Wasanii wa Tanzania wengi wameishia Kidato cha pili, hawana elimu ndio maana wako hivyo walivyo

Wasanii wa Tanzania wengi wameishia Kidato cha pili, hawana elimu ndio maana wako hivyo walivyo

Mkuu nakuunga mkono [emoji817]%..mm mwenyew Nina degree tena na gpa nzur tu (4.0) ila najuta nimepoteza muda sn kudadadek zang!!!

Ila nimeshaingia kwny business..mpaka kieleweke
Mkuu hongera , nchi hii elimu yake ni MZIGO tu watu wamekaririshwa toka utotoni soma upate kazi nzuri uwe na maisha mazuri, basi mtu ana focus na shule akiwaza ajira na maisha mazuri ndio maana wengi hata wakipata hizo ajira wanaona siku zinaenda hajapata utajiri/ maisha mazuri ndio wanajiingiza kwenye wizi na ufisadi. Ukitaka kujua elimu yetu ni mzigo rais juzi alisema alimtengua mwenye elimu ya chuo kikuu alipokuwa waziri wa ujenzi hiyo kazi akampa wa darasa la saba na aliifanya vizuri tu, rejea mkutano wa rais na wadau wa umeme na Tanesco, kama uliangalia ulijionea waajiriwa wa tanesco wenye PHD walivyokuwa mbumbumbu kwenye maswala ya umeme ukilinganisha na wale wazee wa darasa la saba wanao fanya kazi ya umeme kwa vitendo. Acha watu wajifariji kwa kuangalia vyeti vyao.
 
Una point fulani.

Msingi mzuri wa haya mambo ni miaka ya mwanzo.

Ndiyo maana unakuta jitu limesoma mpaka Ph.D lakini kujieleza ni ushamba mtupu.

Kwa sababu msingi mbovu.

Umeongea vizuri hata wasomi wetu wala asikutishe kwa tittle name yake maana unakuta mtu anaelezea kitu chenyeumuhimu eti anachomekea ili mcheke, haya mtu unakuta kujieleza anaenda kuweka na maneno ambayo hayahusiki na alichoulizwa hapo utaona watu hawapo makini na hata viongozi anahutubia saa moja hata haeleweki alikua anawasilisha nini mbele ya hadhara.
 
Una point fulani.

Msingi mzuri wa haya mambo ni miaka ya mwanzo.

Ndiyo maana unakuta jitu limesoma mpaka Ph.D lakini kujieleza ni ushamba mtupu.

Kwa sababu msingi mbovu.
Yes , ndiyo hivyo mkuu
 
Acha kuongea ujinga wewe,Elimu huwa haina hasara labda kama ulienda shule kujifunza ujinga,shida ya wabongo mnaenda shule kukua ndio maana mnaona kama elimu haiwasaidii.
Mkuu assume umesome mpaka phd , halafu umekosa ajira na pia umeshindwa kujiajiri may be kutokana na kozi uliyosoma , je hapo haujapata hasara , au umepata kazi ambayo mshahara wake ( general earnings) , je hapo haujapata hasara , maana ukilinganisha muda ( resources) ulizotumia ni kubwa kuliko unachopata ( return on the investment)
 
unatoka povu sana umesha badili BAHASHA ngapi? Elimu ya TZ haisaidii wengi ndio maana wasomi hawaja fanya la maana zaidi ya kukaa kujisifia usomi wao, wengi walio soma wanalilia ajira tu serikalini, shule inasaidia sana ila sio kama alivyosema mtoa mada kuwa wasanii hawana shule, mbona wamefanikiwa? wameweza kutatua changamoto zao? Acha ujinga wewe usie elewa MADA , pole endelea kujisifia ujinga wako
Huwezi kuelewa nlichoandika, rudi shule kwanza ukasome tena.
 
Mkuu assume umesome mpaka phd , halafu umekosa ajira na pia umeshindwa kujiajiri may be kutokana na kozi uliyosoma , je hapo haujapata hasara , au umepata kazi ambayo mshahara wake ( general earnings) , je hapo haujapata hasara , maana ukilinganisha muda ( resources) ulizotumia ni kubwa kuliko unachopata ( return on the investment)
Mtu aliyesoma akaelimika huwa hana hasara, Tofautisha kwanza hivi vitu kusoma ukaelimika na kusoma kutoelimika

Mafanikio ya kiuchumi hiyo ni natural instincts haifundishwi shuleni,yoyote anaweza kuwa nayo yaani aliyesoma na asiyesoma.
 
Na bado unawasikiliza.
Teh teh teeh! maisha haya bhaana!
 
