing to many.
Mhe. Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli, "Sema Neno Moja Tuu, na Roho Zetu Zitapona!"
Hivyo wasaidizi wa rais lazima mumsaidie rais watu kupanga priorities zake, hili likifanyika, you never know kuna uwezekano wasaidizi wake wa mambo ya siasa wakamsaidia rais wetu kuona umuhimu wa katiba ambayo sio priority yake.

Wasalaam Jumatatu njema ya Pasaka.

Pasakali
Update.
Naendelea kuwasisitiza wasaidizi wa rais wetu wana wajibu wa kumsaidia. Anapopewa zile daily briefings, pia wamweleze kuna vitu vinafanywa illegally hivyo ni FYE only, hapaswi kuvisema.

Watu wanaojua wanaojua simu zinadukuliwa, na kuwa tapped, barua zinafunguliwa, e-mails zinakuwa traced na movements zinakuwa tracked, miamala ya simu, benki inakuwa recorded. Ukisafiri chumba unacholala kinakuwa bugged hata frequent places zako unawekewa tails, na weakness yako kama ndie ule udhaifu wa ngozi nyeusi unawekewa implants za chambo ili ujinasishe mwenyewe, ili vitu hivi kamwe havipaswi kusemwa wazi tena of all the people sio na rais wa nchi!.

Tumsaidieni rais wetu jamani!.

Paskali
 
Naendelea kuwasisitiza wasaidizi wa rais wetu wana wajibu wa kumsaidia. Anapopewa zile daily briefings, pia wamweleze kuna vitu vinafanywa illegally hivyo ni FYE only, hapaswi kuvisema.

Watu wanaojua wanaojua simu zinadukuliwa, na kuwa tapped, barua zinafunguliwa, e-mails zinakuwa traced na movements zinakuwa tracked, miamala ya simu, benki inakuwa recorded. Ukisafiri chumba unacholala kinakuwa bugged hata frequent places zako unawekewa tails, na weakness yako kama ndie ule udhaifu wa ngozi nyeusi unawekewa implants za chambo ili ujinasishe mwenyewe, ili vitu hivi kamwe havipaswi kusemwa wazi tena of all the people sio na rais wa nchi!.

Tumsaidieni rais wetu jamani!.

Paskali
 
Habari wanabodi,
Rais kutaja chanzo cha taarifa kiusalama sio hatari kwa mtoa taarifa?
Na rejea taarifa yake yakumtaja Prof. Mruma kama askari wa siri wakutoa taarifa tokea awali.
Naomba tujadili
Naendelea kusisitiza rais wetu lazima asaidiwe, kuna vitu vinaweza kusemwa in public, na kuna vitu havipaswi kusemwa hata kama vipo!.

Paskali
 
Naendelea na huu msisitizo wa wasaidizi wa rais wetu asaidiwe.
leo natoa u shauri rais wetu ni lazima atenganishe ni wakati gani atalihutubia taifa kama rais wa nchi na ni wakati gani atalihutubia kama Mwenyekiti wa CCM. Kitendo cha rais wa kufanya state event na kulihutubia taifa as Rais wa JMT na Amiri Jeshi Mkuu halafu ndani ya event anahutubia kama Mwenyekiti wa CCM na kuigeuza state event into CCM campaign conference na kupokea wanachama wapya, it's not only it's not fair, but it is wrong!.

Wasaidizi wa rais msaidieni rais wetu kutenganisha ni events gani atahutubia kama rais wa JMT na ni events gani atahutubia kama Mwenyekiti wa CCM.

Mkuu wa nchi anapokuwa fair, nchi inabarikiwa, anapokuwa unfair, nchi inalaaniwa. Baraka hizo la laana hizo zinasababishwa na kitu kinachoitwa karma, karma haijui cha mfalme, cha rais wa nchi or nani ni nani, karma inataka haki bin haki kutendeka, ile mockery ya kuwauliza madiwani wa CCM wanaotaka kwenda Chadema pia waje, it was uncalled for, I was wondering how mtu anayesema Shilawadu ndio the best TV show yake, this was a comedy, turning serious national events na ku insert comedy show inside, it's good kwa wapenzi wa comedy but very distasteful kwa wasiopenda comedy na maigizo kwenye serious matters.

Aambiwe na asaidiwe.

Paskali
 
Sijui kama unaeleweka

Samaki anakunjwa akiwa mbichi
 
Kweli
 
Pascal eee, kwa hili nakubaliana na wewe, inagawaje alikuita mayala=Njaa. Hapo umeongea point mno, hivi hotuba ya marudio ya mambo yale yale kwa mwaka hawa wasaidizi hawaoni kuwa inachosha masikioni mwa watu? tunalilia sana madini wakati tunaweza kuachana nayo kwa muda kwa kuwa hayaozi tukajikita kwenye kilimo. Wakati jeshi letu halina vita , hili jeshi lingekuwa mfano bora wa kuonyesha mashamba yaliyolimwa kisasa kwa kutumia maji ya mito inayotililika nchi mzima tukaweza ku-export kilimo, hawa wasahauli wamekazana kuweka ugumu watu wasiende mjini wakati kijijini ndio balaa tupo panawaka. Shaurini tuachana na mikataba ya zamani ya ziwa victoria tutumie ziwa hili kwa kilimo cha umwagilaji.
 

Mkuu paskali ni vitisho gani vilitolewa? umeme ulizima kwetu kwa siku tatu hivi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…