Wasanii wa hip-hop wa bongo, wamejipoteza kwenye game wenyewe

Wasanii wa hip-hop wa bongo, wamejipoteza kwenye game wenyewe

Ila bro huyo ulie muweka kwenye post yako umemkosea sana,mwamba anapiga mbona anapita kwenye majukwaa makubwa sana,af ni wewe/mimi tunaolalama,hao wameaumua kufanya kazi zao mfano labda wao kuuza kazi zao mkononi wanaona zina faida,miezi kadhaa ilopita Nash Mc alikuwa marekani huko na kafanya mbishe kibao za Hiphop,kasimama kwenye jukwaa la ma Mc hatari,jaribu kumfatilia af Mc'z hao tambua wana kazi zao nje na kazi zao za sanaa Mfano Stereo yeye pia ni muajiriwa wa Equity Bank

Msikilize Nash Mc [emoji1484]


 
Kuwa msafi, presentable, kufanya biashara, kuwa mstaarabu sio ushoga. Hii mentality ndio inafanya wanauza muziki kwa WhatsApp.

Niliona hata Nick Mbishi anaomba email za mashabiki unamtumia pesa anakumwagia mzigo kwenye email lakini pia haina tatizo kama wanatengeneza faida maana platform ni popote ambapo kazi inawafikia walaji hakafu whatspp na email hazina mtu kati hivo msanii anapiga chake moja kwa moja
 
View attachment 2404310

Kuishi maisha halisi sio kuwa mchafu, sasa mtu kama Nash unaamuzaje kwenye matangazo wakati image mbovu anakula kachori mtaani na makubazi.

Cheki swaga za Kendrick Lamar hapo juu yupo kitaa ila msafi alafu hiphop anaiweza ile yenyewe
Kwa hiyo unataka kusema Nash Mc si msafi, hivi unafatilia kiundani hawa wana Hip Hop Tz au kwa kuwa umeshiba ugali na maji mtaani kwenu yametoka umeshindwa fikiria vitu vyengine sasa? hebu fatilia mzee Nash anatokea Temeke na kazi ya sanaa ni KIOO CHA JAMII so unatakiwa uishi kulingana na JAMII yako ilivyo Kendrick Lamar ni msanii nje Africa pia anawakilisha JAMII anayoishi yeye anatakiwa kuishi kulingana na JAMII yake.

Nyie ndo vile vilaza vinavyo kurupukia habari zisizo kuwa na maadili ya KUJENGA JAMII, Unaweza niambia ni Msanii gani MBANA PUA anae WAKILISHA JAMII yake kupitia BUNGE? Angalia sasa HipHop wanavyo wakilisha kuna hao wa Tatu ambae sasa yupo Mmoja, kuna hao wengine walipambana wakakosa nafasi hiyo ya kuwa Mbunge mfano WAKAZI hii yote ni kwa sababu wanaishi na JAMII na wanaiwakilisha vyema katika NYANJA zote za KIMAISHA.
 
Miziiki yenu sahv hata mnachoimba hamjui....
Mara sijui inama nkupake wese
Ohh ingiza taratibu
Ndomana matamasha yenu yanajaa mashog tu

Ova
Matamasha kujaa ndio pesa zenyewe hizo, sasa wasanii wa hiphop uwa wanajazana pale msasani wanaimbiana wenyewe masela kwa masela si bora wakalime hata nyanya
 
Matamasha kujaa ndio pesa zenyewe hizo, sasa wasanii wa hiphop uwa wanajazana pale msasani wanaimbiana wenyewe masela kwa masela si bora wakalime hata nyanya
Ndio maana nyie watoto wa Sinza mnaharibikiwa sana sasa hivi

Ova
 
Tatizo la watu wengi ni kutokuwa na uelewa juu ya huu mziki na ndio maana unapewa tafsiri mbaya

Nash Mc ni moja kati ya wasanii wa Hip Hop ambao wanaishi maisha yao halisia, mtandaoni mpaka mitaani.

Na huo ndio moja ya misingi ya Hip Hop kutoka Underground Hip Hop

Unataka Maalim Nash abadilike. Unataka aweje? Ikiwa mtaani kwako tu kuna bunch of singers wanaoimba mtindo unaoupenda na bado hawasikiki

Dizasta alisema moja ya sababu ya yeye kutokuwa maarufu ni kutokana na jamii kushiba sana ujinga

Hauko tayati kusikiliza Diwani ya Maalim Nash ila uko tayari kusikiliza "Nataka Nikuto" ya Harmonize
Mashairi yao mazuri sana ,mitindo yao ya kuchana ipo poa sana.Tatizo.beat zao.mbaya sana.Hazina mvuto,hazina ule ubunifu na mvuto wq kihip hop.Nilikick na snate tu linagonga hapo.Na libase na kinanda ambacho kinarudia tudia tu.Jamani wasikilize hata beat za DJ Premier,Dr Clue,RZA,Dr Dre,True Master n.k.Wajifunze beat zenye akili.
 
Hilo ndo tatizo mlilo nalo. Mnaamini hip hop haiwezei kuwa na beat kali ila trap. Nikutolee mfano tu beat kama ya still Dre, 1 23,4 ya LL Cool J, Final coundownnya EPMD, Nas is like ya Nas. Je zile ni trap. Na utazifananisha zile beat na mabeat mabaya ambayo wanachania akina Nick na Maalim Nash. Mimi nazungumzia beat zilizoenda shule za HIp Hop sizungumzi trap.
Hao wasanii waliochoka kuna siku walikuja kukugongea mlango uwasaidie unga?

