Washkaji wamejipata mimi niko vilevile

Washkaji wamejipata mimi niko vilevile

Mkuu hivi..
Mda sahihi wa kupambana na upi..?
Sijawahi fundishwa Hilo ...Kuna niliowaacha shule ya msingi wakaenda na umachinga na wengine uvuvi wapo waliotoboa wapo waliobaki nyavuni.... Kuna niliowaacha O'level yaani, Advance mpaka chuo ...wapo waliotoboa na wapo waliong'ang'aniwa.... hakuna formula mda wa mapambano ni upi..... Unapoona FURSA kanyagia hapohapo .... Wengine tulizichezea Sasa hivi tunatembea kama KAA kulia kushoto mbele Nyuma kokote Kule tunasakua kupata mlo, mavazi na watoto waende shule.. noma sana. Kama unalolote la kufanya kukuingizia kipato Anza mapema....
 
Haya maisha ukiweka expectations kubwa ni kujitesa maana unaweza usivipate abadani hadi unasepa

Fahamu msingi wa maisha ni tunapita tu, ukiwa na kidogo kuwa na expectations ndogo
Tujifunze kuthamini vidogo tulivyonavyo japo ni vikubwa tukivitafakari kwa akili
 
Uyu ana sumbuliwa na tamaa tu .uwezi kufanikiwa kwa kuwaza tu Kijana..nilkuaga kama wewe kipindi fulani kabla sija ona mawazo yanani potezea mda tu
Sasa si kawaida lazima uwaze unachotaka kufanya, kuweka plan nzuri halafu uanze kutekeleza Plan zako?? Mimi wakati naanza kazi miaka 20 iliyopita niliwaza na kuandika kwenye kijitabu changu mambo ninayoyataka niyapate kwenye maisha yangu, mfano: Kwa kuwa nilianza kazi nikiwa na Diploma niliweka lengo la kusoma digrii ya kwanza baada ya miaka 3, pia nikaweka lengo la kufungua biashara ya duka au Bar maana nilikuwa na uzoefu nazo nilioupata kwa ndugu zangu, nikaweka lengo la kununua kiwanja ili nijenge, nikaweka lengo la kununua shamba. Ajabu ni kwamba nilikuwa sina uwezo wowote wa kuwa na hivyo vitu but kila mwaka mpya ukianza yale malengo nilikuwa nayahamishia vile vile kwenye diary ya mwaka mwingine. Huwezi amini baada ya miaka 20 sasa malengo yangu yote yalitimia na kupitiliza. Nilifungua kiduka kidogo, kikakua na baadae nikapata sehemu kubwa ya duka na pembeni Bar/Grocery... Duka na bar vikaniwezesha kununua kiwanja na kuanza ujenzi na kumaliza, nikaenda chuo kwa degree na baadae masters... Nikanunua shamba ekari moja na kidogo kidogo nikawa nauziwa mara nusu ekari naunganisha, mara ekari moja naunganisha mpaka sasa nina ekari 5 na nimejenga nyumba ya shamba. My point is ni lazima uwe na malengo from the beginning ili yakuongoze hata kama itachukua miaka 20 au 30.
 
Haya maisha ukiweka expectations kubwa ni kujitesa maana unaweza usivipate abadani hadi unasepa

Fahamu msingi wa maisha ni tunapita tu, ukiwa na kidogo kuwa na expectations ndogo
Tujifunze kuthamini vidogo tulivyonavyo japo ni vikubwa tukivitafakari kwa akili
Kwamba duniani tunapita tu TUSIJENGE BARABARANI eti....🤣🤣🤣
 
Nimerudi nyumbani huu mwisho wa mwaka kama ilivyo jadi yetu tulio wengi.

Nimewakuta Baba na mama hali si shwari, nikicheki madogo all eyes on me, na mmoja anashughulikia mikopo ya elimu ya juu mwaka huu ila mambo bado tafrani.

Juzi tulivyoenda ibadani kukatokea mchango wa ujenzi na ukarabati wa nyumba ya ibada, daah washikaji wa rika yangu wamechangia mifuko ya cement 200, mmoja katoa cheque ya milioni 10 katika maongezi yake anamiliki kampuni ya clearing and forwarding huko mjini. Mwingine kaahidi tipa 20 za mchanga.

Hakika ibada ilifaana sana, mchungaji aliwaita wazazi wa wale washikaji pale madhabahuni na kutamka kwamba hakika mumezaa chema sana na MUNGU amebariki uzao wenu.