Umeongea vizuri hata wasomi wetu wala asikutishe kwa tittle name yake maana unakuta mtu anaelezea kitu chenyeumuhimu eti anachomekea ili mcheke, haya mtu unakuta kujieleza anaenda kuweka na maneno ambayo hayahusiki na alichoulizwa hapo utaona watu hawapo makini na hata viongozi anahutubia saa moja hata haeleweki alikua anawasilisha nini mbele ya hadhara.
Viongozi hususan wanasumbuliwa na "madaraka ya kulevya".Yni mtu anajiona kwa kuwa kapata uongozi, katika system ambayo haiangalii merit, basi lazima yeye atakuwa na akili sana na watu wamsikilize.

Ndipo hapo watu wanachemsha mpaka kwenye hotuba rahisi tu ya kwenye msiba.
 
Huwezi kuelewa nlichoandika, rudi shule kwanza ukasome tena.
Na sitaki kueleweshwa upuuzi, shule hata nikirudi mara kumi nitakuta mtaala ule ule ambao haujakusaidia kutatua changamoto zako., hao wasio na elimu wamefanya makubwa na mzuri kuliko mnao jiita mmefika mbali, si bure hata profesa anakiri alikuwa jalalani.. Elimu tuipate lakini elimu ya ulimwengu nje ya shule ni zaidi.
 
Mkuu nakuunga mkono [emoji817]%..mm mwenyew Nina degree tena na gpa nzur tu (4.0) ila najuta nimepoteza muda sn kudadadek zang!!!

Ila nimeshaingia kwny business..mpaka kieleweke
Kwa hiki ulichokiandika, na hiyo GPA yako uliyoipata chuoni, haviendani kabisa. Ila spirit ambayo umeipata ya kutafuta mpaka kieleweke, nakupongeza.
 
Kwa hiki ulichokiandika, na hiyo GPA yako uliyoipata chuoni, haviendani kabisa. Ila spirit ambayo umeipata ya kutafuta mpaka kieleweke, nakupongeza.
Wengine tuna 3.4 na hatujitii kabisa na tupo confident na vitu tunavyofanya. Bro kuna sehemu alikosea lakini sasa hivi ana muda wa kijirekibisha.
 
suala la kujieleza ni tatizo kubwa sana hata humu JF

kuna watu kitu cha kuelezea kwa sentensi yenye maneno matano tu, yeye anaandika paragraph mbili ndio anaeleweka.

Ila huwa namsifu sana Nyani Ngabu.
 
suala la kujieleza ni tatizo kubwa sana hata humu JF

kuna watu kitu cha kuelezea kwa sentensi yenye maneno matano tu, yeye anaandika paragraph mbili ndio anaeleweka.

Ila huwa namsifu sana Nyani Ngabu.

Duh!

Sasa mi niliyeishia fom foo unanisifu kwa lipi hasa? 🤣🤣🤣
 
Mayweather Jr,Mess,Ronardo Cristiano...ni mabilionea wakubwa...wenzetu wanawekeza katika vipaji,sisi tofauti kabisa...
 
Duh!

Sasa mi niliyeishia fom foo unanisifu kwa lipi hasa? 🤣🤣🤣

🤪🤪🤪pamoja na kuishia fom foo lakini unajua sana kupangilia maneno na kueleweka kwa urahisi ukiwa unaelezea jambo, pengine kuliko hata wenye ma PHD yao.

Kitu ambacho wengine hili tuweze kueleweka kwa urahisi, yatupasa tuandike paragraph mbili ila wewe unakielezea kwa sentensi moja tena fupi tu.
 
Wameajiri wenye degree kabisa mkuu, dunia hii ya leo bado kuna watu wanaringia vyeti?

Hao wanaoringia vyeti wanafikiri bado tupo kwenye enzi ya UJAMAA. Wanatakiwa kujua kuwa UJAMAA ulishafeli duniani.
 
Na sitaki kueleweshwa upuuzi, shule hata nikirudi mara kumi nitakuta mtaala ule ule ambao haujakusaidia kutatua changamoto zako., hao wasio na elimu wamefanya makubwa na mzuri kuliko mnao jiita mmefika mbali, si bure hata profesa anakiri alikuwa jalalani.. Elimu tuipate lakini elimu ya ulimwengu nje ya shule ni zaidi.
Huyo anaekubishia hana point..ELIMU ya bongo upuuzi tu!! Ningekuwa sijasoma mngesema ningesoma ningeona..ila nimesoma had ngaz za juu kidogo(University)

Hunidanganyi kitu..UPUUZI TU!!!

ELIMU GANI UKIINGIZA MAWAZO YAKO INAONEKANA UMEKOSEA!!!!
 
Back
Top Bottom