Washington Post: Hakuna namna Rais Magufuli anaweza kujitenga na uwajibikaji kutokana na matendo ya Makonda

CCM inatizamwa kwa jicho baya sana kwa sasa especially na wafadhili. Wanafahamu kuwa tatizo ni ccm kama ukisoma hiyo makala vyema. Ni mfumo mbaya sana. Ni wazi kelele za tume huru na katiba mpya vitapewa kipaumbele na ccm na serikali yao wajitafakari kabla ya kuendeleza utamaduni wao wa bao la mkono! Maana naona mambo yanabadilika kwa kasi.
Naiona Zimbabwe ya Mugabe ikihamia Tanzania

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niliwahi kusema na narudia kusema. Maamuzi juu ya utawala wa Tanzania yalikwishafanyika tangu mwakajana. Kilichobakia ni utekelezaji.

Tegemeo kubwa, ni kuwa utawala utafanya makosa kwenye uchaguzi wa 2020. Na watawala wakitenda kama inavyotarajiwa, watawala na sisi sote tutajutia, na ukumbuka uchaguzi wa 2015 na 2020 katika maisha yetu yote. Hili nitawakumbusheni daima.

Kati ya sasa na mwezii wa Octoba kutakuwa na makundi mbalimbali ya mamlaka za Dunia, yatakuja ili kujiridhisha na ambayo yamekuwa yakitendeka nchini.

Wenye dhamira na nia ya kugombea nafasi mbalimbali 2020, wasisite, wasihofu. Wafanye maandalizi maana ni ama uchaguzi utakuwa huru kwa kiasi kikubwa (watawala wakipata hekima) au watakuwa mashahidi katika hatua ambayo Dunia itachukua dhidi ya ugandamizaji.
 
Umenena vyema, mwenye masikio na asikie.
 
Duuuu hii taarifa naona wameifanyia utafiti kipindi kirefu sana sasa wameamua kumwaga ugali

Sent using Jamii Forums mobile app
Inaonyesha taarifa wanazo toka kitambo. Na kuna uwezekano watu wako kwenye rada zao. Barua ya juzi ya Mike Pompeo inadai wana ushahidi. Halafu barua kutoka kwa Pompeo siyo kitu kidogo. Hii inaonyesha kuwa mamlaka za juu sasa zina fuatilia yanayoendelea nchini kwa jicho la tai!
 
Inabidi wajitahmini, siyo tu viongozi wa serikali wanaotupiwa macho, bali sasa hata wao wamegunduwa ccm ndo tatizo kwenye siasa zetu.
Mimi nilikiwa MwanaCCM damu damu lakini nilipoanza kuona katiba inafungiwa vitumbua sheria zinatumiwa upande mmoja upande mwingine ni kama sio Watanzania wenzetu halafu mauaji yalipoanza nilijua labda ni siasa za Upinzani tu lakini nilipoona kuwa hakuna hatua zinazochukuliwa nikasema CCM sio baba wala Mama yangu

Tokea wakati huo nikaanza kujitathmini na kuomba toba kuwa nilikuwa kwenye taasisi ambayo ina damu za watanzania wenzangu katika mikono yake.
 
Nakumbuka sana mkuu, hakuna aliyeamini. Kweli wewe ndiye mfano halisi wa ile kauli ya baba wa Taifa alipoulizwa kama anaweza kuachana na ccm. Alisema maneno kama hayo, alisema “ccm siyo baba wala mama yangu”

Mwandishi wa The Washington post alisema wazi kuwa ccm iko madarakani toka uhuru, lakini hatujawahi kuwa na demokrasia ya kweli, ila wanasema hali imeharibika zaidi baada ya Maghufuli kupata urais bila yeye kutarajia mwaka 2015.
 
Back
Top Bottom