Washauri wa Rais Magufuli, mshaurini aache kutumia Kiingereza kwenye hadhara

Washauri wa Rais Magufuli, mshaurini aache kutumia Kiingereza kwenye hadhara

Mmekosa hoja....Nyie hata kiswahili hamjui sembuse kingereza....!!Upinzani wengi ni vijana mpechempeche marioo wa mjini wapenda vya bure,kingereza wamekijulia Kwenye movie na nyimbo za kina Cellin Dione...Wanaume wa kweli hawezi ongea hoja za kijinga kama hizi...!!
Ni mafundi wa kukosoa wakati wao ndio wa kukosolewa.

Ni vijana wa mijini haswa Dar ndio wenye kudhani wana haki miliki ya Tanzania.

Wanamchukia Magufuli kwa sababu utajiri wa nchi anausambaza kote, miundo mbinu iliyomponya Zitto Kabwe imesambazwa kote.

Pesa iliyokuwa ikiliwa hovyo miaka ya nyuma kwa sasa inajenga nchi nzima hivyo hawa wanaoumia mioyo yao lazima watafute namna za kujifariji.
 
Mkuu lugha ya kufundishia Tanzania kutoka form one to phD ni kiingereza,sasa kama lugha inayotumika huijui niambie unatumia mbinu gani kuelewa unachofundishwa au unachosoma kwenye vitabu na mitihani unafanyaje? Please assist
Kwaiyo msomi lazima ajue kuongea kiingereza?
 
Sasa kwanini ulazimishe kuongea lugha usiyoiweza wakati una nafasi ya kutumia lugha unayoimudu vyema.Nae ni hovyo tu
Mabeberu wangapi wanapiga broken za kiswahili au lugha nyingine lakini watu wanachukulia poa tu.

Kumbuka usomi haupimwi kwa kujua lugha ya kiingereza
 
Hachekwi kwa sababu ni Rais. Na mfano wako haufanani na uhalisia. Watu wanashangaa mtu ambaye kasoma mpaka kiwango cha Phd kiingereza ikiwa lugha ya kujifunzia na kufanyia mitihani, na akawa mwalimu akifundisha kwa kutumia kiingereza, lakini hakijui kiingereza kwa kiwango kile. Mimi binafsi namhurumia tu kwani si tatizo lake binafsi bali ni tatizo la mfumo wa elimu yetu. Kiingereza ni lugha tu kama kisukuma au kiswahili. Mbona anafahamu hizi lugha zingine? Vile vile, ukipitia kauli zake, utaona Rais wetu ana tatizo la msingi ambalo si la kujitakia. Ni wa kuhurumiwa tu wala si kuchekwa. Pole Mr. President.
Hapo unaweza kuona level of understanding ya huyo prove iko wapi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio yeye Tu. Watz wengi kingereza ni changamoto hasa tenses
 
Mabeberu wangapi wanapiga broken za kiswahili au lugha nyingine lakini watu wanachukulia poa tu.

Kumbuka usomi haupimwi kwa kujua lugha ya Kiingereza.
Msomi ni nani?

Huyo beberu kama amesoma kwa lugha ya Kiingereza kuanzia elementary school hadi doctorate na akashindwa kuongea kiingereza nae ni utopolo kama wengine tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi kulikuwa na haja ipi ya mh kutumia neno 'stupid' mbele ya mgeni na halaiki ile hasa alipofoka juu ya ucheleweshwaji wa mradi? Niliona hadi wafuasi wa mh chakwera wameinamisha vichwa chini kwa kutoamini.
 
Wewe kwa upeo wako mdogo ndiyo unaona ni hoja ya kijinga. Hapa tunazungumzia mtu aliyeandika thesis ya kitaalam ya kuhitimu Phd baada ya kufanya utafiti na baadae akawa mwalimu akifundisha kwa kutumia lugha ya kiingereza. Aliwezaje kumudu yote hayo wakati hawezi kuongea kiingereza ''cha kuridhisha''? Na wala siongei kile kizuri.

Nimekutana na wasomi wengi ambao english inawapiga chenga lakini wakizungumza unaona kabisa wana mwelekeo wa usomi na unaridhika. Yeye ni mweupe pee. Hata maswali rahisi anashindwa kuelewa sembuse kujibu! Something very very wrong with his education!

Wengi tunatofautiana kimawazo na sio dhambi lakini linapokuja suala la kujua lugha sidhani kuwa kujua kiingereza fasaha ni moja ya sifa za kuchaguliwa kuwa Rais,

Pale Kariakoo, Kinondoni, Temeke etc pana mateja kibao wanamenya mayai kama wametoka kwa mama leo lakini ndio hivyo hawana msaada wowote ktk jamii yetu

Marais wengi tu wapo hapa duniani hawajui Kiingereza lakini inchi zao zimepiga hatua ya juu kabisa ya maendeleo na kiuchumi kuliko baadhi ya inchi zenye Rais anayejua vizuri hiyo lugha
 
Ni Tanzania tu maajabu kama haya hupatikana. Sasa piga mahesabu darasani alikuwa anafundishaje!
'Macho', ni rahisi kulijibu hili swali la "huko darasani".
Jibu liko kwenye tabia yake ya kimabavumabavu (forcefullness); hata kwenye uongozi ni mbinu hiyo hiyo anayoitumia kuziba 'weaknesses' zake.

Atatumia mabavu na nguvu nyingi kuzima watu wasihoji. Inapolazimu, anahonga, kama anavyotembea na maburungutu ya manoti au 'utumbuaji' na 'uteuzi' wa papo kwa papo.

Ni fujo hizo hizo atakuwa anazitumia darasani kuwatia vitisho wanafunzi wamwogope na wasihoji 'weaknesses' zake.
 

Bila shaka hapa utajifunza kitu!
Hamna cha kujifunza hapo,mfano hapo Putin ,Russia lugha ni kirussia tu hamna english ni kama china tu ,huku kwetu english ni lugha ya darasani na lugha ya pili ya taifa huyu mzee amemalizaje shule zote hajui english
 
Back
Top Bottom