Washkaji wamejipata mimi niko vilevile

Amsaidie Kwa kumuombea!!?? ...yeye afanye kazi tu na awe na adabu ya fwedha ..wengi tunaikosea heshima Hela ...
 
Hilo kanisa lazima ni KKKT, wanatukuza sana wenye pesa.
Nadhani nyie ambao bado hamjafanikiwa mlitakiwa muombewe pia ili neema ya bwana iwashukie.
Mchungaji yeye anaombewa na nani!?? .... Ajiombee tu amkumbuke Mungu wake kila wakati inamtosha.... Akikosa mchungaji hatoombewa Daima!?? Siku hizi nao chenga tu .... Naona hata Roma napo huku kwetu kamtindo kanaanza kuota mizizi kaku"jali" wanaotoa sana sadaka na majitoleo mbalimbali michango kibao sadaka mpaka nne Misa Moja , mara mtaa wa askofu , mara ujenzi wa Jimbo kuu mara Nini yaani kidogo sadaka .... Misa zinakuwa kama harambee .....
 
Doh mimi nakula milo miwili tu mwaka mzima huu Breakfast na mchana tu
 
Watoto wetu pangu pakavu tia mchuzi wafundishwe na nani...... Afundishe na atafue Cha ziada Cha kuingiza kipato ... Kuacha kazi sio kazi ,kazi ni kutafuta kazi.
 
Waambie hao washikaji zako huo mchango waelekeze kwako badala ya huko nyumba ya ibada kwani wanaandaa mazingira ya kutozwa viingilio kila siku waingiapo ktk hiyo nyumba ya ibada.

Lkn wakikuchangia wewe na wazazi wako km wahitaji huenda baadae wewe na familia yako mkawa mnawapelekea shukurani mara kwa mara.
 
waambie chief, japo bado sijakata tamaa.
na namtumainia MUNGU
Unakataje tamaa na una ishi Bado !?? Hakuna kukata tamaaa .....hata tukitajirikia uzeeni... Wengine tupo kipindi Cha pili Cha maisha hapa kama wewe tu ...na kipindi Cha Kwanza tulishapoteza tunajitafuta kusawazisha na kushinda hii mechi .....beki zimepanda Ikibidi Hadi kipa atapanda 40's na Bado ungaunga mwana ni pasua kichwa asee...hakuna kurudisha mpira Kwa kipa ni mbele Kwa mbele mpaka kieleweke.....
 
sahihi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…