Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Mjane na Watoto wa Vdevram Purshotam Valambhia waliishtaki Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani.
Walitaka kulipwa dola 64,500,750 kutokana na Mkataba wa ununuzi wa vifaa vya kijeshi kati ya Kampuni ya Transport Equipment Ltd (TEL) ya Marehemu Valambhia na Serikali ya Tanzania ulioingiwa miaka ya 1980.
Kampuni ya TEL ilidai haijakamilishiwa malipo yote ya fedha zitokanazo na Mkataba. Kampuni hiyo iliamua kufungua Kesi Na. 210 ya mwaka 1989 iliyotolewa uamuzi na Mahakama za Tanzania.
Katika harakati za kudai malipo walikata rufaa katika Mahakama Kuu ya Washngton DC, na uamuzi uliotolewa na mahakama hiyo Aprili 19, 2021 umeonesha kukataliwa kwa madai yao.
==
Serikali ya Tanzania yashinda kesi ya madai ya dola za Marekani 55,099,171.66 iliyofunguliwa na familia ya Vipula D. Valambhia nchini Marekani
Serikali ya Tanzania imeshinda Kesi hii iliyofunguliwa na Familia ya Valambhia nchini Marekani. Mahakama imeona kuwa Wameshindwa kuthbitisha kuwa shughuli zinazohusisha Mkataba wa Kampuni ya Valambhia na Serikali ya Tanzania zilifanyika Marekani (suject matter jurisdiction). Tanzania itabaki...