Washkaji wamejipata mimi niko vilevile

Washkaji wamejipata mimi niko vilevile

Mchungaji yeye anaombewa na nani!?? .... Ajiombee tu amkumbuke Mungu wake kila wakati inamtosha.... Akikosa mchungaji hatoombewa Daima!?? Siku hizi nao chenga tu .... Naona hata Roma napo huku kwetu kamtindo kanaanza kuota mizizi kaku"jali" wanaotoa sana sadaka na majitoleo mbalimbali michango kibao sadaka mpaka nne Misa Moja , mara mtaa wa askofu , mara ujenzi wa Jimbo kuu mara Nini yaani kidogo sadaka .... Misa zinakuwa kama harambee .....
Ha haa kwa kweli mimi nimeshaacha kutegemea kuombewa. Naomba kivyangu inatosha.
Nikienda church nabeba sadaka moja tu iliyo ndani ya uwezo wangu. Hizo sadaka nyingine wala sishtuki kujilazimisha kutoa.
 
Nanukuu

"Hakika ibada ilifaana sana, mchungaji aliwaita wazazi wa wale washikaji pale madhabahuni na kutamka kwamba hakika mumezaa chema sana na MUNGU amebariki uzao wenu."

"Mungu why najitafuta lakini sijipati? Dunia hii ni ya wachache? Wazazi wangu wataishi katika umasikini huu wa kutisha hadi lini?"

wakati narudi nyumbani na mama yangu kwa mguu, nikawa napitwa na wana wakiwa kwenye tinted za Black athlete crown, Ford ranger, Subaru nk, wakati mimi naendelea kupita kando ya barabara kukwepa tope la mvua hizi.
By Objective football


Mwisho wa kunukuu
 
Ukitaka kufanikiwa ukiwa Afrika hasa Tanzania lazima uwe mkwepa kodi, mhujumu uchumi, mbadhirifu, mla rushwa na upige madili ya michongo.

Watanzania wengi ni wanafiki sana, Hapa utasikia wengi wanasema mara oooh! Pambana lakini nyuma ya pazia wengi ni wahujumu uchumi..

Walio fanikiwa kihalali barani Afrika ni wachache sana kulinganisha na wengi waliofanikiwa kwa wizi wizi na janja janja.

Mifumo ya kiafrika automatically imekaa kiupigaji.
 
Back
Top Bottom