Washauri wa Rais Magufuli, mshaurini aache kutumia Kiingereza kwenye hadhara

Ni mafundi wa kukosoa wakati wao ndio wa kukosolewa.

Ni vijana wa mijini haswa Dar ndio wenye kudhani wana haki miliki ya Tanzania.

Wanamchukia Magufuli kwa sababu utajiri wa nchi anausambaza kote, miundo mbinu iliyomponya Zitto Kabwe imesambazwa kote.

Pesa iliyokuwa ikiliwa hovyo miaka ya nyuma kwa sasa inajenga nchi nzima hivyo hawa wanaoumia mioyo yao lazima watafute namna za kujifariji.
 
Mkuu lugha ya kufundishia Tanzania kutoka form one to phD ni kiingereza,sasa kama lugha inayotumika huijui niambie unatumia mbinu gani kuelewa unachofundishwa au unachosoma kwenye vitabu na mitihani unafanyaje? Please assist
Kwaiyo msomi lazima ajue kuongea kiingereza?
 
Sasa kwanini ulazimishe kuongea lugha usiyoiweza wakati una nafasi ya kutumia lugha unayoimudu vyema.Nae ni hovyo tu
Mabeberu wangapi wanapiga broken za kiswahili au lugha nyingine lakini watu wanachukulia poa tu.

Kumbuka usomi haupimwi kwa kujua lugha ya kiingereza
 
Hapo unaweza kuona level of understanding ya huyo prove iko wapi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio yeye Tu. Watz wengi kingereza ni changamoto hasa tenses
 
Mabeberu wangapi wanapiga broken za kiswahili au lugha nyingine lakini watu wanachukulia poa tu.

Kumbuka usomi haupimwi kwa kujua lugha ya Kiingereza.
Msomi ni nani?

Huyo beberu kama amesoma kwa lugha ya Kiingereza kuanzia elementary school hadi doctorate na akashindwa kuongea kiingereza nae ni utopolo kama wengine tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi kulikuwa na haja ipi ya mh kutumia neno 'stupid' mbele ya mgeni na halaiki ile hasa alipofoka juu ya ucheleweshwaji wa mradi? Niliona hadi wafuasi wa mh chakwera wameinamisha vichwa chini kwa kutoamini.
 

Wengi tunatofautiana kimawazo na sio dhambi lakini linapokuja suala la kujua lugha sidhani kuwa kujua kiingereza fasaha ni moja ya sifa za kuchaguliwa kuwa Rais,

Pale Kariakoo, Kinondoni, Temeke etc pana mateja kibao wanamenya mayai kama wametoka kwa mama leo lakini ndio hivyo hawana msaada wowote ktk jamii yetu

Marais wengi tu wapo hapa duniani hawajui Kiingereza lakini inchi zao zimepiga hatua ya juu kabisa ya maendeleo na kiuchumi kuliko baadhi ya inchi zenye Rais anayejua vizuri hiyo lugha
 
Ni Tanzania tu maajabu kama haya hupatikana. Sasa piga mahesabu darasani alikuwa anafundishaje!
'Macho', ni rahisi kulijibu hili swali la "huko darasani".
Jibu liko kwenye tabia yake ya kimabavumabavu (forcefullness); hata kwenye uongozi ni mbinu hiyo hiyo anayoitumia kuziba 'weaknesses' zake.

Atatumia mabavu na nguvu nyingi kuzima watu wasihoji. Inapolazimu, anahonga, kama anavyotembea na maburungutu ya manoti au 'utumbuaji' na 'uteuzi' wa papo kwa papo.

Ni fujo hizo hizo atakuwa anazitumia darasani kuwatia vitisho wanafunzi wamwogope na wasihoji 'weaknesses' zake.
 
Bila shaka hapa utajifunza kitu!
Hamna cha kujifunza hapo,mfano hapo Putin ,Russia lugha ni kirussia tu hamna english ni kama china tu ,huku kwetu english ni lugha ya darasani na lugha ya pili ya taifa huyu mzee amemalizaje shule zote hajui english
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…