Unasema kwamba

"Mabeat ya hipo hop meni mabaya. Mfano nyimbo nyingi za Nick Mbishi, mashairi mazuri ila beat"

Nikki mbishi ulimsikia kwenye Tz Bongo?

Alisema trap beats ndio kipenzi cha ma-teenagers
 
Mrisho Mpoto aliwahi kukimbiza huu muziki, kwa mashairi yake ya kufikirisha. Wala hakuwa na beats za kuvutia. Watu tulipenda mashairi yake sababu tuliweza kuelewa ujumbe alioukusidia!

Kizazi cha sasa kinataka nyimbo kama "nyegezi", ndipo uelewa wao unapoishia. Hawawezi kuelewa lyrics na punchlines za watu wanaojua kutumia akili zao vizuri.

Kwahiyo wasilaumiwe wasanii wa hiphop. Tuwalaumu mashabiki kua na uelewa mdogo. Na dalili moja wapo ya uelewa mdogo, ni kuthamini beat badala ya mashairi yanayoimbwa!
Ndo maana mtu mmoja kasema watu wa hip hop wanajifanya wajuaji sana. Sisi tunasema wengi wanafeli kwenye beat. Wana punch line, styles, lyrics nzuri. Ila kama beat zinakuwa mbaya kwa kila muda. Kazi zinaanza kikosa mvuto. Yaani kama jinsi ambayo msaani wa hip hop anavyotakiwa kiwa na punch l8ne na lyrics nk. Ndivyo ambayo composer wa mziki wa hip hop naye anatakiwa kuproduce mziki au beat ambayo ni hip hop. Beat nzuri. Nitolee mfano tu beat ya frwsh ya fid. Hebu jaribu kuwaza Nick Mbishi na mistari yale angetqmbaa pale. Wewe unaona kitu ambacho kingetokea pale.
 
Sijawahi kumsikia MC Nash lakini nimeingia youtube nimeangalia nyimbo zake, yuko vizuri na nyimbo yake ya Maneno naona kaeleza struggle yote ya mziki wa hip hop bongo, pole brother labda kuna siku utatusua
 
Ndo maana mtu mmoja kasema watu wa hip hop wanajifanya wajuaji sana. Sisi tunasema wengi wanafeli kwenye beat. Wana punch line, styles, lyrics nzuri. Ila kama beat zinakuwa mbaya kwa kila muda. Kazi zinaanza kikosa mvuto. Yaani kama jinsi ambayo msaani wa hip hop anavyotakiwa kiwa na punch l8ne na lyrics nk. Ndivyo ambayo composer wa mziki wa hip hop naye anatakiwa kuproduce mziki au beat ambayo ni hip hop. Beat nzuri. Nitolee mfano tu beat ya frwsh ya fid. Hebu jaribu kuwaza Nick Mbishi na mistari yale angetqmbaa pale. Wewe unaona kitu ambacho kingetokea pale.
Dah aisee nimegundua weusi nyimbo zao kali kwa kuwa hata beat huwa tamu.
 
View attachment 2404153
Picha hii inamuonesha Nash MC, mmoja kati ya wasanii wa Hip Hop Nchini​

Ni wazi muziki wa hip-hop wa bongo umepotea kabisa. Wasanii wa hip-hop hawafanyi vizuri sokoni yani kwa sasa bongo ukiimba hip-hop unaonekana kama umechanganyikiwa. Tofauti na zamani kidogo hiphop ulikuwa inafanya vizuri sana.

Sasa huu muziki umefikaje hapa?

Wasanii wa hip-hop ndio chanzo.

Kwanza, hawataki kubadilika kuendana na soko linachotaka.

Pili, hawawezi kujibrand yani unakuta msanii mchafu kavaa makubazi anakula kashata mitaani hawezi kuvutia makampuni kumtumia kama image ya biashara zao.

Tatu, wasanii wa hiphop kila mtu mjuaji umkute Wakazi, Roma, Niki Mbishi sijui Nash MC wao wanajua kila kitu hawataki kujifunza.

Nne, usela wa kizaman tuliitaga usela nondo. Kujifanya umepinda unakaza, mtu akifanya mambo ya maana utasikia sio real huyo wana zile wanaita wanatunza misingi mara wanaokoa mitaa imagine mtaa uokolewe na mvuta ganja mmoja aliyekwama maisha 😄😄

Tano, kupenda lawama hakuna wasanii wenye lawama nchi hii kama watu wa hiphop wanasemaga muziki wao unabaniwa ila wakiambiwa wabadilike kidogo kuendana na soko wanakuwa wakali sijui kwa kuwa vipaji vyao haviruhusu kubadilika 🤔🤔 sasa nani atafanyia promotion bidhaa isiyo na soko

Mwisho nawashauri watu wa hiphop wabadilike muziki unazidi kuwaacha, Prof J alikuwa nominated MTV awards lakini kizazi cha leo ikitoka list ya wasanii wanaofanya vizuri kwenye hiphop Africa huwezi waona ukiuliza bongo hiphop mbona hatuwaoni utaambulia matusi au kumlaumu Sallam Mendez au watajifichia kuwa wao hawaimbii tuzo wanaimbia vijana wa mitaani 😂😂

Ni hayo tu watu wa hiphop msitafute wa kumlaumu tatizo ni nyinyi wenyewe...unakunywa double kick muda wote alafu unataka upewe show mil 10 inawezekana vipi
IMG_20221105_212634.jpg
IMG_20221105_212644.jpg
IMG_20221105_212553.jpg
IMG_20221105_212545.jpg
IMG_20221105_212626.jpg
IMG_20221105_212603.jpg
IMG_20221105_212603.jpg
 
Back
Top Bottom