Hali ile ilinifanya nijiulize maswali yasiyo na mwisho kuhusu hatma ya maisha yangu pamoja na wazazi wangu.

Mungu why najitafuta lakini sijipati? Dunia hii ni ya wachache? Wazazi wangu wataishi katika umasikini huu wa kutisha hadi lini?

wakati narudi nyumbani na mama yangu kwa mguu, nikawa napitwa na wana wakiwa kwenye tinted za Black athlete crown, Ford ranger, Subaru nk, wakati mimi naendelea kupita kando ya barabara kukwepa tope la mvua hizi.
Usiangalie vya wenzako kuwa wamepata tayari ujui wametumia njia ipi isitoshe bado we nikijana. Ni kuangalia unakosea wap unarud upya. We elewa ambao tunajitafuta tupo wengi sana. Na kujipata ni juudi zako na kuomba Mungu
 
Sasa si kawaida lazima uwaze unachotaka kufanya, kuweka plan nzuri halafu uanze kutekeleza Plan zako?? Mimi wakati naanza kazi miaka 20 iliyopita niliwaza na kuandika kwenye kijitabu changu mambo ninayoyataka niyapate kwenye maisha yangu, mfano: Kwa kuwa nilianza kazi nikiwa na Diploma niliweka lengo la kusoma digrii ya kwanza baada ya miaka 3, pia nikaweka lengo la kufungua biashara ya duka au Bar maana nilikuwa na uzoefu nazo nilioupata kwa ndugu zangu, nikaweka lengo la kununua kiwanja ili nijenge, nikaweka lengo la kununua shamba. Ajabu ni kwamba nilikuwa sina uwezo wowote wa kuwa na hivyo vitu but kila mwaka mpya ukianza yale malengo nilikuwa nayahamishia vile vile kwenye diary ya mwaka mwingine. Huwezi amini baada ya miaka 20 sasa malengo yangu yote yalitimia na kupitiliza. Nilifungua kiduka kidogo, kikakua na baadae nikapata sehemu kubwa ya duka na pembeni Bar/Grocery... Duka na bar vikaniwezesha kununua kiwanja na kuanza ujenzi na kumaliza, nikaenda chuo kwa degree na baadae masters... Nikanunua shamba ekari moja na kidogo kidogo nikawa nauziwa mara nusu ekari naunganisha, mara ekari moja naunganisha mpaka sasa nina ekari 5 na nimejenga nyumba ya shamba. My point is ni lazima uwe na malengo from the beginning ili yakuongoze hata kama itachukua miaka 20 au 30.
Dhahabu tupu
 
hapa nimeokota kitu
 
Nimerudi nyumbani huu mwisho wa mwaka kama ilivyo jadi yetu tulio wengi.

Nimewakuta Baba na mama hali si shwari, nikicheki madogo all eyes on me, na mmoja anashughulikia mikopo ya elimu ya juu mwaka huu ila mambo bado tafrani.

Juzi tulivyoenda ibadani kukatokea mchango wa ujenzi na ukarabati wa nyumba ya ibada, daah washikaji wa rika yangu wamechangia mifuko ya cement 200, mmoja katoa cheque ya milioni 10 katika maongezi yake anamiliki kampuni ya clearing and forwarding huko mjini. Mwingine kaahidi tipa 20 za mchanga.

Hakika ibada ilifaana sana, mchungaji aliwaita wazazi wa wale washikaji pale madhabahuni na kutamka kwamba hakika mumezaa chema sana na MUNGU amebariki uzao wenu.

Hali ile ilinifanya nijiulize maswali yasiyo na mwisho kuhusu hatma ya maisha yangu pamoja na wazazi wangu.

Mungu why najitafuta lakini sijipati? Dunia hii ni ya wachache? Wazazi wangu wataishi katika umasikini huu wa kutisha hadi lini?

wakati narudi nyumbani na mama yangu kwa mguu, nikawa napitwa na wana wakiwa kwenye tinted za Black athlete crown, Ford ranger, Subaru nk, wakati mimi naendelea kupita kando ya barabara kukwepa tope la mvua hizi.
Sometime kubali kutojifananisha na mtu. Jali mipango yako na sali saana na pambana saana ipo siku utasimama vizur. Japo kutoboa juhudi pekee hazitoshi lazima sometime uwe fala
 
Back
Top Bottom