Kweli sisi Watanzania ni watu wa kipekee hapa duniani.Hata masuala ya kesi za kisheria tunaingiza uvyama vya siasa?Sifahamu umekigusisha CHADEMA na Lissu kwa misingi gani kwenye Uzi huu!Ila ni aibu kufanya siasa za kichovu katika issues za kitaifa.
Siamini kama Wakili Msomi kama Mh.Lissu anafurahia Tanzania inavyoshtakiwa shtakiwa kwa uzembe wa watawala arrogant tuliokuwa nao tangia enzi za Tanganyika,wanaingia mikataba ya hovyo kwa niaba ya nchi na hawawezi kutimiza hizo terms kwa tamaa zao ndipo zinazaliwa kesi za ajabu ajabu.Ulikuwepo wakati Bombardier ilipozuiliwa Canada?Watawala arrogant wakataka kuficha issue waimalize kimya kimya.Unafamfahamu aliyewaambia Watanzania kuwa ndege yetu imekamatwa? Nadhani sasa Unafahamu jibu la kwa nini Mh.Lissu hafurahii Tanzania kushtakiwa Ama kuchukia Tanzania ikishinda kesi,mashindano nk.Jiongeze.