Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 89,019
- 156,726
Tafadhali ondoa ukabila.Wasukuma wawili toka kolomije na chato hawafuati katiba ya Nchi ndiyo maana Daud Bashite ana nguvu kulilko makamu wa Rais na waziri mkuu
Kama Magufuli na Makonda hawafuati katiba, kinachowafanya wasifuate katiba si Usukuma, ni akili zao.
Tuna wasukuma wengi tu waliotumikia taifa hili kwa uadilifu.
Watu kama Jaji Francis Nyalali, Mzee Paulo "Kishamapanda" Bomani, David Kidaha Makwaia, na wengine wengi sana.
Tunapokosoa mambo, tujikite kwenye hoja. Ukianza kuleta habari za ukabila, unajiondoa kwenye hoja na kujikita kwenye viroja.
Kuna wasukuma wengine wengi tu hatupendi anavyofanya Magufuli. Na tunamsema kwamba anavyofanya si sawa na mafunzo na utamaduni wa Wasukuma. Kwa mfano, Wasukuma hatujafundishwa kupiga wanawake. Magufuli anasema atapiga wapinzani wake mpaka Shangazi zao. Sasa utaona hapo, anasema hivyo kwa utashi wake tu, si kwa Usukuma.
Ondoa mawazo ya ukabila. Ukabila ni sumu itakayokutafuna na kukumaliza mwenyewe.
Sent using Jamii Forums mobile app