Wasanii wanaoimba kuhusu bangi wapewa onyo

Badala wazuie kitimoto hata vitabu vya dini vinekataza wai wanaangaika na ganja. Hii kitu ni tamu hasa ule moshi ukiwa unautolea kwa puani 😋😋
 
Ni sheria ipi iliyovunjwa? Ama hatua gani hizo za kisheria zitachukuliwa?
 
Miss u mwenza. Hlf nitakuletea siku moja...na hivyo vimacho vyako sijui utakuaje[emoji28][emoji28]
Mwenza hapana aiseee me kuna vitu acha niwe mtazamaji na hiyo ikiwepo [emoji1787]mpaka kufikia uzee huu hivyo vitu sijawahi kugusa acha viendelee kunipita
 
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Gerald Kusaya amewaonya Wasanii wa Tanzania wanaotunga nyimbo za kuhamasisha matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo bangi na kusema hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa Wasanii hao.

Akiongea na Waandishi wa Habari, Dar es salaam leo amesema “Kuna Wasanii wanahamasisha matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo bangi, kama kuna Wasaniii ambao wanadhani badala ya kutunga nyimbo za kuhamasisha Jamii wao wanatunga nyimbo za kuhamasisha matumizi ya dawa za kulevya, sheria yetu inasema hao tutawachukulia hatua”

“Kama kuna Msanii anadhani anaweza kupata umaarufu kwa kupitia nyimbo za kuhamasisha matumizi ya dawa za kulevya hatutomuacha hata mara moja, sheria itachukua mkondo na ipo siku nitawaita Waandishi wa habari ili muone kitu gani tumekifanya kwa Wasanii wanaotaka kupata umaarufu kwa kutumia dawa za kulevya”

“Mbona mashairi yapo ya aina nyingi unashindwaje kutunga mashairi ya vitu vyote, si wahamasishe hata kilimo bora au biashara, kwani lazima wahamasishe mambo ya bangi? hatutoruhusu Mtanzania yoyote afanye uhamasishaji wa matumizi ya dawa za kulevya”
Kweni pombe sio dawa ya kulevya?.. Binafsi nashauri mswada wa Bangi urudi bungeni tu [emoji23][emoji23][emoji23]

Iruhusiwe tuu.. Itakuza uchumi kuliko tumbaku na ukizingatia haina madhara kama tumbaku pia
 
Bangi ina majina mengi sana. Tutaimba kuhusu bangi ila kwa lugha za mtaani. Kamishina akapambane na bange mashambani sio kwenye mistari ya ngoma za watu
 
istockphoto-618949892-612x612.jpg
Tuko Pamoja👊🏾
 
Huyu angetuacha na bangi yetu tu, kuna wasanii wapo na mashoga kila siku na huwezi kusikia hili wakiongelea ila linapokuja suala la kiburudisho wanaleta mhaho

Back
Top Bottom