Orodha hiiya matokeo ya leo kuna wavulana watatu pekee
๐๐๐ง๐๐๐ฎ๐ง๐ณ๐ข ๐๐ ๐๐จ๐ซ๐ ๐ค๐ข๐ญ๐๐ข๐๐ ๐๐๐๐ ๐ค๐ข๐๐๐ญ๐จ ๐๐ก๐ ๐ฌ๐ข๐ญ๐
1. Catherine Alphonse Mwakasege (PCB) โ St. Maryโs Mazinde Juu Tanga.
2. Lucy Magashi (PCB) Shule ya St. Maryโs Mazinde Juu Tanga.
3. Mhewa Charles Kamando (PCB) โ Tabora Boys
4. Minaeli Simon Mgonja (PCB) St. Maryโs Mazinde Juu Tanga.
5. Norah Eliaza Kidijoiti (PCB) โ Shule ya St. Maryโs Mazinde Juu Tanga.
6. Jennifer Martin Chuwa (PCB) St. Maryโs Mazinde Juu Tanga
7. Paulina Aldephonce Mabamba (PCM) St. Maryโs Mazinde Juu Tanga.
8. Rachel Joachim Moshi (PCM) St. Maryโs Mazinde Juu Tanga
9. Kurwa Mbizo Elias (PCB) Tabora Boys
10. Oscar Eliakimu Marabe (PCB) Tabora boys
Huko tunakokwenda kuna hatari kubwa sana duniani. Wanawake wanapigiwa debe sana kupitia kiasi,
. Sasa serikali nyingi hasa za Kiafrika zimeweka mkazo mkubwa sana kwa ajili ya kuendeleza wasichana. Sikatai kwa ukweli kwamba wanawake wamedhulumiwa sana tokana na fumo dume. Ila hatari ninayoiona ni juu ya watoto wa kiume kuwa dhaifu mbele ya wanawake. Hii imetokana na kisaikolojia wanaume, kisaikolojia wako dhaifu au kutishika upesi na pengine kufanya pungufu ya wajibu wake kama mwanaume. Wanawake kwa kawaida ni washindani wakubwa wa madaraka na pia ni washawishi wakubwa. Ukiangalia hata katika ndoa mwanamke ana nguvu kubwa sana ya ushawishi akitaka yeye atawale kwa sehemu kubwa ya maamuzi. Familia ambazo zinakaa vizuri asilimia kubwa mwanamke ndio msimamizi mkubwa wa pesa pale nyumbani. Kwa kuwa amepewa hayo madaraka. Mwanaume akifanya hivyo haaminiki. Mfano kuna familia moja anayetoa pesa yote ya matumizi nyumbani na kusomesha watoto ni mwanaume, lakini pamoja na hayo mwanamke anataka ahusike na pesa ya mume wake ambayo inafikirika inatumika visivyo, huku mwanamke anakazi yake na hachangii lo lote kwa familia. Wala hamhusishi mume wake na matumizi ya pesa yake. Lakini bado anataka pesa ya mume wake kwa kila kitu.
Sasa kuna mpango wa kujenga shule za sekondari kila mkoa kwa ajili ya wanawake tu, wakati shule mchnaganyiko na huko wamo. Mwisho itakuwa ni nini?
Tuwaendeleze wanawake lakini tusisahau kuwaendeleza watoto wa kiume. Hii itachangia kuongezeka kwa kuvunjika ndoa na pia watu kutooa kabisa. Tukumbuke kwamba mwanaume ndiye kiongozi wa nyumba hata kama mwanamke atakuwa na PHD.
Nchi zinazoendelea wanakazia tuweke idadi ya wanwake sawa na wanaume kwenye uongozi. Nchi gani imefanya hivyo tangu kuumbwa kwa ulimwengu, angalia Marekani, Uingereza, Ujerumani nk, ipi ina idadi sawa ya viongozi katika yao? Je, wanawake wasiwe viongozi sio maana yake, bali tusilazimishe mwanamke awe kiongozi kwa sababu tunataka kuweka usawa wa kijinsia kwenye uongozi.
Maana yangu tuwaendeleza wanaume lakini tusifanye kwa kutojali uhalisia wa maisha.