Washkaji wamejipata mimi niko vilevile

Washkaji wamejipata mimi niko vilevile

Binidamu tumeumbwa kuhangaika na kuzoea. Wewe ndugu yangu hauna umasikini bali umeizoea hali uliyonayo. Ukikizoea kitu au hali unaiona ya kawaida sana na mwishowe haina thamani. Na akili yako ikikosa kuchangamka inatafuta changamoto mwishowe unatafuta kasoro kwenye mahali ambapo hamna kasoro. Unachotakiwa kufanya ni kuamka na kupambana mpaka uzoee kupambana na ubadilike. Kuna watu wamezoea ku hustle mpaka wakikaa siku moja tu nyumbani wanaumwa. Ukishazoea kupambana hautochoka maana utakuwa umeshazoea hali ya kutafuta na kuwajibika. Maana akili zetu zimeumbwa zichakarike na zizoee vitu vipya kila siku. Jilinganishe na wewe wa jana yako usijilinanishe na mtu mwingine. Jiulize kama Bakhresa angekuwa anajilinganishe na wapemba wenzie angekuwa tajiri mkubwa leo hii. Maana kumiliki mjengo Masaki tu angeridhika na si kuongeza boti za Azam au kumiliki timu za mpira wa miguu. Jizoeshe kujifunza kitu kipya kila siku na pia jikubali na usikate tamaa. Pambana ukipiga hatua kidogo jiüpongeze kidogo then rudi katika kupambania ugali. Usibweteke ukapiga hatua kidogo halafu ukajiachia. Pumzika kidogo halafu rudi kupambania ugali. Mungu akubariki na akulinde katika upambanaji.

Namuunga mkono kwa asilimia mia moja huyu mwanajamii maana amenisaidia kuifafanunua pointi zangu hapo juu.
sahihi chief
 
Kuna mshkaji amejipata sanaaa,nikimwomba ani assist kidogo anasema hamna shida but hakuna utekelezaji.Ila kila siku ni kunisimulia nimenunua hiki,kile n.k. tena kwa gharama kubwaaa.

Na mimi naomba msaada kidogo tu.Hamna shida na mimi napambana ipo siku yangu.
 
Kuna mshkaji amejipata sanaaa,nikimwomba ani assist kidogo anasema hamna shida but hakuna utekelezaji.Ila kila siku ni kunisimulia nimenunua hiki,kile n.k. tena kwa gharama kubwaaa.

Na mimi naomba msaada kidogo tu.Hamna shida na mimi napambana ipo siku yangu.
wana wana nunua vitu kwa bei chafu. huku washkji ambao maisha yametuegemea awatupi hta Abc za kutokea.

zaidi zaidi,anakumbushia stori za mademu zetu wa zamani
 
Nimerudi nyumbani huu mwisho wa mwaka kama ilivyo jadi yetu tulio wengi.

Nimewakuta Baba na mama hali si shwari, nikicheki madogo all eyes on me, na mmoja anashughulikia mikopo ya elimu ya juu mwaka huu ila mambo bado tafrani.

Juzi tulivyoenda ibadani kukatokea mchango wa ujenzi na ukarabati wa nyumba ya ibada, daah washikaji wa rika yangu wamechangia mifuko ya cement 200, mmoja katoa cheque ya milioni 10 katika maongezi yake anamiliki kampuni ya clearing and forwarding huko mjini. Mwingine kaahidi tipa 20 za mchanga.

Hakika ibada ilifaana sana, mchungaji aliwaita wazazi wa wale washikaji pale madhabahuni na kutamka kwamba hakika mumezaa chema sana na MUNGU amebariki uzao wenu.

Hali ile ilinifanya nijiulize maswali yasiyo na mwisho kuhusu hatma ya maisha yangu pamoja na wazazi wangu.

Mungu why najitafuta lakini sijipati? Dunia hii ni ya wachache? Wazazi wangu wataishi katika umasikini huu wa kutisha hadi lini?

wakati narudi nyumbani na mama yangu kwa mguu, nikawa napitwa na wana wakiwa kwenye tinted za Black athlete crown, Ford ranger, Subaru nk, wakati mimi naendelea kupita kando ya barabara kukwepa tope la mvua hizi.
🤣🤣🤣🤣🤣🤣😂😂😂😂 Kama una Afya endelea kupambana ila Kwa kuwa uko weak emotianally ni vyema ukawa mbali na hao Jamaa na kwenu pia ikibidi usiende hata huko kanisani maana utakuja kujitundika Bure kisa ujinga wa kujilinganisha na kujikataa.

Mwisho kama kweli mchungaji wenu aliyasema hayo maneno Sina neno jingine zaidi ya kumwita mpumbavu.
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣😂😂😂😂 Kama una Afya endelea kupambana ila Kwa kuwa uko weak emotianally ni vyema ukawa mbali na hao Jamaa na kwenu pia ikibidi usiende hata huko kanisani maana utakuja kujitundika Bure kisa ujinga wa kujilinganisha na kujikataa.
ufukara ni fedheha, hauvumiliki
 
Back
Top Bottom